Kayoko ni mwamuzi mbovu ila kwenye hii derby kila timu imeathirika na maamuzi yake ya ovyo tofauti na Simba wanavyoona ni wao pekee

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Ukipita mitandaoni na mitaani, utaona wanasimba wanalalamika wameonewa na mwamuzi sababu kubwa zao ni 1) wamenyimwa penati mbili za Kibu, na faulo iliyozaa goli haikuwa faulo ya maana.

Kwenye swala la penati ambayo ni halali ni moja tu na sio mbili kama inavyodaiwa. Ile moja ni faulo iliyochechezwa nje ya kumi na nane ila Kibu akadondekea ndani ya 18 hivyo ni maamuzi sahihi refa kuweka faulo. Kwenye swala la penati alkadharika Yanga walinyimwa penati baada ya Camara kucheza miguu ya mchezaji wa Yanga badala ya mpira.

Hamza alikuwa ni mtu wa mwisho, na Dube alikuwa ameshamuacha kwa mbio, ila akamua kung'ang'ania jezi ya Dube tukio ambalo kisheria alipaswa kula kadi nyekundu moja kwa moja.
Sasa mkimlamikia Kayoko, mkumbuke na msaada wake kwenda upande wenu wa Simba maana amewasaidia pia.
 
Makosa ya waamuzi yako kote duniani
Hata tukupe wewe filimbi
Hukosi kufanya makosa

Kuna waamzi wana technology Bado wanafanya makosa
 
Yanga waliathirika na maamuzi ya Hamza kutopewa red card na Simba kunyimwa penati moja. Aucho akicheza sana rafu Ila alipewa kadi ya njano.
Kwa kifupia refa lazima alaumiwe yeye alitakiwa afate Sheria 17 na sio kubalance maamuzi.
 
Kumbe kubalance pia ni tatizo,
Baada ya Kayoko kutangazwa kwamba atakuwa muamuzi, wadau walimjadili kwamba ana utaratibu wa kubalance timu tabia ambayo Kayoko inatakiwa aiache
 
ATleast sasa wa Tz tunaelimika na kujadili mambo kistaarabu bila kutukanana. Well done wote.

Kayoko, Kayoko, Kayoko jiangalie
 
Yanga waliathirika na maamuzi ya Hamza kutopewa red card na Simba kunyimwa penati moja. Aucho akicheza sana rafu Ila alipewa kadi ya njano.
Kwa kifupia refa lazima alaumiwe yeye alitakiwa afate Sheria 17 na sio kubalance maamuzi.
Debora alicheza sana rafu na hakupewa kadi unakumbuka?
 
Kabla ya mechi kuchezwa, wengine tulipinga mechi kupewa huyo dogo Kayoko! Na binafsi nilimtofautisha na Tatu Malogo kwa jinsia tu!! Ila hamkunielewa!

Baada ya mechi, eti mnaanza kulalamikia jambo lile lile!! Hapa muhimu Yanga imeshinda tu. Full stop. Yanga oyeee!! 💚💛💪
 
Yanga waliathirika na maamuzi ya Hamza kutopewa red card na Simba kunyimwa penati moja. Aucho akicheza sana rafu Ila alipewa kadi ya njano.
Kwa kifupia refa lazima alaumiwe yeye alitakiwa afate Sheria 17 na sio kubalance maamuzi.
Mchezaji wenu deborah fernandez amecheza faulo nyingi lakin hata kadi moja hajapewa
 
Kabla ya mechi kuchezwa, wengine tulipinga mechi kupewa huyo dogo Kayoko! Na binafsi nilimtofautisha na Tatu Malogo kwa jinsia tu!! Ila hamkunielewa!

Baada ya mechi, eti mnaanza kulalamikia jambo lile lile!! Hapa muhimu Yanga imeshinda tu. Full stop. Yanga oyeee!! 💚💛💪
Ile mechi ya ngao ya jamii alikataa magoli mawili ya Yanga na baadae akakataa penalty ya simba ya wazi dakika za mwishoni na alifanya vile ili abalance baada ya kuwanyima magoli mawili ya wazi

Hizi mechi zinamfaa Ahmed Arajiga sababu yule kwenye white anasema hii ni white na kwenye black anasema hii ni black hanaga mambo ya kubalance
 
Yanga waliathirika na maamuzi ya Hamza kutopewa red card na Simba kunyimwa penati moja. Aucho akicheza sana rafu Ila alipewa kadi ya njano.
Kwa kifupia refa lazima alaumiwe yeye alitakiwa afate Sheria 17 na sio kubalance maamuzi.
mwacheni refa hajosoma chemistry hajui balance equations
 
Unazi upi yaani simba mnahisi nyie ndo mnaonewa huku mechi mechi vs azam magoli yote mawili ni ya offside
Acha unazi bhana, huwezi kuwa sahihi wewe peke yako. Public participation yote inaonesha mwamuzi aliiumiza Simba. Hayo ya azam ungeyaongea kipindi hicho.
 
Hamza alitakiwa apewe redcard baada ya kumchezea rafu dube dakika ya 50 ila alipewa yellow card
 
Back
Top Bottom