Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kama ulidhani hii kesi ni lelemama basi unapaswa kujitafakari upya , wakati baadhi ya mamluki wakishangilia kutupwa kwa pingamizi lililohoji uhalali wa Mahakama ya uhujumu uchumi na rushwa kusikiliza kesi ya Ugaidi, Mawakili wa Mbowe wameweka pingamizi ambalo wasomi wengi walikuwa wanalisubiri, la KUPINGA HATI YA MASHITAKA KUTOKIDHI VIGEZO NA MASHARTI YA KISHERIA, kukosewa kwa hati hii kunatokana na uwezo mdogo na umbumbumbu wa Wanasheria wa serikali ,mara zote imesemwa sana kuhusu uwezo wa watu hawa.
=====
Leo Septemba Mosi, 2021 Mawakili upande wa utetezi wameweka pingamizi lingine kuhusu hati ya mashtaka, wamedai kuwa imekosa vigezo vya kisheria na upande wa Serikali wameomba Ijumaa Septemba 3, 2021 kuja na majibu.
Mahakama hiyo imeridhia ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Ijumaa.