Kazi gani ukiifanya lazima kichwa kiwake moto?

Kazi gani ukiifanya lazima kichwa kiwake moto?

Hiyo busainess ni ngumu sana japo ni ya kuweka bond kitu akishindwa kulipa inakupa kazi ya kutafuta mteja wa kununua iyo bond ili uambulie hela yako japo unaweza kupata hasara
Ni changamoto kwelikweli
 
Habari wakuu

Kuna biashara ukizifanya lazima akili kidogo icheze, uwe kama dish limeyumba hivi!

View attachment 3308644

Biashara gani ulishawahi kuifanya ukahisi kabisa kichwa kinawaka moto! Sio kwamba unamwa ila tu kwa uzito,ugumu na changamoto za biashara yenyewe.

Hii haikuwa biashara rasmi ila nilipomaliza Form four enzi za Covid 19 niliwahi kutembeza tangawizi mitaa ya Liberty, Makoroboi, Soko kuu, na Dampo (Mwanza) nachukua tangawizi asubuhi kwa walanguzi wa magunia.

Nachukua kwenye mfuko mdogo napunguza natunza zingine sehemu, zingine napanga kwenye ungo, nikimaliza nazirudia zilizobaki mpaka ziishe, ilikuwa noma sana make wauzaji tu wengi hapo nina Tangawizi za elfu 10 au 20 niuze ziishe.

Nikimaliza jioni naubikia kwa rafiki yangu, tunaenda kwa mama mmoja hivi (jina nalihifadhi), anatupa deli na chupa za chai tunatembeza chai na maandazi saa nne hivi tunakuwa nimemaliza, siku zingine mpaka saa5 .

Nilijifunza mambo mengi ila kichwa kilikuwa kinawaka moto sometime kwa kauli za wateja na msoto wa town jua kali,kuchoka, na mahesabu kuvurugika.

Itaendelea kuhusu biashara zingine...

Heshima mbele,
Wenu Nomadix.
Hakuna biashara ngumu kama ya kukopesha hela ile sio isee.. kuna siku nilimkopesha mteja laki 3 na nusu tu.. baada ya kama siku tatu nikamgumia jamaa yupo na bag stand ameshakatiwa na ticket ya katesh oya sio poa..
 
Back
Top Bottom