Kazi gani ukiifanya lazima kichwa kiwake moto?

Kazi gani ukiifanya lazima kichwa kiwake moto?

Habari wakuu

Kuna biashara ukizifanya lazima akili kidogo icheze, uwe kama dish limeyumba hivi!

View attachment 3308644

Biashara gani ulishawahi kuifanya ukahisi kabisa kichwa kinawaka moto! Sio kwamba unamwa ila tu kwa uzito,ugumu na changamoto za biashara yenyewe.

Hii haikuwa biashara rasmi ila nilipomaliza Form four enzi za Covid 19 niliwahi kutembeza tangawizi mitaa ya Liberty, Makoroboi, Soko kuu, na Dampo (Mwanza) nachukua tangawizi asubuhi kwa walanguzi wa magunia.

Nachukua kwenye mfuko mdogo napunguza natunza zingine sehemu, zingine napanga kwenye ungo, nikimaliza nazirudia zilizobaki mpaka ziishe, ilikuwa noma sana make wauzaji tu wengi hapo nina Tangawizi za elfu 10 au 20 niuze ziishe.

Nikimaliza jioni naubikia kwa rafiki yangu, tunaenda kwa mama mmoja hivi (jina nalihifadhi), anatupa deli na chupa za chai tunatembeza chai na maandazi saa nne hivi tunakuwa nimemaliza, siku zingine mpaka saa5 .

Nilijifunza mambo mengi ila kichwa kilikuwa kinawaka moto sometime kwa kauli za wateja na msoto wa town jua kali,kuchoka, na mahesabu kuvurugika.

Itaendelea kuhusu biashara zingine...

Heshima mbele,
Wenu Nomadix.
Kazi yakuchakata mbususu. Yaani hadi nachanganyikiwa
 
Hakuna biashara ngumu kama ya kukopesha hela ile sio isee.. kuna siku nilimkopesha mteja laki 3 na nusu tu.. baada ya kama siku tatu nikamgumia jamaa yupo na bag stand ameshakatiwa na ticket ya katesh oya sio poa..
Hahahah famasiala nini, watu washapanga mipango kitambo, duh lazima kichwa kiwake moto aisee
 
Kwanini usingechukua chupa ya chai ya nyumbani kwenu ukaanza kuuza chai mwenyewe kuliko kwenda kuajiriwa kuuza chai?
 
Watu wa huku madeni hawaogopi??,. Kwanza hata ukiwapeleka mahakamani hamna kitu utapata maana wanakuja kusikiliza kesi wakiwa wameshatoka kuoga madawa hakimu hamna kitu ataamua😂😂😂😂
Duh huko hatari...ha2ana madawa ya kumfanya mshangazi akio e billionea wakati huna kitu
 
Kwanini usingechukua chupa ya chai ya nyumbani kwenu ukaanza kuuza chai mwenyewe kuliko kwenda kuajiriwa kuuza chai?
Wa kutengeneza hayo maandazi sasa na chai maana nimekulia kwa aunt, yeye muda mwingi hayupo wapo binamu zangu wadogo, aunt yeye anarudi usiku saa2 au 3.
 
Back
Top Bottom