KAZI INAENDELEA! VIJIJI 28, WANANCHI 20,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA UMWAGILIAJI MKOMAZI, KOROGWE TANGA

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
KAZI INAENDELEA! VIJIJI 28, WANANCHI 20,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA UMWAGILIAJI MKOMAZI, KOROGWE TANGA

Mradi wa Mkomazi ni wa kihistoria, kwani ulianzishwa zaidi ya miaka 50 iliyopita lakini utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu na Sasa unatekelezwa kikamilifu chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mradi unatarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 20,000 kwenye vijiji 28 vya kata saba za Mkomazi, Mkumbara, Mazinde, Mombo, Chekelei, Makuyuni, na Magila Gereza.

Mradi wa Mkomazi unakadiriwa kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 18 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 2025.
 

Attachments

  • VID-20250224-WA0097.mp4
    14.6 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…