Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
-
- #21
Watu wengine ambao hata hawauangalii mlango wa jela na wanatajirika ni wacheza mpira na wanasiasa.
Hayo ya kuwahi kuvunja sheria kwa namna moja au nyingine yamkini ni kubwa kwa matajiri wengi.
Ila la uganga na uchawi mimi nadhani linawahusu wachache sana.
Si kweli ndumba ni imani, pana watu wanamiliki zaidi ya b kadhaa au utajiri bila ndumba wengi tu. Utajiri ni akili, utajiri ni tabia na umasikini ni tabia pia. Utajiri wa kichawi na utajiri wa kiMungu ni 50 kwa 50.
Unaweza ukapata utajiri kwa Mungu au Shetani.
Katika kitu nakubaliana na wewe ni hapo kwenye tabia, asikwambie mtu tabia na utamaduni wa mtu ama familia na ndugu zake zina mchango mkubwa sana katika kufanya wafanikiwe ama wafeli.Kwema Wakuu!
Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.
Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.
Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.
Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.
Hiyo ni kanuni ya Kidunia,
Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.
Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi.
Wala hata serikali isiwe na time na wewe.
Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.
Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.
Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.
Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria"
Nikabaki namkodolea macho tuu!
Nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
Ni mil 500 au Bil 500? Yaan kupata tu mil 500 mpaka uchawi?
Waambie haoMsuva ana bilioni moja na kaipata hapa hapa Africa. Haya hilo wasemaje?
Mark Zuckerberg alienda kulala polisi mara ngapi wakati akipambana kuisimika facebook yake?
Sheria zimetungwa Ili kuwadhibiti masikiniNa sheria Kwa sehemu kubwa zipo Kama chujio tuu
Mzee wa fasihi unaweza ukamiliki pesa nyingi bila ndumba mfano fanya biashara ya real estate jiingize biashara za kuuza viwanja utapata b za kutosha, panda miti eka 20 au zaidi baada ya miaka 12 utapata b za kutosha.
Bahati unaivuta uhitaji mganga wala ushirikina.Shida wengi Wana ni vipofu kuhusu elimu ya roho.Mkuu hiyo ni rahisi mdomoni, lakini pesa sio Maneno.
Kila kitu kinahitaji Bahati"Nyota"
Hata ukienda kulima nini kama huna Nyota hakuna utakachoambulia.
Na hapo ndipo Uchawi unapoingia Kwa wengi
Usigeneralize labda sababu matajiri wengi hawana utamaduni wa kuandika historia zaoππππ
Usijidanganye Mkuu.
Alafu wenye akili hawanaga Utajiriππ
Mtu akishakuwa na akili kamwe hawezi kuwa Tajiri labda akili ya kawaida lakini kama unamaanisha Akili nyingi basi utakuwa unakosea.
Kwa hapa Afrika hakuna Tajiri wa hivyo
Songilo puruHawa watu wanaoandika wanatumia nini kufikiria