kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Waliotuletea dini zetu hizi mbili waliambatana na wakoloni kwenye mapito yao. Waliabu na kuimba kwa furaha pamoja na wakoloni. Sisi wageni tulifundishwa kusema na kuamini kuwa tuheshimu mamlaka maana mamlaka zinatoka kwa Mungu. Yaani hata mamlaka za wakoloni wetu pia zilitoka kwa Mungu hivyo kazi ya dini ni kuabudu na kusifia ukubwa na uzuri wa Mungu na Serikali kwetu.
Kama serikali za wakoloni zilitoka kwa Mungu je serikali za Africa na Tanzania kwanini ziwe tofauti huko makanisani na misikitini? Ni lini vitabu vyetu vya dini viliandikwa upya kuondoa maneno hayo? Kama watanzania tuliweza kuimba mapambio na kupiga vinubi kuwasifia viongozi wa serikali za wakoloni ambao walikuwa wanatupora mali zetu kupeleka kwao iweje iwe vigumu kuwaimbia viongozi wetu wanaosambaza maji, umeme, shule, hospitali kwa wananchi wao?
Dini hizi ni social construction tu, ndio maana Kuna mataifa kama China dini hizi sio sana lakini mambo yao hayakwami. China hakuna misikiti na makanisa na ufufuo na uzima lakini China ni taifa kubwa sana kwenye uso wa dunia. India dini kuu ni Hindu lakini India ni taifa kubwa duniani.
Hoja yangu, nyumba za ibada zifanye kazi ya kuimba na kuabudu tu na kazi ya siasa na haki ibaki kwa wabunge, serikali na mahakama. Ilikuwa hivyo zamani na ibaki hivyo hata Leo kwa ustawi wa jamii yetu.
Kumtishia mkuu wa nchi kuwa utakufa, utaugua, utaanguka, nk kwenye nyumba za ibada ni kutumia dini vibaya.. Ukweli hatima ya mahubiri kama hayo itategemea na akili na busara za Rais na waliomzunguuka. Usisahau kuwa askofu na sheikh ni raia pia.