KUCHUNGA NG'OMBE
Ilikua Arusha,nilimwambia jamaa flani anitaftie kazi Nilimkuta tu analinda nyumba 1 hivi, nikamuelezea shida yangu ya kazi akaniambia nimpitie kesho atakua ana jibu. basi nikaondoka.
Kesho yake nikarudi,akaniambia imepatikana kazi ya kuchunga ng'ombe unaweza? nikamwambia ukweli sijawahi kuchunga ng'ombe,akanaiambia sio kazi utaelekezwa tu sehemu ya kuwapeleka kwenye malisho kisha unaangalia wasiende kwenye mashamba ya watu.
nikakubaliana nae, akaniambia utakua unakaa hapo hapo (nikafurahi sana) misoto yangu yote guys mimi pakulala huwa sinaga sijawambia ila (ni siri yangu ntawambia kwenye thread zingine) nikisema naenda home huwa naendaga wapi.
Basi bana tutoke huko, nilipoambiwa ntakua nalala hapo hapo nikafurahi sana nikajua hapa nitakua nimepga ndege wawili kwa jiwe 1, yani ntakua nime solve tatizo la msosi na pili ntakua nimepata sehemu ya kuishi.
Basi jamaa akaniambia itabidi leo tushinde wote hapa ili badae nikitoka hapa nikupeleke,nikamwambia hamna shida tukashinda wote hiyo siku usiku mzma asubuhi yake tukatoka akanipeleka kwa boss, ni Muarusha yule mzee.
Nikafika nikakaribishwa mchana muda wa kula ukafika wakaleta "loshorooo" Hili ni jina la chakula cha kimasai/waarusha huchanganya maindi na maziwa fresh sjui, nikaletewa, kiukweli sikiwezagi mimi hiki kitu muda mrefu tu.
Nakijua maana mimi ni "mkazi wa arusha" hivyo naijua kabisa Loshoroo na siiwezi nishaitest nikatapkaga,basi ilivyoletwa nikapewa Nikawambia Hapana niko vizuri nimeshba kabisa, Hapo sijala nmesema hivyo nikivuta muda wa usiku watapka aina ingine ya chakula ntakula,basi jioni jioni akaja kijana wa huyo mzee akaniambia twende anipeleke sehemu wanazolisha akanionyeshe na njia ya kupitisha ng'ombe.
Tukaondoka tunatembea nakunywa maji tu ku clear njaa,nina hasira kulia nataka sina wakumlilia basi tukaenda akanionyesha tukarudi, Usiku ukafika nikasubiri msosi nione nini kitapkwa ili nile, Muda wa kula umefika
naletewa tena Loshoroooo, yewoomiiiiiiiiii... ki ukweli hiyo siku nilijua nini maana ya maisha ni safari ndefu, nikasema hapa sina namna acha nijaribu tu ntafanyaje sasa,kupga tu mdomoni Nikarudsha chenchi tapikaaa sanaaaa, hadi nikawashtua wenyeji, wakaniuliza vipi unaumwa? nikawambia hapana...
Akatokea mtoto wa kike wa huyo mzee ni mkubwa kbsa kama mmama akasema mtengenezeeni uji hebu, kimoyo moyo nikasema ashukuriwe Mungu, uji ukatengenezwa nikaona wanataka kuweka maziwa kwenye UJI, Nikawambia hapana Hapana usiweke maziwa "wamasai na maziwa sijui wana nini",basi nikatengenezewa uji nikaupiga wote,Usiku ukaisha kwa usalama.
Kesho yake kazn sasa,natakiwa kutoa ng'ombe kwenda kuchunga,Kijana ninaetakiwa kwenda nae kama mwenyeji wangu mjukuuu wa huyo mzeee "katoroka" kaenda kucheza huko,basi nikaambiwa niende tu kuchunga maana jana si nilishaonyeshwa pakuwapeleka.
Nikiwa natoa ng'ombe zizini naona maandalizi ya Loshorooo ya mchana ikiandaliwa,maana yake nikirudi kuchunga nakutana na loshoroo,sawa nikatoa ng'ombe na fimbo yangu nikawa na wa swaga mdogo mdogo,naongea nao road "nyieee rudi huku" tandika sana fimbo ng'ombe viburi kweliii wanahangaika haoooo
Nikafika eneo la kulisha nikawaacha wakawa wanaendelea kula,hapo kurudsha ng'ombe ni jioni,kumbuka nimeamka asubuhi sijala kitu,nmekaaa pale uwanjan nawaangalia ng'ombe, nililia sana hiyo siku,Nililia mpaka kwikwi..
kama ni sikuweza jinyonga ile siku hapa duniani hamna kitu itafanya niondoe uhai wangu tena,ni moja ya siku nilikaa nikijitafakari sanaaa maisha haya mpaka lini,shida hizi mpaka lini, Naendelea kuwaza ila njaa inauma nikaona mimi ninapoelekea ntachinja ng'ombe wa watu nile nyama.
Nikaamka nikajinyooosha nikifkiria nkirudi home nakutana na loshorooo tena Hapana siwezi, nikatupa fimbo kuleee nikawaaga ng'ombe (nikawambia wanangu leo mtarudi wenyewe home) Nikapita na hamsini zangu, mimi huyooooo.... (huko nyuma sijui kilichoendelea) ila kuchunga kukaishia hapo..
Mshahara niliahidiwa 20,000 kwa mwezi, niliukubali kabisa ila kazi ikawa sio riziki.