Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Kuna mahali umesoma nimeandika nilikua naishi home?

unahisi ninavyondika nimeacha nikarudi home unahisi ni

nyumba yenye ma AC geti kali cctv camera,nk sio mkuu?!

Huu ni uzi wa kazi "zilizonishinda tu" nikikwambia nilipokua nalala

nadhani habari ya kazi itafunikwa,ila fahamu tu kwamba mapito

yote hayo nimeyapitia nikiwa mikononi mwa DUNIA na wala si wazazi wala ndugu.

Vishu Mtata
 
Pole sana jamaa..hizo kazi ngumu zinahitaji uzoefu na mwili wenye afya..manake pia hao majamaa wanakula sana hawali chakula zaidi ya ugali na makande..

Kuna jirani yangu mmoja yeye alikua ndio kazi zake kushusha na kupandisha mizigo..iwe cement..magunia ya nafaka n.k.

#MaendeleoHayanaChama
 
Maana kuna mtu nimemsoma na nikakumbukia kuna thread alivyokuwa anajipa mapromo.
Hapana Mkuu,simjui huyo mtu ila naweza mtetea,

Hii thread watu tunafunguka kwasababu ni "past tense tupu"

hamna kitu ya sasa hivi,kila kinachosimuliwa hapa kime happen miaka 10 nyuma huko

wengine miaka 5 nyuma na zaidi,wanaoyapitia haya tunayoyasimua hapa (sasa hivi) sidhani kama wapo

eneo hili la tukio,hao wapo kwenye PRACTICAL wa haya yanayosimuliwa, Hivyo uwezekano wa watu wanaotoa

simulizi kwenye hii thread kuwa na maisha mazuri,kupush mandinga makali,kuishi good Life upo kwa kiasi kikubwa

Kuna mwana hapo juu kasema alipiga kazi za kiwandani miaka ya 2005-2006, Back years mzeee miaka hiyo kuna

kina sisi tulikua tunasubiri Chakula cha kengele kwa wazazi, mtu kama huyo huwezi mkosa walau na Ki Crown mzee

Mfano HAI ni mimi,nitafute nnje ya JF utajua maisha yangu ya sasa, so huu Uzi naamini watu wako real kabisa kabisa maana ni story za miaka hiyoooo.

Mtu kaanza sakanya Life tangu 2005 huko hadi leo 2022 zaidi ya 15+ years akose Nyumba,akose gari aaah weee labda kama hizi hustle anazotupa ilifika mahali akapata Half time ya (ugonjwa au majanga heavy weight).

Kwa upande wangu mimi,simshangai mtu nitakae muona humu halafu nilishaona tambo zake mahali,simshangai kabisa maana yawezekana (100%) tambo zake za sasa ndio outcome ya msoto alioupitia miaka hiyo.

Nakubaliana na wewe eneo 1 tu " Dont take JF serious kwenye kila jambo".
 
nilivochukua mfuko wa 31 nilidondoka nao na kazi ikaishiaa hapohapo nikapepewa buku mbili nakumbuka ..
Cement sio unga wakawaida ule,ule ni mfuko wa MAWE watu hawajui tu

Binafsi cement naiogopa na upambanaji wangu wote sikuwahi shobokea

kazi ya kubeba mifuko ya cement,unaenda nao chini hivi hivi unajiona..
 
kuchunga ng'ombe ase
KUCHUNGA NG'OMBE

Ilikua Arusha,nilimwambia jamaa flani anitaftie kazi Nilimkuta tu analinda nyumba 1 hivi, nikamuelezea shida yangu ya kazi akaniambia nimpitie kesho atakua ana jibu. basi nikaondoka.

Kesho yake nikarudi,akaniambia imepatikana kazi ya kuchunga ng'ombe unaweza? nikamwambia ukweli sijawahi kuchunga ng'ombe,akanaiambia sio kazi utaelekezwa tu sehemu ya kuwapeleka kwenye malisho kisha unaangalia wasiende kwenye mashamba ya watu.

nikakubaliana nae, akaniambia utakua unakaa hapo hapo (nikafurahi sana) misoto yangu yote guys mimi pakulala huwa sinaga sijawambia ila (ni siri yangu ntawambia kwenye thread zingine) nikisema naenda home huwa naendaga wapi.

Basi bana tutoke huko, nilipoambiwa ntakua nalala hapo hapo nikafurahi sana nikajua hapa nitakua nimepga ndege wawili kwa jiwe 1, yani ntakua nime solve tatizo la msosi na pili ntakua nimepata sehemu ya kuishi.

Basi jamaa akaniambia itabidi leo tushinde wote hapa ili badae nikitoka hapa nikupeleke,nikamwambia hamna shida tukashinda wote hiyo siku usiku mzma asubuhi yake tukatoka akanipeleka kwa boss, ni Muarusha yule mzee.

Nikafika nikakaribishwa mchana muda wa kula ukafika wakaleta "loshorooo" Hili ni jina la chakula cha kimasai/waarusha huchanganya maindi na maziwa fresh sjui, nikaletewa, kiukweli sikiwezagi mimi hiki kitu muda mrefu tu.

Nakijua maana mimi ni "mkazi wa arusha" hivyo naijua kabisa Loshoroo na siiwezi nishaitest nikatapkaga,basi ilivyoletwa nikapewa Nikawambia Hapana niko vizuri nimeshba kabisa, Hapo sijala nmesema hivyo nikivuta muda wa usiku watapka aina ingine ya chakula ntakula,basi jioni jioni akaja kijana wa huyo mzee akaniambia twende anipeleke sehemu wanazolisha akanionyeshe na njia ya kupitisha ng'ombe.

Tukaondoka tunatembea nakunywa maji tu ku clear njaa,nina hasira kulia nataka sina wakumlilia basi tukaenda akanionyesha tukarudi, Usiku ukafika nikasubiri msosi nione nini kitapkwa ili nile, Muda wa kula umefika

naletewa tena Loshoroooo, yewoomiiiiiiiiii... ki ukweli hiyo siku nilijua nini maana ya maisha ni safari ndefu, nikasema hapa sina namna acha nijaribu tu ntafanyaje sasa,kupga tu mdomoni Nikarudsha chenchi tapikaaa sanaaaa, hadi nikawashtua wenyeji, wakaniuliza vipi unaumwa? nikawambia hapana...

Akatokea mtoto wa kike wa huyo mzee ni mkubwa kbsa kama mmama akasema mtengenezeeni uji hebu, kimoyo moyo nikasema ashukuriwe Mungu, uji ukatengenezwa nikaona wanataka kuweka maziwa kwenye UJI, Nikawambia hapana Hapana usiweke maziwa "wamasai na maziwa sijui wana nini",basi nikatengenezewa uji nikaupiga wote,Usiku ukaisha kwa usalama.

Kesho yake kazn sasa,natakiwa kutoa ng'ombe kwenda kuchunga,Kijana ninaetakiwa kwenda nae kama mwenyeji wangu mjukuuu wa huyo mzeee "katoroka" kaenda kucheza huko,basi nikaambiwa niende tu kuchunga maana jana si nilishaonyeshwa pakuwapeleka.

Nikiwa natoa ng'ombe zizini naona maandalizi ya Loshorooo ya mchana ikiandaliwa,maana yake nikirudi kuchunga nakutana na loshoroo,sawa nikatoa ng'ombe na fimbo yangu nikawa na wa swaga mdogo mdogo,naongea nao road "nyieee rudi huku" tandika sana fimbo ng'ombe viburi kweliii wanahangaika haoooo

Nikafika eneo la kulisha nikawaacha wakawa wanaendelea kula,hapo kurudsha ng'ombe ni jioni,kumbuka nimeamka asubuhi sijala kitu,nmekaaa pale uwanjan nawaangalia ng'ombe, nililia sana hiyo siku,Nililia mpaka kwikwi..

kama ni sikuweza jinyonga ile siku hapa duniani hamna kitu itafanya niondoe uhai wangu tena,ni moja ya siku nilikaa nikijitafakari sanaaa maisha haya mpaka lini,shida hizi mpaka lini, Naendelea kuwaza ila njaa inauma nikaona mimi ninapoelekea ntachinja ng'ombe wa watu nile nyama.

Nikaamka nikajinyooosha nikifkiria nkirudi home nakutana na loshorooo tena Hapana siwezi, nikatupa fimbo kuleee nikawaaga ng'ombe (nikawambia wanangu leo mtarudi wenyewe home) Nikapita na hamsini zangu, mimi huyooooo.... (huko nyuma sijui kilichoendelea) ila kuchunga kukaishia hapo..

Mshahara niliahidiwa 20,000 kwa mwezi, niliukubali kabisa ila kazi ikawa sio riziki.
 
Tulihangaika sana kuktafta,tungekupata usingepona aisee ahahahahahha
 
Tulihangaika sana kuktafta,tungekupata usingepona aisee ahahahahahha
Ndugu yangu ng'ombe wenu kila nilipokua nikiwaangalia napata wazo la kuchinja au kuuza

nikaona hapa ninapoelekea nitafanya jambo nijikute nishapelekwa KISONGO kurusha ndege

na hivi sina wa kunitoa wala kunidhamini yani kesi hata ya kumsonya mtu ingenipeleka lock up mimi kifungo n nnje nnje labda hakimu aamue kuwa upande wangu.
 
KUBEBA ZEGE
Kwenye site ya ujenzi kituo cha watoto Sam Nujoma road, aisee hiyo kazi acha kabisa. Niliishia siku moja tu nikaenda zangu viwandani Mikocheni
Hiyo kazi kuna kijana wangu alinyatia kwenda kuiba nguo zake ili atorokeee kwani aliona atakufaa!!amefanya kazi toka saa 12 asubuhi hadi saa 3 usiku anaona hakuna hata dalili ya mzigo kuisha!!akaona isiwe tabu .bora nusu shali kuliko shari kamili!!nguo ni zako ila unazinyatia
 
Elfu 20 kwa mwezi duuh?sio poah!
 
Nakumbuka nilivyokuwa mlinzi kwenye mgodi fulani aisee kuwasimamia mafundi juu ya mnara sehemu moja inaitwa knelson kwenye uchenjuaji wa dhahabu nilipata kizunguzungu.Ikabidi nimcheki mkubwa wangu kwenye radiocall aje mwenyewe kusimamia aisee!
Hahaaaa! Mkuu umenikumbusha mbali sana, kuna kampuni inajihusisha na ujenzi wa minara ya mawasiliano, nikaenda kuomba kazi wakasema kuwa rigger lazima uende training na kozi ni ya wiki moja na gharama yake ni dola 400! na ofisi itakulipia, mimi poa, kwanza sinema lilianza hapo kwenye trining kuna bonge la mnara unatakiwa kupanda, nikapambana nikamaliza kozi fresh, nikaenda site sasa(USINIPIGIE SIMU NIPO SITE)ki ukweli malipo yake ni mazuri kwa siku ni 50, 000!!mnara wenye urefu wa mita 72!

Nilipanda niaanza kusikia kama sauti ya maraika wananiambia karibu kwetu kwa baba!!upepo unapiga mluzi halafu ni kisiwani huko, pande zote ni maji tu! ki ukweli kilichofuata sikujua nilijikuta nipo kivulini chini napewa huduma ya kwanza!!kumbe nilikata moto nusu.

Ila sikukata tamaa, nilipambana hadi nikazoea kabisa, ila siku ile daah, ni kazi ngumu kwa mwanzoni ila ukiisha izoea ni nyepesi sana yenye malipo mazuri, ila zingitia maharti yote ya ki usalama, utaifurahia.
 
Hahaaaaaa.
Ila wewe jamaa bingwa wa kukimbia kazi.
Mimi kinyesi nazoa vizuuri kabisa bila tabu.
 

Hao watu ni wauaji
 
Ngoma kama hiyo nilimshuhudia mwamba mmoja wa tanesco akikata moto

Kapanda kwenye msitm sijui alijichanganya nini yule jamaa akapolochoka kutoka juu mpka chini akatua kwa kukaa tulisikia mtu anaguna tu MMHHH!! Akakata moto

Kazi nyingne sio poa
 
Ngoma kama hiyo nilimshuhudia mwamba mmoja wa tanesco akikata moto

Kapanda kwenye msitm sijui alijichanganya nini yule jamaa akapolochoka kutoka juu mpka chini akatua kwa kukaa tulisikia mtu anaguna tu MMHHH!! Akakata moto

Kazi nyingne sio poa
Ni za hatari sana, lakini ukizingatia kutumia vile vifaa vya usalama unavyokuwa navyo hasa mkanda, shockabsorbers, work positioning, miaka yote utakuwa salama na utaifurahia kazi yako, na mimi ndio vilivyoniokoa hivyo, kwani baada ya kupoteza fahamu nilibaki pale pale nina ning'inia hadi nikapata msaada!!na ni kazi zenye matukio machache sana ya ajari kulinganisha na zile za chini ya ardhi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…