Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Kwamba kukaa lindoni ukaona ni kifo lkn hujaona kifo kutembea njiani saa 8 au 9 usiku. Na hukuwaza ulikuwa tayari unakata tiketi ya segerea kwa kuondoka lindoni na kuacha mali ulizokabidhiwa? Ila nahisi hapa kwenye ulinzi hujanyoosha maelezo
sawa
 
Sitosahau kazi ya upagazi kubeba mizigo Kilimanjaro, wale wote maPorter wa Kilimanjaro nawasalimu.

Rafiki yangu alikufa kifo cha kusikitisha nikawa naogopa kumpa taarifa mke wake na mtoto wao alikuwa mdogo. Maiti ilipelekwa singida kwa mazishi. kazi ilikuwa ngumu mno. mzigo ni kilo 20 tu lakin mazingira yalikuwa mabaya mabovu usipime. kuna watu wanatafuta mlo wao kwa taabu sana. Mungu wabariki watu wale. niliki maisha yale baada ya kupata Dollar 80 iyo ilikuwa ni kazi yangu ya mwisho na kampuni ya ZARA TOURS
 
Rafiki yako alikafaje hiko Kifo kibaya??tafadhali tupe news Mkuu tujifunze
 
vanus porter mwenzako huyu
 
tueleze hali ilikuwaje pale ulipofika kwenye lile jiwe la kubusu
 

Mwaka gani ilikua
 
tueleze hali ilikuwaje pale ulipofika kwenye lile jiwe la kubusu
Tunaitaga breakfast kwasababu ukiamka asubuhi na wenge lako unakutana na huo mlima mkali si mchezo, usipokuwa makini unaweza kuporomoka ukapasua kichwa kwenye majabali makubwa

Mwisho wa hiyo hill ndo kuna sehemu inaitwa jiwe la kubusu, hilo jiwe lazima ulikumbatie huku umebeba mzigo wako hakuna namna ndo maana pakaitwa jiwe la kubusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndo wanaitwa ma-porter aka wagumu wanatembea hapo mlimani cruiser cha mtoto.

Experience ya ule mwendo wa kutembea mlimani itakufanya ujue vizuri matumizi ya gear zote 5 za kwenye gari

Gear no 1 hutumika wakati wa kupanda mlima mkali, yaani unageuka gari kabisa na discipline inakuepo hakuna cha race wala nini ni mdogo mdogo

Gear no 2 utakutana na kilima kimeanza kulainika ndo hapo kidogo unavuta wese

Gear no 3 hapo kwa sadala kidogo unapiga story na wana

Gear no 4 na 5 ndo kabisa unachanganya mwendo wese la kutosha uwahi camp kabla wageni hawajakukuta njiani, maana yule guide wa mlima na wageni huwa wanakuwa wa mwisho kufika camp, sasa guide akikukuta njiani ni matusi kilo 7 anakuambia
“ww malaya kaza hiyo sifuri huku hakuna shangazi wala mjomba mpaka saivi hujafika camp unakata viuno na bag la wageni”

Gear no 1 pia hii hutumika wakati wa kushuka mlima hapa ndo utaimba haleluya ni kheri kupanda kuliko kushuka maana kunakuwa na mteremko mkali sana na umebeba mzigo hapo mgongoni yaani miguu inakosa balance kabisa swala la kuanguka na mzigo wako kama tembo ni kawaida sababu ya utelezi maana sehemu nyingi za kushuka huwa zimezungukwa na forest hivyo mvua mvua zinakuwepo through out the seasons

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hebu andaa thread ya hiki kistory ulichomokaje kwenye hii case?
 
Mkuu umetisha sana, hivi kuna wanawake ma porter? Hao jamaa daaa, huruma sana , jamaa kama wakimbizi miziko hadi kichwana maisha hayako fair.
 
Tamaa mbaya sana.[emoji28]

#MaendeleoHayanaChama
 
Mwamba richie ze best inaonekana kule kauzeni Ni wakulima wazuri Sana wa miwa hasa kuanzia pale Magadu kwenda mbele kule Mzinga
 
Mi nilikuwa naosha vyombo restaurant huko ugaibuni
Nimeosha vyombo ila hapa hapa bongo na haikunishinda,ni 1 ya kazi ambazo kupitia hiyo kazi mafanikio yangu mzizi wake ni hiyo kazi.

Ni kazi yangu ya kwanza iliyonifundisha mengi sana maana hapo kazini kulikua na jiko hivyo nimejua vitu vingi sana kupitia hapo,ila nilikaribishwa kama "muosha vyombo" tena wakati napewa kazi boss aliniuliza "unaweza sugua masufuria yale makubwa" akanipointia yale masufuria ya sherehe,yakang'aaa kama mapya?

nikamwambia shaka ondoa naomba kazi boss,akasema pita karoni Anza kazi nikuone,Nilisugua sufuria aliporudi akauliza,nani kanisaidia kuzisugua,wafanyakazi wakamwambia "huyo sharo wako hapo" kasugua,Nikaajiriwa rasmi kama muosha vyombo.

Kazi niliiipenda nilijivunia mnooo,japo wakati naianza niliianza kwa ugumu na shida sana,si rahisi kama ninavyoandika na kusmulia hapa.

Ki ufupi upambanaji ule wenyewe wenyewe niliuanza kwenye kibarua hicho,Godoro langu la kwanza,kodi yangu ya cghumba cha kwanza DAR nilipata hela kupitia kazi hiyo.

MOSHI HOTEL/MANZESE-TIP TOP
 
Kuna vijana nawajua wanna pataga kazi za kuswaga punda kuwatoa singida, mantra kuwa nafuu kuja kuwauza wilaya za geita wanatembea njiani usiku na mchana wiki 2 ,,,, mmoja aliponea kukiwa na fisi usiku, ILA siku hzi kwa sehemu kafanikiwa anamaisha safiii tuuu, kashaacha kuswaga punda, mvumikivu hula mbivu
 
Nishafanya ukonda
Nishazibua choo
Nishakata michongoma
Nishachukuaga kazi ya kupiga rangi
Nlipopewa advance nkala kona.
Nishauza mazagazaga tx market kinondoni.....enzi hizo wazungu,wageni wakumwaga pale dokoni

Vp niendeleee


Ova
 
Wakati nasoma O level nilikuwa najipikia vimaandazi usiku asubuhi napeleka dukani.
Siku moja usiku nikawa napikia ndani bahati mbaya umeme ukakatika nikawa natumia mshumaa.
Akaingia mdogo wangu kuubeba mshumaa sijui hata alikuwa anaenda kutafuta nini muda ule nilikuwa nimemaliza kupika mafuta nimeipua nimeyaweka chini.
Sijui ilikuwaje nikawa nasimama nitoke pale bahati mbaya nikagusa yale mafuta yakamwagika nikateleza nikaanguka nikaungua mana bado yalikuwa yamoto.

Nimefanya biashara ya mkaa sasa yale magunia yanapangwa kwenda juu ili kushusha gunia lazima upande kwenye kitu ili uweze kuyafikia uvute ile uweze kumimina kwaajili ya wateja wa reja reja.
Siku zote napanda nashusha wala sioni tabu ila sometimes unatumia hata dkk10 kuvuta mpaka lifike chini mana unakuta kwenye kupangwa limebanwa na lenzie so lazima utumia akili na nguvu litoke.
Nna ndoo yangu kubwa huwa naigeuza napanda napambania kombe hadi linashuka na muda mwingine anakuja mteja anabeba na pikipiki lakini dereva hataki kuchafuka hivo unapambana kushusha halafu kulipakia mnasaidiana.
Siku hiyo nimepanda vizuri nikaanza kuvuta sijui nilibugi wapi nilianguka nikaangukia mkono ukateguka nikabaki najiuguza wiki nzima.

Kulima ni kazi kiukweli nikiona mtu ni mkulima hasa wa jembe la mkono namheshimu sana.
Nikiwa advance tulipewa adhabu waliovuta ya kupanda mchicha mpaka uvune ndio adhabu inaisha.
Hapo sijawahi kulima na kwetu hatuna hata shamba mbaya zaidi tukapewa sehemu ambayo ilikuwa imeota ukoka halafu watu wanapatumia pia kama njia palikuwa pagumu ukipiga jembe linadunda.
Aisee sitasahau huyo mwalimu alikuwa akija akikuta mmegusa kidogo anawatoa darasani wenzenu wanasoma nyie mnalima.
Nililima lakini sisogei wala sioni dalili ya kusogea.Tulikuwa na Headgirl wetu alikuwa anapiga kazi basi akija kutusimamia anatusaidia kidogo.Nimelima nasema hapa naweka mbegu naambiwa bado umetifua juu juu tu bado jembe linatakiwa kufika chini.
Mpaka tunakuja kumwaga mbegu mikono imeota malengelenge hadi yamepasuka yanauma balaa.
Part iliyobaki ilikuwa sio ngumu kunyeshea japo maji yalikuwa ya tabu ila bora kufuata maji mbali kuliko kulima.Mwasandende huko ulipo punguza ubabe usio na maana,chuki na upendeleo.

Hapo napofanyia biashara jirani yangu anauza cement.
Akaja mteja anataka mifuko minne ya cement abebewe mpaka eneo lake la kazi.
Changamoto ikawa mbebaji mana boda aliitwa akagoma anataka elfu nne akapunguza mpaka tatu lakini mteja akagoma.
Kuna mama jirani anauza mboga mbaga akauliza atalipwa sh ngapi akaambiwa elfu mbili akakubali.
Kazi yangu ikawa kumsaidia kuweka kichwani na alipaona ni karibu na ukweli ni karibu sema mziki wa uzito wa cement.
Kabeba trip zote ile ya mwisho akajikuta kaingia period ghafla.Kilichomfanya abebe aongezee hela akalipe kibati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…