Kwenye maisha kuna mambo mengi sana watu wanapitia mengi mpaka unamuona mtu ana biashara akikwambia mapito aliyopitia mpaka kufikia hapo "acha kabisa" (naongelea wapambanaji) wale wapewa mitaji na ndugu/wazazi hampo eneo hili.
Basi bana tutoke huko leo acha tucheke (kwa watao ona inachekesha) tuchangamshane, lakini zaidi tuelimishane na kujifunza mawili matatu,maana hata katika ujinga kuna vya kujifunza,elimu ipo kila mahali.
Katika maisha yangu bana mimi sikuwahi pewa mtaji wa kufanya chochote hadi kufika hapa nilipo,sio ndugu sio wazazi sio BIKO wala any jackpot bali ni akili na kuthubutu kwangu katika sehemu tofauti tofauti.
Leo nitasimulia baadhi ya kazi nilizo thubutu ila yakanishinda, (maisha si mepesi asee) yalinishinda na nilizikimbia bila kuaga wala kuongea kitu na muajiri wangu,wakati naanza maisha niliambiwa na brother angu mmoja kauli yake hii "mdogo angu usije ukachagua kazi,fanya kila kazi ya halali unayoijua"
Huo usemi ulinikaa kichwani kila nilipotembea ulikua ukijirudia rudia kichwani mwangu,ila jamani acheni niwambie wahenga kuna misemo yao sio ya kuifatisha kabisa.,hebu acha nianze simulizi zangu hapa.
ULINZI
Nikiwa katika harakati za kutafuta kazi yakufanya nipate mtaji wakufanya kitu njiani kwenye nguzo ya umeme nikaona tangazo la kampuni ya ulinzi inatafuta vijana wa ulinzi,Kigezo cha elimu kilikua drs la 7 tu,Haina cha mdhamini zaidi ya pasport size zako,kigezo kingine kilichonishawishi nikakamatika waliandika "Hata kama hujapitia mafunzo ya Mgambo" wanakupokea.
Kampuni nyingi za ulinzi usipokua na mafunzo ya mgambo hawakupokei (hili nilishachunguza maana nilishakataliwa kampuni flani flani) kwa kukosa sifa hiyo tu. Basi baada ya kuona hizo vigezo zao nikaona hapa hapa ndio pakutokea, haina kurudi nyuma Huwa nina utaratbu wa kutembea na pasport size kwenye wallet kila ninapoenda,basi kwakua kigezo kikubwa n pasport size na ninayo,nikaona acha niende.
Kufika ofisi zao nikaingia nikajitambulisha nikahojiwa maswali kadhaa basi baada ya hapo wakaniuliza upo tayari kuanza kazi lini? nikawajibu "yani hata sasa hivi" (hapo ndio nilipojichanganya)" wakaniambia safi kabisa kijana,kaa pale subiri tukutaftie uniform.
Nikawa nimekaaa reception pale wakaingia store wakanletea sare,ila sare zilikua OVERSIZE yani kubwa mno kwangu na ilibidi nizivae pale pale,basi sikua na ajizi nikazitupia mwilini kwakua zilikua kubwa sikua na haja ya kuvua nguo nilizokua nimezivaa,nilivaa juu yake zile,viatu nilikua fresh tu (napenda vaa Timberlands) na uzuri hiyo siku nilikua na Black Tims chni hivyo kwenye upande wa viatu nilikua safi.
Baada yakukamilika kimavazi nikawa nimekaa pale kusubiri kupelekwa eneo la kazi,wakati tumekaa pale akaingia kiongozi wao nikaona watu wote wamesimama, kwakua namimi nishakua askari ikabidi nisimame kikakamavu kama askari,ripoti ikatolewa idadi ya askari na mimi nikiwepo,kisha jamaa akapita,tukakaa chini.
Mida ya saa 11 tukafatwa na gari nikapanda kwenye gari safari yakuanza sambazwa vituo vyetu vya kazi ikaanza,basi nikapelekwa kwenye lindo langu Nikamkuta mwamba Kapanda hewani kinoma,basi kufika pale akanielekeza vyakulinda,akanikabidhi daftari la vitu vya kulinda na tukazunguka nae kuvihakiki kwamba vipo kisha tulipomaliza akaniambia yeye anasepa,tukaagana akaniacha.
ilikua ni kama dispensary flani hivi kubwa kubwa,wanafunga saa mbili basi baada ya kufunga haoo wakaniaga wakaondoka,nikabaki peke yangu Usiku huo.
Sijui ikawaje umeme ukakatika eneo hilo tu na nyumba za jirani ambazo nyingi ni ofisi tu za watu sio makazi ya watu kuishi,hivyo kuna ukimya mno,Giza likatawala Uoga ukaja,ukakolea,kama dk 15 hv kupita nikaskia watu wameruka ukuta wamedondokea kwandani, Nikakimbia kujificha kwenye kistore flani, Nikawa nachungulia.
Nikaona majamaa wawili wameingia wanachukua vyuma vyuma ambavyo ni 1 ya vitu niliambiwa nilinde,siwezi sema lolote nawaangalia mkojo umenibana,roho inadunda inataka kuchomoka,Ghafla nawaona wengine wawili wanatokea wakawa wanne ila hawa wawili walikua na nondo wamezishika na mwngine kashka kishoka.
Mkojo ukazidi nibana nikawa naona haya leo ndio mwisho wangu,kupgana siwezi mimi hawa watu wote nawafanyaje,hapo store kulikua na pipa nikadumbukia,ila kabla sijadumbukia nikawapgia kelele wajamaa nikawambia "Nyie tokeni Hapo" halafu nikadumbukia kwenye pipa nikajifunika.
Nikawasikia na wao wamekurupuka wamekimbia,nikawa nimekaa kwenye pipa kama dk 10 nilisikia ukimya umezidi nikatoka kimya kimya kiminyato,kuchungulia kweli sioni mtu,Pale Pale nikasema Hapana ntakufa mimi siwezi hii kazi,nikavua nguo zao nikafungua geti nikapita na mishe zangu nikaondoka na kazi ikaishia hapo Hiyo ni saa nane usiku inaenda saa tisa huko.
KUNG'OA KISIKI
Nikiwa katika tafuta tafuta`nikafika nyumba 1 nikaomba kazi,akatoka maza mmoja akaniambia kuna kisiki cha kutoa unaweza,nikamwambia bila shaka nipate tu jembe,Akasema vifaa vyote vipo Je kazi nitaifanya kwa sh ngapi? nikjisemea kimoyo moyo,yani najipangia mwenyewe malipo? Nikaropoka Nikamwambia Boss hii kazi nzito ukinipa 15,000 itantosha.
Akasema sawa kijana ukikitoa vizuri ntakuongeza 15,000 nyingine, nikamwambia sawa boss Hapo nina mizuka kama yote,nikawa najisemea hapa nina 30k ya chap chap,Kazi ikaanza..
Piga jembe,piga shoka natikisa kisiki kinaniangalia kama hamna nilichokifanya, Lima sana kwatua sana natingisha kisiki kinantolea macho tu,Boss anakuja anauliza maendeleo namwambia Shaka ondoa hiki kinatoka chote utafurahia...
Akiondoka naanza kazi tena pga shoka kata mizizi lakini wapi,nilianza kazi saa nne asubuhi kufika saa tisa mchana kazi haielekei kuisha au kukamilika,nikamwambia Boss nakuja naenda Dukani fata vocha nimpgie maza mara moja home, Nilivyopita huko huko sikurudi nyuma,nikaona ntaja kufa mimi.
Duniani kuna visiki nyie acheni kabisa kuna miti ukiambiwa utoe kisiki chake hata upewe wiki unaweza usiweze kwa namna ardhi ilivyo ngumu,mti una mizizi kama mkia wa pweza kuupata huo mzizi mkuu tu ni kazi ya masiku,Aaaah nilikimbia mimi.
KUUZA LOTION NA VYOMBO VYA PLASTIK
Kama kawaida niko zangu barabarani natembea sina hili wala lile nikaona tangazo wanatafutwa wafanyakazi watu wa SALES AND MARKETING kigezo kikubwa uwe umefika chuo kwa level yoyote uwe na vyeti vyako tu kuthibitisha elimu yako. Mshahara kuanzia 300,000 - 500,000 NIKAONA yes HAPA HAPA nikachukua namba za simu nikarudi home kusanya vyeti vyangu,kesho yake asubuhi sana nikapga simu nikiwa nimekamilika.
Nikaelekezwa ofisi zilipo kufika pale tukaambiwa wale mliokuja na vyeti vyenu mtakua viongozi kwahyo leo leo mtaanza kazi hii,tukaelekezwa majukumu Ajabu nikaona tunaletea mabeseni,malotion lotion (yale wanayopaka wadada wa kazi) kisha tukaambiwaa Viongozi nyie mtazunguka kutangaza hizi biashara za kampuni kampuni ikishajulikana basi kazi rasmi ya mshahara wa 300k to 500k itaanza,
kwasasa tutalipwa kulingana na mauzo ya siku, sisi viongozi tukapewa mzigo wetu na mabegi na lotion zetu kila kundi tulikua na mwenyeji mmoja aliekua anatutembeza huko mtaani,basi bwana tukatoka pale na mabeseni yetu tukaingia mtaani kila kikundi tupo mtu 4, tukifika sehemu watu wamekaa yule mwenyeji anajitambulisha anaongea maneno 20 kidogo kisha anasema leo ana ofaa ya vitu flani flani, (nilipooona vile nkakumbuka aina ya kazi niliyoipata)
tulizunguka anzia ile asubuhi hadi jioni kwa mguu sijala hata kitu yule mwenyeji wetu alinunua maji ya kandoro akatugaia na sisi kidogo,asee imefika jioni muda wa kurudi nikikumbuka tulipotoka ni wapi halafu tunatakiwa kurudi kwa miguu tena,nikaona Enough is Enough,Nikawambia wazee nimebanwa haja kubwa ngoja ntafute pori nakuja. Niikaingia pori flani nikatokea mbele panda boda boda straight hadi stand,nikalipa kisha panda dala dala hadi home nafika maskani saa 1 nina njaa sio kawaida,na vyeti vyangu kwenye begi kazi ikaishia hapo.
KUTEMBEZA MAJI NA SODA
Nakumbuka ndio miaka hiyo naingia Dar nikapata wana siwajui ila niliwaona tu ni wapambanaji nikawaelezea nia yangu,shida yangu wakaniambia "imeisha hiyo wakwetu" twende ukachukue mzigo upge kazi,huyu jamaa yeye alikua anauza maji ya kutembeza,juice,soda za take away,biskut,nk
Nikamwambia mimi mtaji sina lakini,akasema usijali nakupeleka kwa boss wangu atakupa mzigo,kweli tukatoka haoo tukafika kwa muhindi mmoja hivi akanitambulisha akamwambia "mimi iko letea wewe kijana ya kaziii", muhindi akauliza "hii hapana sumbua kama ile nyingine"? jamaa akamwambia hii iko safi kabisa, basi baada ya hapo nikapewa kitrey Jamaa akanipakia mzigo wa kwenda kuzungusha..
Unachotakiwa n unaenda na mzigo unauza kwa bei ya reja reja il wewe unachukua kwa bei ya jumla,take away pale tulikua tunachukua kwa 800 wewe unauza 1000 faida 200,basi jioni mzigo utaobaki unarudsha kwa muhindi Fresh maisha yanaenda.
Basi bana jamaa akanipakia trei langu kajaza soda,maji,vinywaji vyotee muhimu mzigo huooo,yani kujitwisha tu lazima mtu akutwishe,tukatoka haooo jamaa akaniambia sasa mwanangu hapa tunagawana mitaa wewe pita kule mimi kule tutakutana badae... Nikamwambia fresh...
Tukaachana, tembea tembea na wewe mzigo ni mzito sina mfano,Kujitwisha peke ako huwezi Napishana na watu hata kununua maji hawanunui,Mchana ukakolea jua likakolea kiu ikanikamata,Acha kabisa Kuhusu Kiu Bora ushikwe na njaa utavumilia ila sio kiu cha maji.
hapo nimejikaza imefika saa 11 inaenda 12 jioni sijauza hata biskuti,ki ukweli ilifika mahali nikaona hapa ninapoendea ni kufa Kizembe,nikatafuta kivuli nikajitua mzigo wangu, Nikachukua fanta passion nikafungua Nikainywa yoteee,Kiu hakijaisha njaa ndio imekolea,Nikachukua Biskuti na fanta nyingine nikashushia.
Baada ya hapo nikaamka nikaomba kutwishwa safari moja kwa moja mpaka kwa muhindi,kufika pale ashukuriwe Mungu sikumkuta,nilikuta wafanyakazi,nikawambia mzigo wangu msiguse naenda chooni mara 1 nakuja,Nikauweka pale nilivyotoka ndio kimoja yani sikugeuza shingo...Nilijiona ntaja kufa kwenye kazi za wahindi kizembe..
Basi kuna kazi nyingi sana nimeshazifanya hadi kufikia hapa nilipo,bandiko lenyewe hili naliandika nafuta naliandika nafuta yani tangu Wiki iliyopita naandikaga tu,kazi zingine nitaziendeleza kwenye comment maana kama ni kujaribu tu wanangu nimejaribu sanaa tu...
Naomba kuishia hapa tukutane kwenye comment hapo tuendelezeane mikasa,ila yote kwa yote Tufahamu jambo moja ktika utafutaji Ni marufuku kukata tamaa,fanya kila uwezalo feli kosea anguko zomewa ila mwiko kukata tamaa,uta aibika lakini nakuhakikishia mwisho wake huwa ni mzuri tu.
Hakunaga mwisho mbaya au mbovu kwa mtafutaji mpambanaji,nimeshuhudia na nimeliona kwangu binafsi hamna kitu na enjoy kama background ya maisha yangu ya nyuma,i have many many untold stories ambazo ki ukweli ndio siri ya mafanikio yangu,siku ntakuja na ID feki ntaachia makombora .
Haya ninayo yasimulia ni ma trailer tu mapicha kamili yapo nitayasimulia siku 1 all in all tupambane tusikate tamaa maisha ni mazuri sana ukijishughulisha no matter what fanya unachoona ni sahihi kikikushinda usilazimishe Jaribu kingine,usigande na jambo 1 yawezekana bahati yako haipo kwenye hilo unalofanya.
Ushauri ni mwingi nazidi kurefusha tu thread asee,tukutane chini hapo,sema mwanangu
Mbekenga unazingua yani unaosha vyombo ughaibuni unaogopa mwambia wife? au umekosea hukumaanisha wife ulimaanisha mchepuko au kimanzi flani?
Men we dont hide our hustles kwa wake zetu,we tell them ukweli mweupe uamuzi ni wao wauchukie au waupokee,kuna heshima katika hiyo kazi yako ya kuosha vyombo mkuu Mwambie waifu utaona atavyo kuheshimu. Change brother mfanye mke rafiki ako acha mambo za kizamani...
Ila umepambana japo wewe hiyo haijakushinda tuambie kilichokushinda maaana vyombo unaendelea kuosha means hamna changamoto yyte eneo hilo... Tupe zile ngumu kumeza ulizoona hapana hizi siwezi...