Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Kuchimba kisiki ni msala nakumbuka nikiwa gerezani nilikutana na hiyo kazi vilikua visiki kama kumi na sita afu tupo mtu tano asikuambie mtu tulivuja jasho.
Mimi nishawahi kutwa na msala wa gerezani wa kazi flani Ngumu sana kuifanya,nikaona huu ushenzi

hiii kazi nisipoangalia ntaja fia hapa hapa,nikaangalia huku na kule kisha nikajidondosha chini puuuu

nikaanza kurusha miguuu kama nina dege dege,huku natoa mapovu( hapo nishakusanya mate kibaooo)

nikawa nayatema kwa pembeni kidogo kidogo,nikaskia wana wanasema Oyaa huyu atakua ana dege dege

askari akaitwa akaja akasema mbebeni muwekeni pale kivulini,nilipopelekwa kivulini nikasema hapa nikitulia

tuu ntalishwa rungu kwa sana watanishtukia, basi nikazidisha drama nikajirusha kama jongooo nakwambia

askari akaona huu msala atatufia huyu,nikabebwa ikaitwa TAX dakwa speed hadi gerezani,kufika gerezani nikajifanya

napumua haaaaaa huku nakoromaa,ndio ikawa pona yangu ila bila ile tekniki Ningefia pale walahi vile...
 
Hahahhaaa ilikua bahati yako tu unaweza kuzuga hiyo siku ila kesho yake kama kawa mzigoni kazi kazi pole sana kwa yalikukuta gerezani sio mchezo.
 
Noma sana! Nilishafanya kibarua kampuni ya usafirishaji makaa ya mawe bandari ya mtwara ( ilifikia hatua ukitema mate yanakuwa rangi nyeusi supervisor alikuwq mkaburu ni shida kwa siku 10000.kazi haziishi lakini nilitika salama
 
Noma sana! Nilishafanya kibarua kampuni ya usafirishaji makaa ya mawe bandari ya mtwara ( ilifikia hatua ukitema mate yanakuwa rangi nyeusi supervisor alikuwq mkaburu ni shida kwa siku 10000.kazi haziishi lakini nilitika salama
Kuna mtu aliniambia kazi za kiwandani zinalipa sana,siku hiyo nimewahi kiwandani kufika nikasimama kwenye foleni yani ile foleni tu ilinifanya niachane na ile kazi nikatafute mishe zingine za kufanya.
 
Write your reply...moja ya nyuzi bora kabisa sio story za kina Mpwayungu hustle za uongo uongo nimecheka sana. jamani kuna wengine hatujatoboa 40s Ila tuliyoyapitia Mungu tu ndo anaelewa ....siku Mungu akinipa kibali nishare na Mimi niliyopitia.....bado sijafika Ila kuna saa nikiangalia nilikotoka nalia SAA nyingine nacheka!
 
Show ilikua kali nakubali mkuu[emoji23]
 
Nilipewa kazi ya kulinda sehemu karibia na chichi na lacasa chica tulikuwa na kajumba chetu yani ka post tulikuwa wawili

Malaya wakitoka kujiuza chichi wanakuja kujistiri kwenye kibanda maana kurudi mwenyewe saa tisa usku ni mushkeli

Malipo yao ilikuwa ni kuwala mbususu kipindi kile mimi nilikuwa muoga ila mzee ambaye nilikuwa naye ndio zilikuwa pigo zake

Mzee alikufa na ukimwi nikabaki mwenyewe ile kazi nikaipiga chini siku malaya walivyopigana visu kwenye ugomvi wao kwakua waliuana kwenye post yangu ikawa crime scene plus kuchukuliwa maelezo na kuwa shahidi nilikoma
 
KUBEBA ZEGE
Kwenye site ya ujenzi kituo cha watoto Sam Nujoma road, aisee hiyo kazi acha kabisa. Niliishia siku moja tu nikaenda zangu viwandani Mikocheni
Umenikumbusha kipindi fulani nilienda kupiga kazi kwenye Site ya ujenzi, Bosi ni mhindi.

Kupandisha mfuko wa cement ghorofa ya kwanza ilikuwa kasheshe.
Nilipiga kazi siku moja, sikurudi tena. Nikasubiri siku ya malipo nikafuata 6500 yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…