Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Nikiri tu kwa kusema NDIYO.mwanaume kaumbiwa mateso ila mmh.Acha mapambano yaendelee,nimepishana na bus la kanisa moja hapa limeandikwa Efatha,nimewaza na mi nijipeleke kwenye hizo mambo .Na jua linawaka bwana.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3064]
 
Kumbe unaongelea za bongo. Mi nilikuwa naosha vyombo restaurant huko ugaibuni ila mpaka sasa waifu hajui. Rafiki yangu alikuwa anaogesha wazee na yeye waifu wake hajui mpaka sasa.
Lakini pesa si mlipata
 
Mzee wa Mmaa umetendea haki nia ya Uzi huu,nilitaka visa vya namna hiyo

yani unapga kazi unaona kabisa noo hiyo hela wasinipe,uhai wangu n wathamani sanaaa [emoji23] [emoji23]
Aisee haya maisha acha kabisa nikikumbuka nilivyosota,kumbe sikuwa peke yangu ukitokea familia ya chini hamna wa kukushika mkono lazima kitaa kikuchakaze na kikufunze displine hata siku ukipata pesa hutachezea
 
Kuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea mavi twende kuna kazi huko,,

Nikamuuliza kazi gani? akasema mwenye nyumba anataka chemba ya choo tuchote mavi yote na ndooo tukamwage kwenye shamba lake ili ile chemba iongezwe urefu yani pale ilipo ifukuliwe zaidi kwenda chini..

ila huwezi kufukua zaidi bila kutoa kinyesi chote, tukamwambia si aite tu gari ya kunyonya mavi inyonye, Akasema njia ya kufika kwake gari ya mavi haifiki na hata wakifosi gharama ni kubwa mno inafika 1m na huyo mzee hiyo hela hana..

hivyo mzee katoa ofa ya watu kuchota mzgo wote na ndoo na kwenda kuumwaga huko shambani kwake, Tukauliza OFA yake sh ngapi?

Jamaa akasema kazi tunaifanya watu wa 4 tu mzee kasema atatoa 100,000 kwa kila mtu,jamaa mmoja akasema mwambie aongeze walau iwe 150,000 tukapge kazi, nazama chumvini nalamba inye live na ulimi sembuse hiyo harufu inishinde? mwambie aongeze dau...

Jamaa akavuta simu kwa mshua akamwambia vijana wa kazi wamepatikana ila wanasema 100k haitoshi waongeze 50k iwe 150k, mzee akajibu Sawa njooni.

Jamaa akasema oyaa mshua kakubali, Huyo mwingine akawambia sasa sikilizeni hapa tunaenda nunua mafuta ya Taaa kidumu cha lita 5 tunamwaga mwaga mule kwenye chemba mote Harufu inakata kazi tunapga freshi..

Kusikia hivyo tukaona jamaa katoa idea nzuri sana,kweli haooo hadi kwa mangi tukanunua mafuta ya taaa haooo safari ikaanza kwenda site.

Tumefika tukaenda kwenye chemba, ilikua tayari ishabomolewa lile zege la juu hivyo limebaki shimo pana tu unaona inye live live,mafinyo finyo live live, Jamaa akamwaga mafuta ya taaa pwaaaaaa koteee..

Tukaletewa ndooo kila mtu na ndoo yake,gloves kazi ikaanza nikadumbukiza nikachota ndoo ya kwanza nikatoa,jamani jamani jamani nilienda kumwaga shambani nikapitiliza huko huko sikurudi nyuma tena.

Asee inye isikieni tu,ile 150,000 nikaona wala isinipe presha mimi,na niikose tu siwezzi chezea gwede gwede kama vile ni rost... nimeondoka nimefika maskani nasimulia waliobaki,nusu saa haijaisha namuona mwenzangu mwingine huyu hapa karudi, aaah weee kuna kazi za kufanya bwana sio kazi ya kuchezea tope la binadamu..
Controla unachonichekesha unanguvu ya kuthubutu lakin Sasa kuingia mitin ni dakika sifur [emoji23][emoji23][emoji23]we jamaaa umenichekesha leo
 
Haijalishi unapitia changamoto gani katika maisha

Haijalishi unapitia magumu gani katika maisha yako

yawezekana umechoka,unahisi kama unateseka peke ako

si kweli', ukipitia huu uzi utagundua wote wanayoyasimulia haya

sifa yao kuu ni 1 "uvumilivu" na "kutokukata tamaa",usikatishwe tamaa

na mapito unayoyapitia kwa wakati huu,wenzako walishayapitia na sasa

imebaki kama simulizi za kuchekesha,lakini nakwambia hivi sio vichekesho

wakati watu wakiyapitia haya walikua wakilia machozi,wakivuja jasho,mioyo yao

ilikufa ikasinyaa,nk lakini leo hii zimegeuka kama "SHUHUDA" tunacheka tunafurahia

Chochote unachopitia sasa,Hali ngumu yoyote unayoiona mbele yako sasa amini

nakwambia ni "linapita" hutoteseka milele,hutoonewa milele,hutolia milele,hutohuzunika

milele,kesho yako itakua kicheko na simulizi na shuhuda kwa wengine,Kwa sasa

piga moyo Konde songa zako mbele Mkombozi wa kesho yako ni wewe mwenyewe,Usichoke kupambana,Mungu yupo anakuona.

And lets all say Amen!

Ameeen.......
Ameein
 
3.Kuvua bahari ya upande wa sahare Tanga

Nilikuwa nina shida na nauli nikimbie Lusanga kuna mishe mchizi alinisanua nikapata kazi ya kuvua mwana aliniunga tu picha linaanza jioni ile nikatokea na ka t-shirt kangu manga nyepesi maana tulienda vua maji ya usiku [emoji3] wale wadigo na Wapemba wa ile mashua sijui boat whatever the case .. walikuwa wanacheka

Niligundua kwa nini wanacheka tupo katika ya bahari ule upepo wa baridi niliokuwa napigiwa nao plus yale maji yakikurukia ushapata picha

Kwa nini nilijuta kuna kitu wenyeji wanaita sijui bawa la mvua wataalamu mtaiweka sawa ile maji yanaongezeka yanapanda juu kwa kasi yanavuka hadi kingo za beach ambapo watu wanakaa kunakuwa na maji yanasogea hio ishu ilitukutia usiku plus mawimbi maji yakawa yanaingia kwenye chombo chetu tuna kazi ya kuyatoa na visado boti linapigwa pushi na mawimbi mara chemli imeanguka imepasuka mpemba mmoja akanambia "wajua kuogelea weye ..mimi siokoi ntu nanusuru roho yangu mie " wengine wanakazi ya kutoa maji na visado huku wakisema "shahada" yaani kwa imani ya dini ya kiislamu unaenda peponi ukifa kama utaisema

Nilisema sirudii tena [emoji1787][emoji1787]
Nimecheka kama chizi, machozi yakinitoka aisee
Sipatii picha khali uliyokuwa nayo wakati huo ukizingatia wenyeji unaowaona ndo wamekwisha kata tamaa
 
Mzee hiii thread vinavyosimuliwa n kama vichekesho ila usiombe uwe ndio unayaptia haya yanayosimuliwa in Reality....
 
Kumbe unaongelea za bongo. Mi nilikuwa naosha vyombo restaurant huko ugaibuni ila mpaka sasa waifu hajui. Rafiki yangu alikuwa anaogesha wazee na yeye waifu wake hajui mpaka sasa.
Naomb usimulie ilikuwaje
 
Mimi nishawahi kutwa na msala wa gerezani wa kazi flani Ngumu sana kuifanya,nikaona huu ushenzi

hiii kazi nisipoangalia ntaja fia hapa hapa,nikaangalia huku na kule kisha nikajidondosha chini puuuu

nikaanza kurusha miguuu kama nina dege dege,huku natoa mapovu( hapo nishakusanya mate kibaooo)

nikawa nayatema kwa pembeni kidogo kidogo,nikaskia wana wanasema Oyaa huyu atakua ana dege dege

askari akaitwa akaja akasema mbebeni muwekeni pale kivulini,nilipopelekwa kivulini nikasema hapa nikitulia

tuu ntalishwa rungu kwa sana watanishtukia, basi nikazidisha drama nikajirusha kama jongooo nakwambia

askari akaona huu msala atatufia huyu,nikabebwa ikaitwa TAX dakwa speed hadi gerezani,kufika gerezani nikajifanya

napumua haaaaaa huku nakoromaa,ndio ikawa pona yangu ila bila ile tekniki Ningefia pale walahi vile...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sio kila hustle wife ajue eti kisa mnapendana. Kuna misala mingi kama mwanaume unatakiwa usimame mwenyewe tu mradi wao wasilale njaa.

Kusema kila kitu sio uanaume. Binafsi nilipataga msala job wife alijua nipo likizo ndio baadae nikamwambia nimesimamishwa kazi.

Hata baadae nilipotimuliwa alijua ni kwa sababu niliyokua nimemwambia kumbe sababu ni nyingine kabisa ambayo alikuja kuijua kama 4yrs later wakati maisha yalishasonga kivingine.

Alijua baada ya kufungua makabrasha yangu kwenye briefcase alishangaa sana kujua kumbe nilikua na msala mkubwa kiasi kile na niliwezaje kupretend niko normal. Ulikua msala mzito wa kula mvua za kutosha ila niliupangua kivyangu na hadi leo akiniangalia hanimalizi
Weewe ndio mwamba mkuu,Nime appreciate sana hii comment ni kweli Kuna mambo mwanamke anatakiwa ayajue baadae sana,Akiyajua wakati huo huo tatizo linakuwa kubwa sana.

Wanawake wengi ni watu wa hisia sana.

"A true measure of a man isn't what he reveals to the world but what he hides from it"
 
Kuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea mavi twende kuna kazi huko,,

Nikamuuliza kazi gani? akasema mwenye nyumba anataka chemba ya choo tuchote mavi yote na ndooo tukamwage kwenye shamba lake ili ile chemba iongezwe urefu yani pale ilipo ifukuliwe zaidi kwenda chini..

ila huwezi kufukua zaidi bila kutoa kinyesi chote, tukamwambia si aite tu gari ya kunyonya mavi inyonye, Akasema njia ya kufika kwake gari ya mavi haifiki na hata wakifosi gharama ni kubwa mno inafika 1m na huyo mzee hiyo hela hana..

hivyo mzee katoa ofa ya watu kuchota mzgo wote na ndoo na kwenda kuumwaga huko shambani kwake, Tukauliza OFA yake sh ngapi?

Jamaa akasema kazi tunaifanya watu wa 4 tu mzee kasema atatoa 100,000 kwa kila mtu,jamaa mmoja akasema mwambie aongeze walau iwe 150,000 tukapge kazi, nazama chumvini nalamba inye live na ulimi sembuse hiyo harufu inishinde? mwambie aongeze dau...

Jamaa akavuta simu kwa mshua akamwambia vijana wa kazi wamepatikana ila wanasema 100k haitoshi waongeze 50k iwe 150k, mzee akajibu Sawa njooni.

Jamaa akasema oyaa mshua kakubali, Huyo mwingine akawambia sasa sikilizeni hapa tunaenda nunua mafuta ya Taaa kidumu cha lita 5 tunamwaga mwaga mule kwenye chemba mote Harufu inakata kazi tunapga freshi..

Kusikia hivyo tukaona jamaa katoa idea nzuri sana,kweli haooo hadi kwa mangi tukanunua mafuta ya taaa haooo safari ikaanza kwenda site.

Tumefika tukaenda kwenye chemba, ilikua tayari ishabomolewa lile zege la juu hivyo limebaki shimo pana tu unaona inye live live,mafinyo finyo live live, Jamaa akamwaga mafuta ya taaa pwaaaaaa koteee..

Tukaletewa ndooo kila mtu na ndoo yake,gloves kazi ikaanza nikadumbukiza nikachota ndoo ya kwanza nikatoa,jamani jamani jamani nilienda kumwaga shambani nikapitiliza huko huko sikurudi nyuma tena.

Asee inye isikieni tu,ile 150,000 nikaona wala isinipe presha mimi,na niikose tu siwezzi chezea gwede gwede kama vile ni rost... nimeondoka nimefika maskani nasimulia waliobaki,nusu saa haijaisha namuona mwenzangu mwingine huyu hapa karudi, aaah weee kuna kazi za kufanya bwana sio kazi ya kuchezea tope la binadamu..
Nimecheka sana😂😂😂😂
 
Daah kweli kuzaliwa mwanaume kazi... Nmecheka sana. Kuna kazi zina watu wake asee
 
Kutengeneza kalai yaani unakata bati la pipa afu unalitwanga linakuwa kalai afu kalai moja unalipwa 400,kuna tangazo moja nililikuta kwenye nguzo ya umeme ?mara tunatafuta mastoo kipa,madereva n.k, nika apply bhana kufika ofisini nika kubaliwa nikapelekwa kwa wenzangu nikawakuta kama wamekata tama hivi utawasikia wanasema hi guy !!? We believe in mechandize if you tired don't quite,,haha watu soli za viatu zimeisha wamepiga tai chini ndala haha nikasema nimepatikana baadae tunakabidhiwa mizigo ya chupa ya chai na mabeseni,kilichofata ni kuuza mlango kwa mlango,mda mwingine una kutana na wahuni wanakupiga biti,,,unashindia tu mihogo ya kutafuna ,maisha haya noma sana
 
Back
Top Bottom