Kazi ya Kuuza Movie/Series Kwa Kijana Mwenye Uzoefu nayo

Kazi ya Kuuza Movie/Series Kwa Kijana Mwenye Uzoefu nayo

Ofisi inajihusisha na ujasiriamali wa kuuza Series/movies kwa watu majumbani.

Anahitajika kijana mwenye uzoefu na kazi ambae ameshawahi kuifanya na mwenye uzoefu nayo.

Lakini kwa ambae anajua computer vizuri kutumia na Kuitengeneza matatizo madogo madogo pia unaweza kufaa.

Kazi ni Kuingiza Movie kwenye kifaa atakachokuja nacho mteja.

Kupanga Movie kwnye mafaili yake kulingana na mwaka na siku husika.

Usafi wa Eneo lako la kazi na kuhakikisha usalama wa vifaa vyako..

Mshahara : 300,000 kwa mwezi
Muda Wa kuingia 1:00 asubuhi
Muda wa Kutoka : 5:00 usiku

Eneo la Kazi : Dar/Temboni/Mwika Annex.

Kwa atakaesikia hii amtaarifu na mwingine.

Mawasiliano : Inbox
Napendekeza uurekebishe,hiyo saa 1 asubuhi mtu wa kuweka wapi utampata wapi?,fanya kuingia saa 2 asubuhi kutoka saa 4 usiku ili huyo mtu hata hakai tembon aweze kurudi kwao
 
Asante, ila I did it on purpose ili niendane na bandiko na aina ya mtu anayetakiwa

Wengi wao ndio wale wanao andika h badala ya a,e,i,o na u,
Mfano
Hanakuja
Hendelea.....
Acha dharau.

Nilianza hizi kazi nikiwa form one kipindi hicho hakuna websites za kudownload nyimbo au video.

Nyimbo ilikua anakupa DJ au mnarip kwa kutumia Ashampoo au Windows Media Player. Nikaifanya nikiwa chuo na nilivyomaliza pia.

Kisha wewe mtoto wa kishua unaamini kila aliye pale hajui kuandika au siyo?
 
Tatizo ni umbali tu na chumba nilichopanga ila kama siyo mimi ningekuunganisha na watu.

Napiga windows zote, natroubleshoot network, naweza kutroubleshoot matatizo ya PC, softwares, natengeneza mega. In all honesty yaani nikikaa eneo la tukio nikikupigia mashine imeharibika ujue hiyo tunaipeleka machinga complex au hard ware iko hovyo na hatuna spare.

Funny times bwana
 
Back
Top Bottom