Jukumu la mwanamke kwa mwanaume ni Personal Assistant. Majukumu ambayo PA anayafanya kwa CEO yanafanana na anayofanya mke kwa mume.
Mwanamke anatakiwa kuwa female version ya mwanaume duniani. Afanye vile vitu mwanaume hawezi fanya kwa niaba yake.
Mfano, kumfariji anapokuwa ameghafirika, kumshauri, kumkumbusha mambo muhimu, kuwa sikio lake pale anapohitaji mtu wa kumsikiliza tension zake, kumpikia na kumuandalia chakula kizuri, kumuuguza akiumwa, kumtunzia Siri na faragha zake, kuongea nae kwa sauti ya kike yenye upole na utii ndani yake, mtunza mali zake, msimamizi wa mali zake pale anapokuwa hayupo, msisimuaji wa mwili wa mwanaume na kumpa raha za kimwili, mbeba uzao wake na kulea watoto wake na warithi wa himaya yake.
Mwanamke ana majukumu hayo kwa mwanaume.