Kazi ya mtandaoni

Kazi ya mtandaoni

Red pen

Member
Joined
Mar 4, 2019
Posts
51
Reaction score
37
Habari wanaJF,

Mimi ni mwalimu wa kike niko Kagera. Nina degree ya elimu kutoka UDOM mwaka 2014 ndio nilimaliza nikiwa na G.P.A ya 3.4. Nina uzoefu wa miaka 4 mpaka sasa nikiwa kazini.

Mimi ni mtu ninayependa sana kujituma, kufanya kazi kwa bidii, ninauwezo mkubwa wa kutumia computer (MS word na Excel), ninauwezo wa kufanya vizuri kaz bila uangalizi na usimamizi wa mtu.

Ninauwezo wa kuandika contents (articles na vitabu), ninaongea lugha ya Kiingereza na Kiswahili vizuri (fluently).

Nina vifaaa kama Pc, smartphone yenye uwezo wa kufanya kazi hata kama sina computer karibu, internet ya kasi kubwa n.k.

Ninaomba kazi ya kufanya even through online. Kazi yoyote halali kutoka kwenye NGO's, serikalini, binafsi kama una blog, websites, shule ( kufundishwa online), kampuni mbalimbali na mashirika. Nipo tayari kufanya kazi kuanzia sasa kwa masaa 7 kwa siku.

Tafadhari niko serious na hili, mwenye kujihitaji tuwasiliane ikibidi nimpe uthibitisho kutumia nakala za vyeti, na niko tayari kufanya interview.

Asanteni.
 
Mbona hujadadavua unataka nini? Unataka kazi ya kufundisha shule? Au online business? Hujaeleweka kipi ni kipi
 
Jifunze Forex kama una moyo wa chuma lakini mwisho ukishaimaster vizuri utapata wanafunzi wa online huku na wewe unapiga Dola taratibu
 
Red pen Nimesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho sijaona ulipoandika umesomea nini zaidi ya kusema umesoma education na GPA yako baada ya hapo ukaenda kujisifia umesoma education sasa najiuliza sipati picha.
 
Kwa nini usiolewe dada mwalimu, huoni umri unaenda sana? Yaani badala ya kuwaza kukesha na mumeo unawaza kukesha na laptop.
 
Kasoma education Ina maana kasomea ualimu nini sasa usichoelewa hapa
Ukiwa na kichwa huwezi elewa kuna ualimu mwingi mkuu, ualimu upi kasomea yeye ukisema umesomea elimu ina maana nyingi ualimu wa sayansi au arts sasa ameleta tangazo asaidiwe lazima awe spefic elimu ni pana sana
 
Jifunze forex kama una moyo wa chuma lakini mwisho ukishaimaster vizuri utapata wanafunzi wa online huku na wewe unapiga dola taratibu
Asante ndugu ila Forex hapana nishaijaribu, nilisoma hadi vitabu na kumpata mentor ila mambo yakawa ndivo sivyo.
 
Nimesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho sijaona ulipoandika umesomea nini zaidi ya kusema umesoma education na gpa yako baada ya hapo ukaenda kujisifia umesoma education sasa najiuliza sipati picha
Sijajisifia ila nilikuwa naeleza qualifications mbalimbali nilizonazo, nimesomea ualimu na kuchukua kozi mbalimbali za computer.

Asante.
 
Mbona hujadadafua unataka nini? Unataka kazi ya kufundisha shule? Au online business? Hujaeleweka kipi ni kipi
Yaweza ikawa ya kufundisha kupitia online au virtual assistant (secretary) au mwandishi wa contents mbalimbali kwenye blogs, web au kazi yoyote ya kampuni au shirika fulani nikawa nawafanyia kazi through online.

Asante.
 
Ualimu wako ni wa masomo gani kalamu nyekundu?
 
Ukiwa una uhitaji wa Mwalimu wa English language, History kuanzia msingi mpaka vyuo nafundisha, Ms Word na Excel.
Ukiwa na kichwa huwezi elewa kuna ualimu mwingi mkuu ualimu upi kasomea yeye ukisema umesomea elimu ina mana nyingi ualimu wa sayansi au arts sasa ameleta tangazo asaidiwe lazima awe spefic elimu ni pana sana
[/Q
mcheki GLOBAL CITIZEN atakupa hints za kazi online
 
Back
Top Bottom