Wananchi walipaswa kushawishiwa na CCM kwa kasi ya maendeleo. Na hivyo ccm ingreendelea kushamiri na kupendwa na wananchi.
Lkn naona ccm wanahangaika kutafuta MTU sahihi wa kuwashawishi wananchi kuipenda ccm as if hiki ni chama kipya kilichosajiliwa juzi. Kumbe ni chama kilichozeeka na kimeongoza nchi hii tangu uhuru wake.
Kwa kero hizi:-kasi duni ya maendeleo, katiba mbovu, rushwa kushamiri, ajira kukosekana, rasilimali zetu kukwapuliwa hovyo, rais kutegemea mikopo kuendesha nchi, miradi mingi kusuasua, n.k, hakuna mtu ataweza kuwashawishi watanzania kuipenda ccm.
Mama Samia atateua na kutengua watu wengi sana lkn hatopatikana mtu sahihi.
Njia pekee ya kueneza CCM ni Serikali kuwajibika ipasavyo ktk kuwaletea wananchi maendeleo, kujenga usawa wa kisiasa nchini kwa kuwa na katiba bora, kuchagiza ukuaji wa uchumi utakaotengeneza ajira nyingi, kuifuta rushwa, kuzuia ubadhirifu, kujitegemea kiuchumi, n.k.
Hata huyo atakayetuliwa hiyo tarehe 3 April atapwaya tu. Suala siyo nani ni mwenezi, bali ni mfumo mbovu wa uendeshaji wa serikali ndiyo unaopelekea kazi ya uenezi kuwa ngumu