Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Inategemea na kampuni unayofanyia Kuna kampuni kubwa kama GARDA WORLD, G4S ,security group SGA, SUMA JKT n.k Kuna rafiki zangu wanafanya kazi huko kitengo cha IT na wengine walinzi.

Walinzi unaozungumzia wewe ni wale wa kampuni kama MOKU ,KAMANDA SECURITY na zingine za wazawa.
 
Yessssssss.. niaje!

Asee kazi nyingine ndugu zangu sio kazi. Mshahara 180 or less na hapo hujafanya kosa. Unagewa mkataba huo unaweza ukalia na unaambiwa kama hauuwez tunakuruhus njia ile nyeupe!.

Hapo unashngaa kila siku unalipwa elf 6 lakini siku hiyo ukikutwa na kosa unakatwa elfu 20. Hapohpo ikifika mwisho wa mwez kulipana mpaka maandamano.

Miaka kadhaa nyuma nilipiga hii kazi! Dah 😁😁 sijui pepo lile la kufanya yoyote nilitolea wapi mana sio kwa ujinga ule. Mshahara kupewa mpaka kivumbi na unapewa mshahara na masimango kibao.

Ilifika kipindi mshahara mnapokea tarehe 15. Kuna mwez flani nikPewa mshahar tarehe 24 yani nimefanya kaz siku 54. Hiz kaz ndo mana wanajazana wazee wa hovyo kwa hovyo tu

Tupia vioja na vimbwanga vya hii kaz hapa!

View attachment 3071851
Oke Oke. So ulianza kazi ya Ulinzi na sasa unataka uingie JW sio?!
 
Enzi zile kwenye mashamba ya chai kulikua na mlinzi mkuu, ukiwa karibu naye anafanya mipango unatolewa shambani unakua mlinzi wa usiku sehemu Kama factory, nyumba za mameneja na pampu ya maji.
Sasa Kuna dogo mmoja alipangwa pampu ya maji mbali kabisa na kambi, usiku ule baridi ikawa too much kwa Bahati nzuri supervisor alishapita kukagua Kama lindo Lina MTU, dogo akaona arudi home kwasababu hakuna kukaguliwa Tena. Alipofika home anamkuta mlinzi mkuu anapiga story na mke wake.
Dogo alivua lile kabuti na buti na kumuambia mlinzi mkuu kazi imemshinda.
Kuna kipindi sisi ilikuwa ukipangwa jenereta unaenda na shuka. Mana kipindi niko kaz hi nilikuwa visiwani so kuna visiwa zanzibar havin umeme ila kuna jenereta kubwa zinarun umeme a hotel husika. Sas kaz kubwa ple ni kubadil pale moja linapozima au kuongeza mafuta ili umeme uwepo.

Na ujinga wa lile jenereta hujui linazima mda gani. Nimekomaa mpaka saa 7 usiku hola. Nikabeba shuka nikaenda kujitundika bichi.. kumbe usiku wa saa 8 lilizima na likakaa nusu saa halijawashwa mpaka bosi wa kisiwa kaenda kuwasha mwemyew. Asubuh nimeamka nakuta jenerata inayowaka na nilyoiacha vitu viwili tofaut. Nikajua huu msala 😁

Nilikatwa elf 40 ile siku
 
Inategemea na kampuni unayofanyia Kuna kampuni kubwa kama GARDA WORLD, G4S ,security group SGA, SUMA JKT n.k Kuna rafiki zangu wanafanya kazi huko kitengo cha IT na wengine walinzi.

Walinzi unaozungumzia wewe ni wale wa kampuni kama MOKU ,KAMANDA SECURITY na zingine za wazawa.
Yesss ingawa hata jkt suma ina madhaif mengi sana ya kuendeshwa kijinga jinga
 
Walinzi wa sokoni wao hata wasipolipwa sawa tu.
kuna jamaa alikuwa mlinzi mlo aliokuwa anakula ni wa kiwango kingine zaidi ya yote ukihitaji sendo ama yeboyebo wee mwambie no tu unayovaaga kesho yake asubuhi fuata kwake .

matunda hadi alikuwa anatugawia sisi ma bachelor nk
 
Wenye makampuni wanalipwa pesa nyingi kwa kila kichwa ,si chini ya laki 5 ila Maboss ndiyo wanawalipa hela hiyo tena hiyo 150 ni nyingi wengine wanalipwa kilo aka jiwe(laki 1).

Ndiyo maana wanakuwa wezi lindoni ,wanaiba vifaa.
 
Back
Top Bottom