Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Inategemea na kampuni unayofanyia Kuna kampuni kubwa kama GARDA WORLD, G4S ,security group SGA, SUMA JKT n.k Kuna rafiki zangu wanafanya kazi huko kitengo cha IT na wengine walinzi.

Walinzi unaozungumzia wewe ni wale wa kampuni kama MOKU ,KAMANDA SECURITY na zingine za wazawa.
 
Oke Oke. So ulianza kazi ya Ulinzi na sasa unataka uingie JW sio?!
 
Kuna kipindi sisi ilikuwa ukipangwa jenereta unaenda na shuka. Mana kipindi niko kaz hi nilikuwa visiwani so kuna visiwa zanzibar havin umeme ila kuna jenereta kubwa zinarun umeme a hotel husika. Sas kaz kubwa ple ni kubadil pale moja linapozima au kuongeza mafuta ili umeme uwepo.

Na ujinga wa lile jenereta hujui linazima mda gani. Nimekomaa mpaka saa 7 usiku hola. Nikabeba shuka nikaenda kujitundika bichi.. kumbe usiku wa saa 8 lilizima na likakaa nusu saa halijawashwa mpaka bosi wa kisiwa kaenda kuwasha mwemyew. Asubuh nimeamka nakuta jenerata inayowaka na nilyoiacha vitu viwili tofaut. Nikajua huu msala 😁

Nilikatwa elf 40 ile siku
 
Yesss ingawa hata jkt suma ina madhaif mengi sana ya kuendeshwa kijinga jinga
 
Walinzi wa sokoni wao hata wasipolipwa sawa tu.
kuna jamaa alikuwa mlinzi mlo aliokuwa anakula ni wa kiwango kingine zaidi ya yote ukihitaji sendo ama yeboyebo wee mwambie no tu unayovaaga kesho yake asubuhi fuata kwake .

matunda hadi alikuwa anatugawia sisi ma bachelor nk
 
Wenye makampuni wanalipwa pesa nyingi kwa kila kichwa ,si chini ya laki 5 ila Maboss ndiyo wanawalipa hela hiyo tena hiyo 150 ni nyingi wengine wanalipwa kilo aka jiwe(laki 1).

Ndiyo maana wanakuwa wezi lindoni ,wanaiba vifaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…