Siyo msomaji mzuri wa Biblia, ila kuna verse zinasema, Mungu aligawa vipawa mbalimbali, wengine walimu, Wakulima, wavuvi, mafundi, waimbaji, walinzi, wanasheria, nk nk, wote hawa wapo ili kukamilisha kazi na utukufu wa Mungu shambani mwake na kila mmoja ataulizwa alichofanya kwenye eneo lake, kuna mahali ktk biblia panasema, enyi watoza ushuru, msitoze zaidi ya ipasavyo, na nyie wakulima leteni malimbuko gharani mwa Bwana ili kiwepo chakula cha kutosha ( rejea msosi uliompeleka Yakobo Misri), kwa ufupi kila kazi njema ni ya Mungu na tutalipwa kwa kadri tunavyoifanya. Mbele za Mungu hakuna kazi nzuri zaidi kuliko nyingine, ni sawa na viungo vya mwili, hakuna kilicho bora kuliko kingine.