Kazi zipo ila wafanyakazi wenye sifa sahihi za uzalishaji kwa vitendo ndio hakuna

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Wapo watakao kuja na vyeti vingi na ufaulu wa A+ na kusema wana sifa sahihi za kupata kazi, lakini ukiwapa kazi wafanye kwa vitendo wanashindwa na kupelekea kupata hasara au kushuka kwa mauzo/faida.

Mfano: Kiwanda X kinazalisha baiskeli 1000 kwa siku, na ili kiwanda X kiendelee kuzalisha na kiweze kuwalipa wafanyakazi wake vizuri, kinataka kupata uhakika wa mauzo wa baiskeli 200 kwa siku.

Kiwanda kikaamua kumuajiri mtumishi mmoja mwenye PhD ya masoko (meneja masoko) ili aweze kutumia elimu yake katika kuhakikisha kwa siku, baiskeli zisizopungua 200 ziwe zimeuzwa.

Matokeo yake, huyu mtu ambaye ni meneja masoko akashindwa kutimiza lengo la kiwanda, na kutaka kulipwa kwa kuamini ana elimu sahihi.

Mwisho wa siku, kiwanda X kikamfuta kazi kwa sababu hana sifa sahihi za uzalishaji wa vitendo.

Cha kujifunza: Kabla ya kuanza kulalamika ajira hakuna, jifanyie tathmini kwanza, una sifa sahihi za uzalishaji kwa vitendo ukiachana na hizo karatasi ulizonazo?​
 
Kongole mkuu.
Ni kweli na ndo mana siku za nyuma kulikuwepo kitu kinaitwa Induction na Probation period. Mwajiriwa mtarajiwa anafanya kazi chini ya mtu mwenye uzoefu kazini hata kama ni PhD holder. Muda ilikuwa ni mwaka1 au zaidi na Huyo supervisor anaweza akawa ni Diploma holder au 1st degree na atamwandikia Report ya Competence au Incomptent. Hivi vyeti vya Ku-google, Computer au kutumia AI... mmh!
 
Tatizo ni elimu au ni sisi wenyewe?
 
Ila uafisa masoko ni kutafuta lawama tuu kwa baadhi ya kazi, sasa uuze baiskeli 200 kwa siku ndo nini wakuu 😂
 
Mtaalamu wa miamba, halafu hajui mwamba upi wenye madini
Au Mechanical Engineer lakini hajui hata kutengeneza opener ya kufungulia kizibo cha soda.
Au Civil Engineer/Structural Engineer lakini hajui hata plasta au sakafu inatengenezwaje
 
Ila uafisa masoko ni kutafuta lawama tuu kwa baadhi ya kazi, sasa uuze baiskeli 200 kwa siku ndo nini wakuu 😂
Si ndio kazi ulioisomea? Au mwingine anaweza kusema yeye ni mtaalamu mbobezi wa magonjwa ya figo, halafu huku wagonjwa wanakufa na magonjwa ya figo.​
 
Au Mechanical Engineer lakini hajui hata kutengeneza opener ya kufungulia kizibo cha soda.
Au Civil Engineer/Structural Engineer lakini hajui hata plasta au sakafu inatengenezwaje
Yaani zote ni mbwembwe za kwenye makaratasi.
 
NIni kifanyike ili kuleta ufanisi kwa kile tunachokisomea?
Kuanzia mashuleni na vyuoni mfumo wa elimu ubadilishwe.
Ujerumani watoto wanaanza kujifunza fani zao kwa vitendo kuanzia primary school sasa mtu huyu hadi akifika chuo anakuwa ni specialist tayari kwenye fani yake
 
Si ndio kazi ulioisomea? Au mwingine anaweza kusema yeye ni mtaalamu mbobezi wa magonjwa ya figo, halafu huku wagonjwa wanakufa na magonjwa ya figo.​
Ishu ya udaktari haiwez kuingia humu, kwan wagonjwa wasipokuja hosp utamlaumu daktari?

tubaki na hiyo ya afsa masoko, hakuna afsa masoko atakuletea faida ya 100% kwenye biashara ambayo ww mmiliki hujaweka misingi yako, weka misingi then afsa masoko aje apite kwenye hiyo njia yako huku akiweka elimu yake hapo
 
Waajiri wasiangalie vyeti pekee, watengeneze mazingira ya training kwa waajiriwa ili wawe vile watakavyo wao, bila kukimbilia judgment...
Kwa nchi zetu hizi zinazoendelea inawezekana kufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom