Kazi zipo ila wafanyakazi wenye sifa sahihi za uzalishaji kwa vitendo ndio hakuna

Kazi zipo ila wafanyakazi wenye sifa sahihi za uzalishaji kwa vitendo ndio hakuna

Kuanzia mashuleni na vyuoni mfumo wa elimu ubadilishwe.
Ujerumani watoto wanaanza kujifunza fani zao kwa vitendo kuanzia primary school sasa mtu huyu hadi akifika chuo anakuwa ni specialist tayari kwenye fani yake
Kwa hizi nchi zetu, ni nani awe chachu wa kubadilisha hiyo mifumo?
 
Ishu ya udaktari haiwez kuingia humu, kwan wagonjwa wasipokuja hosp utamlaumu daktari?

tubaki na hiyo ya afsa masoko, hakuna afsa masoko atakuletea faida ya 100% kwenye biashara ambayo ww mmiliki hujaweka misingi yako, weka misingi then afsa masoko aje apite kwenye hiyo njia yako huku akiweka elimu yake hapo
Mgonjwa asipoenda hospitalini, ni ishara nzuri kuonyesha wagonjwa wamepungua, ukiona gari nyingi zipo gereji, tatizo sio gereji bali ni magari husika yanatafuta suluhisho.​
 
Kwa nchi zetu hizi zinazoendelea inawezekana kufanya hivyo?
Inawezekana, unawakubali watu kama intern/Vibarua, siyo ajira rasmin, then unakua unawalipa posho kwenye training au wanajitolea kwenye training.
Kuna makampuni yanafanya hivyo mengi tu...
 
Tatizo ni elimu au ni sisi wenyewe?
Ni vyote kwa pamoja:
1. Elimu na vyeti husika vinapatikana kirahisi -rahisi mno lakini vyote vikiwa vimesha chakachuliwa sana. Can you imagine a graduate anashindwa kufanya hesabu za kuzidisha au kugawanya simple Numbers i.e Arithmetics eti ni mpaka atafute calculator. anasema kwani kalkuleta kazi yake nn na iko huko kwenye laptop yake?
2. Masomo/Course nyingine zimerahisishwa kiasi kwamba upatikanaji wake zipo on line i.e. kwa njia ya Mtandao na mtu mhitimu "anasemekana" amefaulu kabisa na kutunukiwa cheti.
3. Juzi kati hapo, mjukuu wangu (Ke) std.5 aliniuliza swali la F2 lililohusu Female Reproductive system - nikashangaa. Kweli huyo kiumri na akili yake vinaendana na somo hilo?? i.e. Syllabus itumikayo maShuleni kwa sasa esp. shule za msingi inaacha maswali mengi ya kujiuliza.
 
Wapo watakao kuja na vyeti vingi na ufaulu wa A+ na kusema wana sifa sahihi za kupata kazi, lakini ukiwapa kazi wafanye kwa vitendo wanashindwa na kupelekea kupata hasara au kushuka kwa mauzo/faida.

Mfano: Kiwanda X kinazalisha baiskeli 1000 kwa siku, na ili kiwanda X kiendelee kuzalisha na kiweze kuwalipa wafanyakazi wake vizuri, kinataka kupata uhakika wa mauzo wa baiskeli 200 kwa siku.

Kiwanda kikaamua kumuajiri mtumishi mmoja mwenye PhD ya masoko (meneja masoko) ili aweze kutumia elimu yake katika kuhakikisha kwa siku, baiskeli zisizopungua 200 ziwe zimeuzwa.

Matokeo yake, huyu mtu ambaye ni meneja masoko akashindwa kutimiza lengo la kiwanda, na kutaka kulipwa kwa kuamini ana elimu sahihi.

Mwisho wa siku, kiwanda X kikamfuta kazi kwa sababu hana sifa sahihi za uzalishaji wa vitendo.

Cha kujifunza: Kabla ya kuanza kulalamika ajira hakuna, jifanyie tathmini kwanza, una sifa sahihi za uzalishaji kwa vitendo ukiachana na hizo karatasi ulizonazo?​
Kwa sasa kupata competent employee ni mtihani
 
Ni vyote kwa pamoja:
1. Elimu na vyeti husika vinapatikana kirahisi -rahisi mno lakini vyote vikiwa vimesha chakachuliwa sana. Can you imagine a graduate anashindwa kufanya hesabu za kuzidisha au kugawanya simple Numbers i.e Arithmetics eti ni mpaka atafute calculator. anasema kwani kalkuleta kazi yake nn na iko huko kwenye laptop yake?
2. Masomo/Course nyingine zimerahisishwa kiasi kwamba upatikanaji wake zipo on line i.e. kwa njia ya Mtandao na mtu mhitimu "anasemekana" amefaulu kabisa na kutunukiwa cheti.
3. Juzi kati hapo, mjukuu wangu (Ke) std.5 aliniuliza swali la F2 lililohusu Female Reproductive system - nikashangaa. Kweli huyo kiumri na akili yake vinaendana na somo hilo?? i.e. Syllabus itumikayo maShuleni kwa sasa esp. shule za msingi inaacha maswali mengi ya kujiuliza.
Mtoto wa std3 anajifunza what is physics! Imagine
 
Back
Top Bottom