Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Kongole mkuu.Wapo watakao kuja na vyeti vingi na ufaulu wa A+ na kusema wana sifa sahihi za kupata kazi, lakini ukiwapa kazi wafanye kwa vitendo wanashindwa na kupelekea kupata hasara au kushuka kwa mauzo/faida.
Mfano: Kiwanda X kinazalisha baiskeli 1000 kwa siku, na ili kiwanda X kiendelee kuzalisha na kiweze kuwalipa wafanyakazi wake vizuri, kinataka kupata uhakika wa mauzo wa baiskeli 200 kwa siku.
Kiwanda kikaamua kumuajiri mtumishi mmoja mwenye PhD ya masoko (meneja masoko) ili aweze kutumia elimu yake katika kuhakikisha kwa siku, baiskeli zisizopungua 200 ziwe zimeuzwa.
Matokeo yake, huyu mtu ambaye ni meneja masoko akashindwa kutimiza lengo la kiwanda, na kutaka kulipwa kwa kuamini ana elimu sahihi.
Mwisho wa siku, kiwanda X kikamfuta kazi kwa sababu hana sifa sahihi za uzalishaji wa vitendo.
Cha kujifunza: Kabla ya kuanza kulalamika ajira hakuna, jifanyie tathmini kwanza, una sifa sahihi za uzalishaji kwa vitendo ukiachana na hizo karatasi ulizonazo?
Mtaalamu wa miamba, halafu hajui mwamba upi wenye madiniUngetolea mfano fani nyingine mkuu hapo kwenye masoko ni pagumu kwa kweli
NIni kifanyike ili kuleta ufanisi kwa kile tunachokisomea?
Tatizo ni elimu au ni sisi wenyewe?Kongole mkuu.
Ni kweli na ndo mana siku za nyuma kulikuwepo kitu kinaitwa Induction na Probation period. Mwajiriwa mtarajiwa anafanya kazi chini ya mtu mwenye uzoefu kazini hata kama ni PhD holder. Muda ilikuwa ni mwaka1 au zaidi na Huyo supervisor anaweza akawa ni Diploma holder au 1st degree na atamwandikia Report ya Competence au Incomptent. Hivi vyeti vya Ku-google, Computer au kutumia AI... mmh!
Huo ni mfano tu, vitu vipo vingi?soko la baiskeli 😁😁😁hata wewe ungefeli mkuu
Ungetolea mfano fani nyingine mkuu hapo kwenye masoko ni pagumu kwa kweli
Au Mechanical Engineer lakini hajui hata kutengeneza opener ya kufungulia kizibo cha soda.Mtaalamu wa miamba, halafu hajui mwamba upi wenye madini
nakuelewa.lakini huwezi kutoka shule ukafiti moja kwa moja mtaani hata iweje.mtaa una mambo yake tofauti na shuleHuo ni mfano tu, vitu vipo vingi?
Ila uafisa masoko ni kutafuta lawama tuu kwa baadhi ya kazi, sasa uuze baiskeli 200 kwa siku ndo nini wakuu 😂
Waajiri wasiangalie vyeti pekee, watengeneze mazingira ya training kwa waajiriwa ili wawe vile watakavyo wao, bila kukimbilia judgment...NIni kifanyike ili kuleta ufanisi kwa kile tunachokisomea?
Yaani zote ni mbwembwe za kwenye makaratasi.Au Mechanical Engineer lakini hajui hata kutengeneza opener ya kufungulia kizibo cha soda.
Au Civil Engineer/Structural Engineer lakini hajui hata plasta au sakafu inatengenezwaje
Kuanzia mashuleni na vyuoni mfumo wa elimu ubadilishwe.NIni kifanyike ili kuleta ufanisi kwa kile tunachokisomea?
Ishu ya udaktari haiwez kuingia humu, kwan wagonjwa wasipokuja hosp utamlaumu daktari?Si ndio kazi ulioisomea? Au mwingine anaweza kusema yeye ni mtaalamu mbobezi wa magonjwa ya figo, halafu huku wagonjwa wanakufa na magonjwa ya figo.
Kwa nchi zetu hizi zinazoendelea inawezekana kufanya hivyo?Waajiri wasiangalie vyeti pekee, watengeneze mazingira ya training kwa waajiriwa ili wawe vile watakavyo wao, bila kukimbilia judgment...
Wapo waliopo maofisini zaidi ya miaka 30, lakini mambo ni yale yale.nakuelewa.lakini huwezi kutoka shule ukafiti moja kwa moja mtaani hata iweje.mtaa una mambo yake tofauti na shule