KC Dorothy: Leo Jeshi la Magereza limenizuia kumwona Lissu

KC Dorothy: Leo Jeshi la Magereza limenizuia kumwona Lissu

Wazee wako kijijini umewajulia hali?!
Ahsante baba, bahati mbaya wenye akili km wewe kizazi hiki ni wachachr sn. Tuna jamii ya vijana walalamishi ktk kila jambo, vijana wazushi, wavivu mpk ktk kufikiri. Vijana wasio na heshima kwa wakubwa zao, kwako kila mtu ni kutukana, kukejeli, kukebehi, ni kizazi cha nyoka hiki
 
ndo shangaa, mkewe na watoto hawajaenda kumwona mtu anatoka huko na majanaba anakuja kumsumbua mkuu wa gereza, asubiri tarehe 24 atamwona kwenye itv, shenzi kabisa
Siku ukitiwa ndani ndio utajua ulichoandika
 
IBADA YA PASAKA GEREZANI: KUMTEMBELEA TUNDU LISSU

Katika kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka mwaka huu, niliamua kuitumia siku hii kwa namna ya kipekee kwa kwenda kumtembelea Ndugu Tundu Antipas Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA na pia Mwenyekiti wangu katika Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), aliye katika Gereza la Ukonga.

Mnamo saa 3:00 asubuhi nilikuwa tayari nimewasili gerezani tukiwa tumeambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu, Ester Thomas. Cha kushangaza, baada ya kufika, tuliambiwa tupaki gari kwa dakika 10 nikisubiri maelekezo ya utaratibu wa kumuona. Hata hivyo, baada ya dakika hizo kupita, nilielezwa kuwa hatuwezi kumuona Ndugu Lissu kwa sababu anaruhusiwa kuonwa na watu watatu tu, ambao ni wanafamilia wake pekee. Tumefanya juhudi za kumtafuta Kamishna wa Magereza Tanzania zimegonga mwamba bila mafanikio. Tumekuwepo kwa masaa zaidi ya mawili hata fursa ya kumuona bwana jela imegomewa haturuhusiwi

Hili ni zuio lisilo la haki, linaloendeleza ukandamizaji wa demokrasia na ukiukwaji wa wazi wa sheria na haki za binadamu. Ni ishara ya kurudi kwenye enzi za giza za dhuluma, vitisho na utawala wa kiimla ambapo hofu inapandikizwa makusudi ili kuwakatisha tamaa Watanzania katika mapambano yao ya haki.

Wito wangu kwa Watanzania ni huu: Tusiogope, tushikamane tuisimamie kweli na haki. Tuwe thabiti katika kupambana na udhalimu wa serikali ya CCM.

Tukio hili limenikumbusha kwa uchungu jinsi ambavyo kumbukumbu zangu za kuwa na taifa huru zinafutwa polepole. Linaashiria kurudi kwa sura mpya ya ukoloni, ukoloni wa ndani ambao ni lazima tuupinge kwa nguvu zote.

Kampeni zote muhimu kwa ajili ya kuhakikisha tunaleta mabadiliko ya kweli katika nchi yetu zinapaswa kuendelea kwa ari na kasi zaidi. Tuendelee kusimama imara katika mapambano haya ya kutetea haki, kulinda demokrasia na kuhakikisha ustawi wa Watanzania wote.

Pasaka hii imenikumbusha maana ya matumaini, mshikamano, na nguvu ya kusimama pamoja kwa ajili ya haki.

Tusikate tamaa. Tushikamane.Tupambane. Tusonge mbele.
NO reform no election tuzuie uchaguzi usifanyike
 
Bora wamefanya vzr ulinzi wa Lissu ni muhimu Sana kwa sasa kuliko kitu chochote

Unafiki tu watu mmetoka juzi kusaliti upinzani kwa kusaini uhuni Leo ndio mnajifanya kwenda kwa Lissu kumtembelea

Kiufupi hatuwaamini tofauti yenu na maccm ni ipi?
Huyo Dorothy ni mnafiki anaenda kumuamgalia huku anachekea tumboni
 
We danga huna kazi ya kufanya au unataka utrend kupitia huyo kibaraka? Halafu magerezani siyo sawa na kwenda kwa mjombako kuna taratibu.sahiv tumewajua mkitaka kutengeneza maudhui km kawaida yenu wazushi mnazusha kuwa mmeenda kumwnona huyo mhaini, kumbe mtu umelaza makalio kitandani.
wanaweza mpelekea hata sumu
 
Back
Top Bottom