Kebehi dhidi ya Nyerere na Magufuli, ni ishara Watanzania wana uelewa mdogo. Viongozi hawa wajengewe kumbukizi

Ni kumkoseaheshina sana Mwalimu Nyerere kumfananisha na Magufuli. Utawezaji kulinganisha dimbwi na bahari?
 
Mara nyingi vichaa huamini kuwa wana uelewa mkubwa sana kuliko watu wote walio wazima. Ukiona upo yofauti na wengi, fanya tafakuri ili kujirambua kama umzima wa heri.

Kwa kipimo chochote kile hakina kipimo cha kumweka Magufuli karibu na Mwalimu.

Ilikuwa ni bahati mbaya sana kwa Taifa. Machache mazuri yaliyofanyika wakati wa utawala wa Magufuli hayatoshi kuyafuta mabaya yaliyofanyuka wakati wa utawala wake.

Sina shaka, huko mbeleni, watapatikana wa kuyairodgesha mabaya yote ili hata wasiotambue leo, watapata ufahamu.
 
Acha utani wa ajabu na kejeli kwa watanzania. Huwezi mfananisha Nyerere na Magu ata kidogo
 
Naona mmeamua kutafuta njia ingine ya kuipigania Legacy
Teh! Teheeeeee!!!!!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli kuna watu na viatu, yaani una akili timamu then unamkubali muuaji, mwizi na muongo kama Jiwe!!!!
 
Mkuu umeua bendi kabisa, unajua wajinga na masikini ni wengi kuliko werevu na watu makini? Sasa Jiwe alitembelea kwenye ujinga wao akiwaita wanyonge na wao wanafurahi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ungekuwa karibu ningekunasa kibao, yaani Nyerere wetu unamfananisha na takataka kweli????
 
Kila mtu anavigezo vyake vya kulinganisha mambo, mimi naona kuna baadhi ya mambo na sera wanalingana japoMagu alikuwamkali zaidi na hakutaka siasa za kijinga kwenye ukweli.
Nikikuuliza swali dogo kama la bei ya ndege alizonunua sidhani kama unajua, hapo bado ile 1.5 tr kama unajua ilienda wapi.
 
Kifo cha shujaa wa Africa kimewauma sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli kuna watu na viatu, yaani una akili timamu then unamkubali muuaji, mwizi na muongo kama Jiwe!!!!
Huwa naamin ktk utofauti wa kimawazo na mitizamo, ktk utofauti wa fikra na priority

Naamin ktk uongoz imara na sio laini, naamin ktk ujenzi wa taifa na sio kula taifa, naamin kweny uzalendo wa ndan na sio kusifiwa na westerners

Naamin pia kuwa niyapendayo mm na kuyaamin kuwa yafaa yanaweza yakawa vinginevyo kwa wengine na wala hakuna shida.

Pamoja na utofauti wetu huo wote, kuna jambo lipo common ktk maisha nalo n uhalisia wa mambo na ukweli.

JPM alikua kiongozi mzalendo sana, mfia nchi kwelikweli na aliyeipenda TANZANIA mno. Alitamn wananchi wawe na nguv wawe huru wawe na maisha mazur. NI NGUMU MNO MNO MNO KUIFUTA LEGACY YA JPM

JPM ni kama mtume kwa Tanzania hatokuja sahaulika daima na atapendwa na vizazi na vizazi. Jitihada zenu za Kumfuta JPM ktk historia ya TANZANIA ndio humuandika kwa wino wa dhahabu.

Kuhusu JPM hata ww hapo ulipo unajua ukwel kuwa alikua kiongozi shupavu na jabari kbsa
 
A
Jamaa alikuwa mwizi na muuaji hatari
Aliiba nini ndg yang...??? Alimuua nan...??? Huwez kuongelea wizi kipind cha JPM huko n kulogwa na pesa unazokula za kumchafua CHUMA.

Aliiba kitu gan au ufisadi gan yan... Ivi ukila pesa za kumchafua JPM ndio inabid kuwa na roho ya upofu kwa kias hicho... Waambie wakuongez mshahar kwa maan hiyo kaz n ngum sn.

Uvccm wezi sn wanatajana, kifaa cha milion 20 wananunua kwa 170 milions, ngorongoro imeuzwa kwa UAE na masai wanaondolewa, tozo kila kitu, mifumuko ya bei, maisha magumu, uongoz wa ovyo, safar zisizo na tija, usaliti uliokithiri, kesi za mchongo kwa viongozi wa upinzan, kuharibu vyama pinzan mfn NCCR

Huo kwako ndio uongozi, mikopo mpk nchi imewekwa mstari wa hatari na hakuna lolote la maana linafanyika... Shenzi kbsa

JPM hastahili hata kutamkwa na wajinga na mahaini kama nyie
 
Nyerere swa. Huyo mwingine kajenge sanamu nyumbani kwako uiabudu. Ukiona haitoshi chukua ushauri aliotoa Ayatolah Zito " Waende Chato wakafukue kaburi wachimbiwe pembeni" yote ni kumuenzi.
 
Kwa hiyo ulifurahia uchafuzi alioufanya magufuri kipindi cha uchaguzi?nazani utakuwa na matatizo,sababu hata waliokuwa huko nyuma viongozi wakubwa,hawakufurahishwa na alichokifanya ndiyo maana walimsnich mapema kabla hajaharibu inchi
Kufurahi ama kuhuzunika sii issue, democrasia ni jumba la sanaa - wala halihitaji huruma. Ukiweza kufanya - fanya, km huwez waachie wengine wafanye
 
Hakika
 
Sidhani kama unao uwelawa wa kutosha; ndiyo maana unathubutu kumweka Nyerere na Magufuli. Kama kuna watu wanamzungumzuia Nyerere, kwa hakika hawamkebehi bali wanakosoa tu baadhi ys sera zake na maamuzi. Hakuna binadamu aliyekamilika. Nyerere alikuwa kiongozi mzuri sana lakini bila shaka yoyote alifanya makosa. Wanaomzungumzia Magufuli wala siyo kwamba wanamkebehi kwa sababu haitoshi hata kidogo kufanya hivyo. Bali wanachojaribu tu kufanya ni kumlaani na kuonyesha jinsi ambavyo mifumo yetu ilivyokosea na kushangaa ilikuwaje nchi hii kupata kiongozi wa aina yake. Kwa hakika kuibuka kwake na kudumu kwake katika madaraka ni jambo ambalo kwa sasa litaendelea kushangaza wengi na bila shaka kuna siku mjadala huru na makini zaidi utakuja kufanyika. Hili haliwezi kupita hivi hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…