Huyu si ndie alichoma mitakataka na kufanya mitambiko ya kihindi mlangoni kabla hajaingia ofisini kama PM? Kwa tukio lile peke yake waingereza wasingemwacha! Ilikuwa matusi makubwa kwao!Kaosha CV,kushindwa ilikua lazima
Huyo hajui sera za nje za nchi alizozitaja. Atasubiri sana.Unadhani kuingia vitani na Urusi ni sera yake binafsi??
Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa katika kukabiliana na chama cha Labour.
Waziri Mkuu Sunak alisema wapiga kura wametoa "uamuzi wa kutisha" juu ya chama chake baada ya miaka 14 madarakani.
Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alisema watu kote nchini Uingereza walikuwa wametangaza kuwa "tayari kwa mabadiliko".
Katika hotuba yake ya kukubali kushindwa baada ya kushikilia kiti chake cha Richmond na Northallerton, Bw Sunak alisema: "Chama cha Labour kimeshinda Uchaguzi huu Mkuu na nimempigia simu Sir Keir Starmer kumpongeza kwa ushindi wake."
Bw Sunak aliongeza: “Leo, tutabadilishana mamlaka kwa njia ya amani na yenye utaratibu na nia njema kwa pande zote. "Na ni jambo ambalo linapaswa kutupa imani sote katika utulivu na mustakabali wa nchi yetu."
"Watu wa Uingereza wametoa uamuzi mzito usiku wa leo, kuna mengi ya kujifunza ... na ninawajibika kwa hasara hiyo. Kwa watahiniwa wengi wazuri, wa Kihafidhina waliofanya kazi kwa bidii ambao wamepoteza usiku wa leo, licha ya juhudi zao zisizo na kuchoka, rekodi zao za mitaa na utoaji, na kujitolea kwao kwa jumuiya zao. Samahani."
=====
Pia soma: UK General Election: Waingereza leo kupiga kura kumchagua Waziri Mkuu na Wabunge
Miezi 18Huyu jamaa kakaa madarakani muda gani ?
Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa katika kukabiliana na chama cha Labour.
mkuu usiniambie hujui namna walowezi wa kingereza walivyoweza kufyeka wenyeji wote katika nchi hizo!Duh!...mpya hii
hahahaaaaa.......Sentence ilikuwa tata kwako. Nimeirekebisha.
Ndio tatizo lilianza hapo,amwulize Thabo Mbeki na Victoria SabuniHuyu si ndie alichoma mitakataka na kufanya mitambiko ya kihindi mlangoni kabla hajaingia ofisini kama PM? Kwa tukio lile peke yake waingereza wasingemwacha! Ilikuwa matusi makubwa kwao!
Hizo sababu zote ulizotaja chanzo chake ni kudorora kwa uchumi. Sababu ya kudorora ndo hiyo ya kuburuzwa na Marekani kujiingiza kwenye vita ya Urusi vs UkraineHizi sababu ni zako binafsi wala siyo ambazo zimefanya Tories washindwe uchaguzi. Waingereza wana shida zao kama kupanda kwa kugharama za makazi, huduma mbovu za afya (NHS) na masuala mazima ya uhamiaji ambao waingereza wengi wanaupinga kwa sababu ndo sehemu ya kuongezeka kwa gharama ya maisha na kuongeza pressure kwenye huduma za afya.
Suala la vita ya Urusi vs Ukraine wote sera yao ni moja ambayo ni kuisaidia Ukraine dhidi ya Urusi.
Kwa taarifa yako tu Tory imeanza kuchokwa tangu mwaka 2021 kipindi ambacho Waziri Mkuu alikuwa Boris Johnson, baadaye Ritz Truss Waziri Mkuu ambaye aliweka rekodi ya kukaa muda mfupi zaidi (Siku 44) ndo akaja Sunak. Conservative kushindwa uchaguzi ni kitu ambacho kilikuwa hakikwepeki japo hata hiyo Labour yenyewe Waingereza hawaimini ndo maana chama kama Reform UK ambacho kinapinga Uhamiaji kimepata kura nyingi japo hakijapata viti vingi vya bunge.
Vita vya kujitakia na utitiri wa wahamiaji haramu umegharimu mataifa mengi ya dunia ya kwanza.Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.
Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.
Hii coment inatakiwa iekewe laminationSema Uingereza ni nchi inayoelekea kufeli kiuchumi. Kinachoifanya iendelee kujikongonya ni uimara wa pesa yao tu. Wananchi wanataka kumantain standard yao ya maisha wakati hali haziruhusu.
Na watangulizi wake nawo hawakua syrong?hajatoka kwasababu ya kuipiga vita urusi bali kwasababu Rish hakuwa strong hivyo wanahitaj mtu atakae irudisha heshima ya UK na kulinda tamaduni zao UK
Sirikali zinazoondoka hapo uingereza sio sababu ya makosa madogo kama unavyotaka kuaminisha watuUingereza iko top 10 kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani. Wako hivyo sababu hawakubali kulea madhaifu madogo, huwezi kazi tembea aje mwingine.
Badala ya kukaa kwa sifa ya kuongozwa na serikali moja kwa miaka 20 eti tuna imani, wao umekosea sera moja ondoka.
Reporting ........Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.
Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.