Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Kanji aliwekeza kimbelembele kwenye vita ya Urusi na Ukraine akasahau waingereza wanampimia tu hawali mabomu.

Huyu mpya kama zinamuingia nae aende kwa akili vinginevyo watamla kichwa soon tu.
Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa katika kukabiliana na chama cha Labour.

Waziri Mkuu Sunak alisema wapiga kura wametoa "uamuzi wa kutisha" juu ya chama chake baada ya miaka 14 madarakani.

Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alisema watu kote nchini Uingereza walikuwa wametangaza kuwa "tayari kwa mabadiliko".

Katika hotuba yake ya kukubali kushindwa baada ya kushikilia kiti chake cha Richmond na Northallerton, Bw Sunak alisema: "Chama cha Labour kimeshinda Uchaguzi huu Mkuu na nimempigia simu Sir Keir Starmer kumpongeza kwa ushindi wake."

Bw Sunak aliongeza: “Leo, tutabadilishana mamlaka kwa njia ya amani na yenye utaratibu na nia njema kwa pande zote. "Na ni jambo ambalo linapaswa kutupa imani sote katika utulivu na mustakabali wa nchi yetu."

"Watu wa Uingereza wametoa uamuzi mzito usiku wa leo, kuna mengi ya kujifunza ... na ninawajibika kwa hasara hiyo. Kwa watahiniwa wengi wazuri, wa Kihafidhina waliofanya kazi kwa bidii ambao wamepoteza usiku wa leo, licha ya juhudi zao zisizo na kuchoka, rekodi zao za mitaa na utoaji, na kujitolea kwao kwa jumuiya zao. Samahani."

=====

Pia soma: UK General Election: Waingereza leo kupiga kura kumchagua Waziri Mkuu na Wabunge
 
Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa katika kukabiliana na chama cha Labour.

Keir Starmer hatakuwa Waziri Mkuu baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa.

Keir Starmer atakuwa Waziri Mkuu baada ya Rishi Sunak kushindwa.

Mwisho! Period, point blank!

Kule huingii madarakani mwenzio akikubali uingie!

Unaingia ukishinda!

Amekubali, hajakubali!

Futa kichwani mwako hayo ma third world mentality potofu yanayokufanya mpaka unakosea hata kunakiri vichwa vya habari vya wenzio
 
Duh!...mpya hii
mkuu usiniambie hujui namna walowezi wa kingereza walivyoweza kufyeka wenyeji wote katika nchi hizo!

hata hapo Israel, laiti tungekua miaka ya giza, hao wapalestina wangefyekelewa mbali zamani sana, sema ndio hivyo wamepata hio idea miaka ya 1900 mwanzoni kabisa (ndipo walianza kupeleka walowezi wa kwanza wa kingereza hapo),

hujiulizi kwanini ni UK ndiye alianzisha mpango wa kuwarudisha 'wayahudi' hapo?

as of US, Canada, New Zealand, Australia hili lipo hata mitandaoni, ni walowezi wa kingereza ndio walifyeka wenyeji wote kwenye hizo nchi.......

unakumbuka walichokifanya Diego Garcia? waliondoa wenyeji wote na sasa ni base ya kijeshi ya US (ofcoz alikodishiwa na UK kwa miaka 50,), kile kisiwa ni 'mali' ya UK mpk leo ila amekodi US ndio kaweka base ya kijeshi pale......

kwa afrika walijaribu kwa madiba, ikawa too late....... wadachi wamewasumbua sana, pia nadhani mazingira ya wakati huo na nature ya eneo lenyewe iliwasumbua! wao walitaka kuifanya ile 'rasi ya tumaini jema' kuwa nchi, but mazingira hayakuruhusu ndio mana sauzi ipo pale ilipo!
 
Huyu si ndie alichoma mitakataka na kufanya mitambiko ya kihindi mlangoni kabla hajaingia ofisini kama PM? Kwa tukio lile peke yake waingereza wasingemwacha! Ilikuwa matusi makubwa kwao!
Ndio tatizo lilianza hapo,amwulize Thabo Mbeki na Victoria Sabuni
 
Hizi sababu ni zako binafsi wala siyo ambazo zimefanya Tories washindwe uchaguzi. Waingereza wana shida zao kama kupanda kwa kugharama za makazi, huduma mbovu za afya (NHS) na masuala mazima ya uhamiaji ambao waingereza wengi wanaupinga kwa sababu ndo sehemu ya kuongezeka kwa gharama ya maisha na kuongeza pressure kwenye huduma za afya.
Suala la vita ya Urusi vs Ukraine wote sera yao ni moja ambayo ni kuisaidia Ukraine dhidi ya Urusi.
Kwa taarifa yako tu Tory imeanza kuchokwa tangu mwaka 2021 kipindi ambacho Waziri Mkuu alikuwa Boris Johnson, baadaye Ritz Truss Waziri Mkuu ambaye aliweka rekodi ya kukaa muda mfupi zaidi (Siku 44) ndo akaja Sunak. Conservative kushindwa uchaguzi ni kitu ambacho kilikuwa hakikwepeki japo hata hiyo Labour yenyewe Waingereza hawaimini ndo maana chama kama Reform UK ambacho kinapinga Uhamiaji kimepata kura nyingi japo hakijapata viti vingi vya bunge.
Hizo sababu zote ulizotaja chanzo chake ni kudorora kwa uchumi. Sababu ya kudorora ndo hiyo ya kuburuzwa na Marekani kujiingiza kwenye vita ya Urusi vs Ukraine
 
Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.

Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.
Vita vya kujitakia na utitiri wa wahamiaji haramu umegharimu mataifa mengi ya dunia ya kwanza.

UK iligeuka kuwa kama Mumbai sijui Pakistani etc

Lengo kuu kwa utawala mpya Europe North America ni kusafisha nchi zao.

Kutakuwa na deportation kubwa kwa hizi nchi..
 
Sema Uingereza ni nchi inayoelekea kufeli kiuchumi. Kinachoifanya iendelee kujikongonya ni uimara wa pesa yao tu. Wananchi wanataka kumantain standard yao ya maisha wakati hali haziruhusu.
Hii coment inatakiwa iekewe lamination
Ila uingereza ishafeli tayari sema pesa yake inaifanya tu isianguke kwa haraka ila anguko la uingereza kiukweli halikwepeki kwenye hio angle ya uchumi nisuala la muda tuu
 
hajatoka kwasababu ya kuipiga vita urusi bali kwasababu Rish hakuwa strong hivyo wanahitaj mtu atakae irudisha heshima ya UK na kulinda tamaduni zao UK
Na watangulizi wake nawo hawakua syrong?
 
Uingereza iko top 10 kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani. Wako hivyo sababu hawakubali kulea madhaifu madogo, huwezi kazi tembea aje mwingine.

Badala ya kukaa kwa sifa ya kuongozwa na serikali moja kwa miaka 20 eti tuna imani, wao umekosea sera moja ondoka.
Sirikali zinazoondoka hapo uingereza sio sababu ya makosa madogo kama unavyotaka kuaminisha watu
Kuhusiana na suala la uingereza kwamba wapo na uchumi kama unavyosema hili lipo wazi
Ila ukweli nikwamba kwamiaka sasa zaidi ya kumi uingereza uchumi wake haupo stable gharama za maisha zipo juu
Uingereza kwasasa wanagawa mpaka vyakula kwa watu kisa tu hawana uwezo wakujinunulia wenyewe uingereza inflation imekua juu sana kodi za majengo zimekuaa juu sana kodi za umeme maji nk zimekua juu sana
Sunak katoka kwa kushindwa kuueka uchumi wa UK walau ukatengemaa na haujaanzia kwakw yeye kafanywa tu mbuzi wa kafara kwakweli
UK wanahitajia wafanye kazi laa sivyo baada ya miaka miwili kama itafika watafanya tena uchafuzi kama wajuzi halaf watu watakuja kuwasifu hapa kama wana demokrasia kumbe ni kufeli kwa sirikali zao kila muda
 
Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.

Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.
Reporting ........
 
Back
Top Bottom