Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Uingereza raia wake ni too demanding na wana deko la kuwa na historia ya viongozi wazuri zamani. Hawaridhiki na hawakubali mapungufu kidogo au uwezo pungufu kidogo wa kiongozi. Na hawana muda wa tumpe muda sijui tuwe na imani, mara anashauriwa vibaya. Wao ukifanya kosa moja ndio wamemaliza hivyo hawana imani na wewe.
Well Said Mkuu, sisi TZ ndio bado tuna “ tumpe muda”… hizi tumpe muda hakunaga huko UK…
 
Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa katika kukabiliana na chama cha Labour.

Waziri Mkuu Sunak alisema wapiga kura wametoa "uamuzi wa kutisha" juu ya chama chake baada ya miaka 14 madarakani.

Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alisema watu kote nchini Uingereza walikuwa wametangaza kuwa "tayari kwa mabadiliko".

Katika hotuba yake ya kukubali kushindwa baada ya kushikilia kiti chake cha Richmond na Northallerton, Bw Sunak alisema: "Chama cha Labour kimeshinda Uchaguzi huu Mkuu na nimempigia simu Sir Keir Starmer kumpongeza kwa ushindi wake."

Bw Sunak aliongeza: “Leo, tutabadilishana mamlaka kwa njia ya amani na yenye utaratibu na nia njema kwa pande zote. "Na ni jambo ambalo linapaswa kutupa imani sote katika utulivu na mustakabali wa nchi yetu."

"Watu wa Uingereza wametoa uamuzi mzito usiku wa leo, kuna mengi ya kujifunza ... na ninawajibika kwa hasara hiyo. Kwa watahiniwa wengi wazuri, wa Kihafidhina waliofanya kazi kwa bidii ambao wamepoteza usiku wa leo, licha ya juhudi zao zisizo na kuchoka, rekodi zao za mitaa na utoaji, na kujitolea kwao kwa jumuiya zao. Samahani."

=====

Pia soma: UK General Election: Waingereza leo kupiga kura kumchagua Waziri Mkuu na Wabunge
Demokrasia hiyo......

Angalau hata UK wameepuka. kiongozi wa mrengo ule wa kulia...hawa jamaa wasumbufu.
 
Uingereza raia wake ni too demanding na wana deko la kuwa na historia ya viongozi wazuri zamani. Hawaridhiki na hawakubali mapungufu kidogo au uwezo pungufu kidogo wa kiongozi. Na hawana muda wa tumpe muda sijui tuwe na imani, mara anashauriwa vibaya. Wao ukifanya kosa moja ndio wamemaliza hivyo hawana imani na wewe.
Ikitokea na Trump ameshinda Urais USA, hiyo vita ya Ukraine na Urusi haipo mbali kumalizika.
 
Yalioikumbuka uingereza sio mapungufu kidogo
Unadhani ma PM wote watano walikua na mapungufu madogo madogo kama usemavyo
Kiukweli UK kuna majambo hayapo sawa haiwezekani nchi kama UK ndani ya miaka 7 sijui 8 wawe washabadilisha PM zaidi ya watatu kisa jambo dogo tuuu
Uingereza iko top 10 kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani. Wako hivyo sababu hawakubali kulea madhaifu madogo, huwezi kazi tembea aje mwingine.

Badala ya kukaa kwa sifa ya kuongozwa na serikali moja kwa miaka 20 eti tuna imani, wao umekosea sera moja ondoka.
 
Demokrasia hiyo......

Angalau hata UK wameepuka. kiongozi wa mrengo ule wa kulia...hawa jamaa wasumbufu.
hujui kama Sunak ni mlengo wa kulia?
kuanzia 2010 wameongozwa na mlengo wa kulia mpk leo Sunak anaondoka!

yumkini hujui kuwa torry ni right wing[emoji1787]
 
Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.

Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.
Sera za Uingereza za kuingia vitani au kutokutenda hiyo siyo kazi ya PM bali ni kazi ya vitengo vya usalama na sera zao za ma,ni ya nje. Utaona kama huyo waziri mkuu hataisaidia Ukraine
 
Pamoja na ushindi mwingereza amepoteana sana; wamethibitisha kuwa si wale watu tulioamini 'wana akili'.
Labour wakiweza kukwepa mitego hatimaye kutoburuzwa na US nitahisi wameanza kujitambua.
Wewe ndio huna akili kabisa, huwezi kuwatenganisha, UK, USA na Israel ni kitu kimoja.

Huelewi hata dunia inavyokwenda.
 
Ikitokea na Trump ameshinda Urais USA, hiyo vita ya Ukraine na Urusi haipo mbali kumalizika.
Trump hata akishinda hana uwezo wa kupingana na US interest.

Ndio maana FBI na CIA wako huru pamoja na vyombo vyao vingine.

Trump anakaa ikulu anaambiwa moja mbili tatu na kwa nini.
 
Pamoja na ushindi mwingereza amepoteana sana; wamethibitisha kuwa si wale watu tulioamini 'wana akili'.
Labour wakiweza kukwepa mitego hatimaye kutoburuzwa na US nitahisi wameanza kujitambua.
mkuu zinduka usingizini,
british empire haijawahi kufa, na nchi zinazounda hio empire ni UK yenyewe,US, Canada, New Zealand, Australia, na Israeli,....... (hizo nchi zote ni waingereza hao, hakuna myahudi humo)
 
Duh!...mpya hii
 
Back
Top Bottom