Maamuzi ya kuahirisha mpira wa jana ni kati ya maamuzi mabovu kuwahi kufanyika
Kwa sababu sababu zilizokuwepo hazikuwa na uzito wa kutosha kuahirisha mpira
1. Kitendo cha Simba kupeleka team uwanjani bila taarifa jioni/usiku, kilitosha kabisa kuwazuia kwa sababu; uongozi wa Uwanja unatakiwa kuwa na taarifa ili kuweka mazingira sawa ikiwepo kuwa na walinzi, wafanyakazi nk kwa ajili ya kusimamia taratibu za uwanja.
2. Kimsingi waliozuia Simba isiingie uwanjani ni walinzi wa uwanja, hata kama kulikuwa na washabiki wanao dhaniwa ni wa Yanga maeneo ya uwanjani....
3. Tusiaminishwe kuwa washabiki wachache tu ndio wenye nguvu ya kufanya kazi ya ulinzi wa uwanja kuliko wafanyakazi/walinzi wa uwanja walio ajiriwa.....tukiamini hivyo kuna siku team zitazuiwa kwenda uwanjani ili team nyingine ipate point tatu....
4. Mimi bado naamini team ya SIMBA ILIZUILIWA na walinzi wa uwanja kwa kutokufuata taratibu (kwenda uwanjani jioni/usiku bila taarifa) hayo ya mashabiki wa Yanga yamejazilishiwa tu.....
Kimsingi sababu zilikuwa Nyepesi ukiangalia gharama za maandalizi na washabiki ambao wengi tu walisafiri kutoka mikoani na Nnje ya Nchi. Inamaana mechi za Yanga na simba wanaenda kuzipunguzia ushabiki (fedha) kwani hakuna mtu ataliipa hela yake kwenda dar wakati kwa sababu nyepesi nyepesi mechi inaweza kuaharishwa!