clarewency
Member
- Sep 10, 2024
- 24
- 20
Utaratibu wa Timu kupewa pointi 3 baada ya timu nyingine kutofika uwanjani upoje? Maana:Usilete matusi Yako hapa,
Nimeamka nimepitia Mitandao yangu pendwa miwili X formerly known as Twitter na JF.
Nilichokiona hata waliokua wanatetea swala la Simba mapema Ile wamegeuka nao saiv wanailaumu Bodi.
1. Ilitakiwa Yanga wafike uwanjani muda wa mchezo husika.
2. Kuwe na viongozi wote wa mechi husika wakiwemo makamishina na refarii uwanjani ambaye atawaongoza waingie uwanjan muda ukifika.
3. Saa moja na robo refarii angepuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa mchezo.
4. Refarii angesubiria timu nyingine iingie uwanjani kwa muda wa dakika 15.
5. Baada ya dakika 15 kutimia bila timu nyingine kuingia uwanjani, refarii angemaliza mechi na timu iliyokuwepo uwanjan ingepewa ushindi na alama 3.
Je! kwa jana hayo yote yalikamilika ili Yanga wapewe ushindi na alama 3 kama kichwa cha habari cha bandiko hili kinavyodai?