Kelele zikiwa nyingi na kuwazomoea Bodi Kwa Maamuzi ya Kijinga, msije kushangaa Yanga anapewa Point 3 maana washaanza kuraruana tayar.

Acha kukurupuka, mpira huu siyo wa makaratasi, una kanuni kasome uache mazoea.
 
Bodi ya Ligi huu unaweza kua uzi wenu wakupata mawazo kutoka kwa umma.
 
Oky umeonekana Asante Kwa Mchango wako.
 
Kama mlijua walipanga si mngewaruhusu waingie uwanjani kupiga tizi ili wasipate sababu?
 
Ni wazi kolo kala kona , walianza kugomea marefa, juzi wakafanya ambush uwanjani, wakaenda na waandishi wao kabisa si ajabu hata hao mabounsa ni wao.
Mwanzo mlikuwa mnasema simba kwa nini afanye mazoezi usiku, ooh kwani siku zote hawajafanya mazoezi, sasa hivi mmejua kanuni inawalalia mnaanza kujitoa kwa kuwabambikia mabaunsa kuwa siyo wa kwenu, asiye wajua nani wakati kila siku mnasafiri nao ktk kila mechi na sura zao zinaonekana. Technolojia ipo ndugu acheni kujificha ktk shamba la karanga.
 
Punguza jazba, leta timu mechi ikipangwa tena la sivyo mnafatwa hukohuko bunju.

Zoezi la dk 30 ndio lifanye ushindwe kucheza mechi, koro kala kona hilo liko wazi, hamna cha mabaunsa wala mabodyguard.

Yaani simba ya wale wang'oa viti washindwe kuingia uwanjani hapo, no janjajanja za kukimbia kipigo hizo.
 
Mpira wetu una siasa nyingi utashangaa MAZA anasema mbugi lipigwe sasa nani atabisha? Uliona ishu ya UGALI SUKARI ilivyomalizwa?
Ndio siasa zenyewe hizo, mambo ya kikanuni yanaamuliwa kimamlaka.
 
Hiyo kanuni inatambua ushirikina? Onesha kanuni inayosema timu ikizuiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa ugenini mechi inahairishwa.
 
Simba waliyajua mapungufu yao na ya bodi ya Ligi, Simba SC kama taasisi Wana kesi ya kujibu walikulupuka kutoa taarifa ya kuto shiriki mtandaoni badala ya kuwasiliana na mamlaka husika kwakifupi hawakuwa makini, (not smart)

Je TFF na Bodi ya Ligi wana weledi wa kusimamia Ligi yetu ama wako kama sanamu hivi- figure heads

Viongozi wa TFF hawana elimu ya ujasiriamali wanaendesha shirikisho kama familia ama ndondo cup najaribu kuangalia hasara ya matangazo na maandalizi ya mchezo husika pamoja na gharama za mashabiki na makundi ya football scouting
 
Kosa hili huenda limesababishwa na maagizo kutoka juu kwani kukosa mazoezi ya saa moja si sawa na wachezaji kupata ajali mbaya.Bodi imeingizwa mkenge na yanga ana haki ya point na mitano tena
 
Hiyo kanuni inatambua ushirikina? Onesha kanuni inayosema timu ikizuiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa ugenini mechi inahairishwa.
Soma vizuri kanuni ya 31 inatoa mwanya wa timu kugomea, ndiyo inasema ikiwa timu itagomea "bila sababu ya msingi inayokubaliwa na tff" huu ina maana kuwa mchezo unaweza kutochezwa ikiwa tu kutakuwa na sababu ya kikanuni inayokubaliwa na tff.
 
Kwenye hizo kanuni wapi wapenzi wa mpira wanalindwa? Yaani watu wapoteze muda na pesa kusafiri kutoka Zambia alafu mechi isichezwe kisa kuna timu imezuiwa kufanya mazoezi ya dakika 30.
 
Wewe ndiyo unakurupuka bila kuzisoma kanuni kwa kina. Soma kanuni ya 31 inatoa mwanya wa timu kugomea mchezo ikiwa kuna sababu inayokubalika kikanuni.
Naomba hiko kifungu cha kanuni mkuu kama hutajali. Natanguliza shukrani.
 
kwa hiyo Baada ya kughairisha wakaacha wazi mpaka jioni?
Na yanga nao licha ya mechi kughairishwa wakaenda hivyo wakiwa wanajua hakuna maofisa wa mchezo,marefa wala watu wa bodi ya ligi?
kama ni hivyo Haji manara Apewe hadhi ya udokta wa maono.
Rage ashapewa PhD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…