Kenani Kihongosi: Siungi mkono mamlaka ya Rais kupunguzwa

Kenani Kihongosi: Siungi mkono mamlaka ya Rais kupunguzwa

Akitaka ufe leo unakufa, au unabishi? Akiagiza uuawe unauawa!
Akiagiza hakuna kumtangaza mpinzani hata kama ameshinda uchaguzi na hatangazwi!!! Akiagiza tujifikize kwa mitishamba halafu wataalamu wakikosoa wanaadhibiwa!!! Ambaye hakosolewi si mungu huyo??
Mifano hai ipo mingi labda ujitoage ufahamu
Trump hana hayo mamlaka?
 
Huu ubishi sasa mbona South Korea, Brazil, France, Peru, Argentina, Chile , Columbia au tuweke na majina yao, zilikuwa kesi gani?
Ahsante sana kwa kurudia kutoa mifano ambayo nimeishaitaja. Na kwa mifano, je, ndio ihalalishe na sisi tuwe kama wao? Kuna nchi ngapi duniani hazifanyi hivyo na mambo ya naenda?
 
Kenani Kihongosi: Mimi siungi mkono mamlaka ya Rais kupunguzwa ila wananchi milioni 61 wanataka!
 
SAsa kwenye ile reply ulikuwa unauliza nini wakati ulikuwa unazijua?
Hoja ni kwamba hizo nchi ni chache sana kuishawishi Tanzania kuwaiga. Pia pamoja na kuwa na hiyo sheria haijawahi kuwasidia. Peru zaidi ya Marais Saba wameshtakiwa. Imewasaidia nini? Korea Kusini pamoja na hiyo sheria Kuwepo, bado ndio nchi inaongoza kuwa na Marais na ndugu zao wala rushwa! Inawasaidia nini?
Sisi Tanzania kuna mtu anaweza kutoa ushahidi kuwa Marais Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia wanalijihusisha au wanajihusisha na rushwa? Seriously?
 
Tulia we kiazi hujui lolote. Google maana huna ujualo. Nenda kasome kuhusu kashfa ya Bill Clinton ya Monica Lewinsky na nini kingemkuta akiwa madarakani, ndio utajua huna ujualo ww kiazi mbatata.
Ndio maana nikakwambia hujui tofauti ya Court Trials na Impeachment! Ahahahahaha!!
Alichotaka kufanyiwa Bill Clinton ni Impeachment! Ahahahahaha! Hata Tanzania hiyo sheria ipo. Fuatilia

Lakini kwa Marekani hiyo hiyo, huwezi kumshtaki Rais mahakamani akiwa Rais au baada ya kutoka! Na kwa taarifa yako nyingine dogo, Rais wa Marekani ana mamlaka ya kusaini mtu yeyete "asishtakiwe" kwa makosa aliyoyafanya akiwa mtumishi.

Na mamlaka anakuwa nayo hasa pale mwishoni anapojiandaa kutoka ofisini. Na Rais mwingine akiingia hawezi kukiuka! Fuatilia dogo!
 
Back
Top Bottom