Kenge ana madhara gani kwa Binadamu?

Kenge hana madhara kwa binadamu,zaidi kuiba tukuku twako. Kenge nae anamkimbia binadamu. Labda akikakuta katoto mmekalaza nje hapo kwenye huo mwembe anaweza akajitwisha akapita nako. Lakini huyo ni wale wakubwa kabisa. Zaidi hapo hana madhara
 
chai hii
 
Mkuu kwani umeenda kuishi ukengeni ama?
 
Kuna bwana mmoja alienda kukata kuni alivyochoka akalala kenge akatokea akamuingiza ulimi puani jamaa alivyoamka aliona kichwa chepesi alivyoenda hospital kuchekiwa akaonekana hana ubongo aliula wote kenge.
Hii chai nimeipiga teke
 
Uongo huu maana ubongo ulipo na pua ni mbali japo kuna connection ndogo
 
Hii stori ya kenge kunyonya ubongo sijui ilitokea wapi.

Stori ndefu fupi, huo ni uongo.

Kenge ni mwoga. Ana speed ambayo huitumia kukimbia na siyo kushambulia.

Kenge ni hatari kwa mifugo midogo, mfano kuku, bata, sungura na mayai.

Kenge ambaye analinda mayai yake huweza kujaribu kutishia kwa kutoa sauti na kufanya bluffing moves ila akiona umesimama kidete huretreat na kukimbia.

Ambacho ni hakika ni kua kenge atashambulia mtoto mchanga kwakua mtoto mchanga hawezi msukuma kenge. Kuna familia zingine Ulaya zinafunga kenge lakini hua hawawi chanzo cha fatal accident.

Ingekua ubongo unatoka kwa kuvutwa na ulimi, sasa si mtu ukipenga kamasi ungeona na ubongo unatoka?
 
Huu ndiyo ukweli
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hizi stori tulikuwagaga tunapigianaga enzi za primary
 
Ungeeleza wanakutishaje.. na kivipi unahofu.. hao unaweza fanya wakimbie ila usiwatishe kujiona kama wataumia hapo ndio wanakuwa wakali

Natumaini utapata suruhisho.. ongea na majirani zako uwaulize pia.. na najua palipo na kuku na mayai wanapenda kuwepo sana hata kwa mabanda wanaweza kuchimba shimo na kuingia kwenye banda.

Soma hapa pia labda itakusaidia
Wanaitwa Nile monitors kwa kimombo

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…