Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #101
Dalmine,
Amin kwa sote na Allah ajaalie viongozi wetu wajue kuwa tunajemga fitna kubwa kwa hii hali ambayo siku moja tutakuja kujuta.
Allah awajaalie viongozi na wauone huu ukweli na wafanye marekebisho kwani dhulma inaangamiza.
Kipuyo,Salaam Aleykum sheikh Mohamed Said!
Nilisubiri kwa hamu uandike Taazia/Tanzia ya Hayati Magufuli kipenzi cha wanyonge wakiwemo waislamu.
La Pili nilitamani sana Rais wetu ateue waislamu tupu kwenye sehemu zote ili tupunguze kelele za daraja la pili la watanzania.
Ahsanta
Daraja la kwanza ni ninyi Waislamu.Kipuyo,
Hili suala la mimi kuandika taazia ya JPM nimelijibu kuwa sikupata kumfahamu kwa kiwango cha kuweza kumuhadithia.
Suala la kuteua Waislam watupu hii itakuwa dhulma.
Hivi sasa uwiano ni 20:80 katika serikali na hili halipendezi kuwepo kwenye nchi yeyote yenye waumimi wa imani mbili tofauti moja ikahodhi fursa zote.
Ikiwa sasa utakuwa na Tanzania ambayo Wizara ya Elimu yote iko mikononi kwa Waislam hii ni dhulma na kukaribisha fitna.
Kutahadharisha serikali katika kulinda haki na usawa haijapata kuwa kelele.
Nashukuru kwa kutambua kuwa tunalo daraja la kwanza.
Kipuyo,Daraja la kwanza ni ninyi Waislamu.
Ukisafiri kwa njia ya barabara karibu kona zote za nchi,hoteli zote zilizopo pembezoni mwa barabara kwa ajili ya abiria kupata chochote zinamilikiwa na waislamu,je kwa nn nisiseme ninyi ni raia daraja la kwanza kwa nchi yetu?
Pili,Matajiri wakubwa nchi hii ni ninyi,kwa nn nisiseme ninyi ni raia daraja la kwanza nchi hii?
Tatu,ukitaka kuchinja nyama kwa matumizi ya watu wengi,lazima ichinjwe na muislamu,sasa kwa nn nisiseme nyie ni daraja la kwanza?
Kilichobaki ni nyie kupewa wizara zote ili tutulie
Huwa mnalishwaga sumu huko nyie..haha..hv wazir mzima aanze kuhangaika na matokea na shule ya kiislam ili iweje labda?? Wacheni kulalamika mzee..somesheni watoto elimu dunia wacheni kuwachanganyia na lugha za kiarabu ndo mana wanashindwa kumudu darasan..Lupweko,
Hii hapo chini kanitumia msomaji mmoja:
"Nakumbuka Prof. Ndalichako alipokuwa Mkurugenzi wa Elimu kuna skuli moja ya Kiislamu walifelishwa skuli nzima.
Baada ya Waislam kufuatilia ndio Wizara ikaomba radhi na kusema kuna makosa ya bahati mbaya.
Sitasahau kadhia hiyo na zawadi ya Prof. ikawa ni kuwa, "Promoted to a full ministerial post. Minister of education to date."
J,Kiongozi ebu elezea hiyo dhulma bas japo kidogo na sisi vijana tuzijue..mana naskia huwa waislam wanalalamika wanafanyiwa dhulma..ni zipi hizo?
J,Huwa mnalishwaga sumu huko nyie..haha..hv wazir mzima aanze kuhangaika na matokea na shule ya kiislam ili iweje labda?? Wacheni kulalamika mzee..somesheni watoto elimu dunia wacheni kuwachanganyia na lugha za kiarabu ndo mana wanashindwa kumudu darasan..
Msamehe bure,uzee umemfanya asahau mengiHuyu mzee wetu ana udini sana.
KAULIZA MWENYE KUULIZA ITAKUWAJE HISTORIA MPYA INAYOANDALIWA IKIFANANA NA HII HISTORIA YA SASA?Msamehe bure,uzee umemfanya asahau mengi
Wanaokuheshimu kwa udini unaoeneza wa shida vichwani mwao.KENYA ABDALLAH HASSAN KATIBU MKUU WA KWANZA MUISLAM WIZARA YA ELIMU AMEFARIKI
Kenya Abdallah Hassan nimemfahamu toka utoto wangu Moshi katika miaka ya 1960.
Siku hizo mimi nikiwa shule ya msingi madarasa ya chini sana yeye alikuwa Mawenzi Secondary School.
Kenya alikwenda Makerere, Uganda nilikuja kujua baadae.
Kenya angefariki na mimi wala nisingenyanyua kalamu yangu kuandika chochote kuhusu yeye kama isingetokea mwaka wa 1987 jambo lililogusa Waislam wengi Tanzania.
Mwaka huo Prof. Kighoma Malima alichaguliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Waziri wa Elimu.
Hili lilikuwa halijapata kutokea.
Ilikuwa kama vile Rais Mwinyi amevunja mwiko alioweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere toka uhuru mwaka wa 1961kuwa nafasi hiyo haishikwi na Muislam.
Baada ya kuwa Waziri wa Elimu Prof. Malima Rais Mwinyi akamchagua Kenya Abdallah Hassan kuwa Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.
Rais alikuwa kapiga msumari wa moto juu ya kidonda.
Wizara ilichafuka na wahariri wa magazeti wakawa wanachonga penseli zao ziandike vizuri.
Kuna watendaji ndani ya wizara waliona kama vile sasa bwawa limeingia luba itakuwa tabu kuogelea kwa raha na salama.
Yaliyotokea sasa ni historia.
Prof. Malima aliondolewa kwenye Wizara ya Elimu baada ya kujadiliwa Dodoma.
Hayo ndiyo yaliyofanya mimi hii leo nimkumbuke kaka yangu Kenya Hassan.
Mola amghufirie dhambi zake na amlipe Pepo ya Firdaus.
Amin.
View attachment 1735030
Bila...Wanaokuheshimu kwa udini unaoeneza wa shida vichwani mwao.
Kichuguu,
Muhimu ni yale ambayo Prof. Malima aligundua yanafanyika ndani ya Wizara ya Elimu na akaandika taarifa kwenda kwa Rais.
Rais alishtuka na akajua kuwa anakabiliwa na tatizo kubwa hajapata kukutananalo.
Taarifa hii ya Prof. Malima iliibiwa na kuvujishwa kwenye magazeti.
Taarifa hii ilikuwa kwenye agenda ya kikao cha Dodoma ambacho Nyerere alihudhuria.
Kwa unyeti wa agenda hii ilionekana bora isijadiliwe.
Ndugu yangu wewe unanufaika na mfumo huu ulioko na hili linakufanya ukatae kutaka kuujua kweli.
Je, ulikuwa unayajua haya?
Aliyeiba taarifa ile ya Prof. Malima kwa Rais alifahamika na hakufanywa lolote zaidi alipongezwa.
Nakuwekea hapo chini picha ya Rais Ali Hassan Mwinyi na watendaji wake.
Prof. Malima ni huyo mstari wa mbele wa kwanza kushoto.
View attachment 1738342
Kwani hata wwangekuwa wwaislaamu shida nn?Ujoka,
Katika Wakurugenzi watano Wizara ya Elimu wote watano walikuwa Wakristo.
Una fikra gani katika mgawanyo huu?
Inside 10,Kuna vitu nilivyokwisha andika kuhusu profesa malima kudanganya watu kuwa yeye ndiye alieanzisha utaratibu wa wanafunzi kutumia namba kwenye mitihani ili waislamu wasionewe na wao wakakubali. Wote waliokubali kuwa Malima ndiye aliyeanzisha utaratibu ule itakuwa ni wale ambao hawakuwahi kufanya mitihani hiyo kwani matumizi ya namba kwenye mitihani yaliachwa na mkoloni, na wala utaratibu huo haukuwahi kubadilishwa. Malima akatia uwongo kuwa watoto wenye majina ya kiislamu walikuwa wanafelishwa, na hiyo ikampa wafuasi ambao walikuwa hawajui mitihani ile ilikuwa inatungwa na kusahihishwaje.
Usahihisjai wa matokeo ya darasa la saba ulikuwa unafanywa na waalimu wa misingi huo huko mikoani ambapo kila swali lilikuwa lisahahishiwa na grupu la waalimu wachache tu; na grupu hilo lilikuwa halijui swali jingine mwanafunzi huyo kafanya nini. Mitihani ya darasa la 12 ilikuwa inasahahihishwa na kundi la waalimu wa shule za sekondari kwa utaratibu kama huo huo wa darasa la saba. Mitihani mingi ya darasa la 14 ilikuwa isahahihishwa na waalimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam. Sasa maofisa wa wizara wangeingiliaje matokeo ya usahihishaji wa mitihani hiyo na kuwafelisha watoto wa kiislamu tu?
Hata hivyo, yeye akiwa pale Wizarani, je alibadilisha nini? Je alipofukzwa Wizara ya fedha ilikuwa pia ni kwa sababu ya Nyerere kumchukia kwa vile ni mwislamu?
Malima hata historia yake ya kwenda kusoma marekani ninaijua na niliwahi kuiweka hapa; safari yake ya kwanza ilikuwa ni kuombewa na Nyerere kutoka kwenye conncetions alizokuwa nazo wakati huo. Malima asingekuwa hapo alipofikia bila Nyerere kumpeleka Marekani kwa mara ya kwanza wakati akiwa Katibu wa TANU Rufiji. Babu alimfukuza Malima pale wizara ya Mipango kwa vile alisema alikuwa incompetent, ndipo Nyerere aakampeleka UDSM kama profesa. Alipoanza juhudi za kurudi kwenye siasa, ni Nyerere aliyempigia debe sana mwaka 1981, na baadaye kumfanya kuwa waziri wa mipango - akaleta SAP ambayo haikusaidia kujenga uchumi bali blah blah tu.
Kwa vile malima alikuwa incompetent kweli kama alivyosema Babu, hakuna la maana alilofanya kwenye kila position aliyopewa hadi ikafikia hata mwisho Mwinyi naye akamfukuza wizara ya fedha. Chuo kikuu pale alipotoa professorial inaugural lecture yake ya "Political Economy of Devaluation in Developing Countries" wataalamu wote wa uchumi walijiuliza huyu ni profesa gani.
Kutokana na Malima kufilisika kimawazo, ndiyo akaona akakimbilia siasa za dini, na njia pekee ya kuwapata wafuasi wenye mlengo wa dini ni kumshambulia nyerere. Kwa waislamu wa aina hiyo ukishamshambulia Nyerere kuwa alikuwa anapiga vita uislamu, unawapata wengi sana, na ndiyo siasa za watu wa namna hiyo.
Prof. Malima kuwa mtu asiyejiweza yaani "incompetent," kisha awe alma mater wa Princeton University ambayo ni Ivy Leaguebni vitu visivyoingia akilini na ukweli huu ni mbali kuwa akiwa mwanafunzi Mzumbe alikuwa akiongoza katika hesabu.
Kisha huyu mtu asiyejiweza akawa mhadhiri Idara ya Uchumi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Historia za namna hii hazitakupa raha maisha yako yote! Kuna historia nzr na za kurithi siyo hizi!! Kila jema!Kichuguu,
Tuko pale pale nimesema ufunguliwe uzi wa Prof. Malima maudhui ya uzi huu uko wazi.
Nimetabasamu kidogo ulipomtaja Prof. Issa Shivji kuwa naweza kupata yakini kutoka kwake.
Prof. Issa Shivji tunafahamiana vyema.
Wakati yeye, Prof. Saida Othman na Dr. Ng'wazi Kamata wanaandika kitabu cha Julius Nyerere Prof. Shivji alinihoji hasa kuhusu Nyerere na uhusiano wake na wazee wangu.
Nilimweleza kila kitu na nikatoa nyaraka na picha.
Kwa ufupi niliwapa hazina yote kuhusu Nyerere niliyokuwanayo Maktaba.
Hapa mimi nasimama.
Kasome kitabu cha Nyerere na angalia Prof. Issa Shivji kaandika nini kuhusu mimi.
Kwa kuwa tuko katika suala la elimu nitakueleza nini Prof. Shivji kaandika kuhusu Waislam.
Nyerere aliivunja EAMWS mwaka wa 1968 na kuunda BAKWATA wakati EAMWS inajenga Chuo Kikuu Cha Waislam na yeye ndiye aliyeweka jiwe la msingi.
Prof. Shivji ameandika kuwa EAMWS ilikuwa inajenga Islamic Centre sio Chuo Kikuu.
Nilisikitika sana.
Prof. Shivji kaandika hivi ili isionekane kuwa Nyerere ana mkono katika kurudisha nyuma maendeleo ya Waislam katika elimu.
Naamini umenielewa.
Haya ndiyo matatizo tuliyonayo.
View attachment 1739219
Saimile,Historia za namna hii hazitakupa raha maisha yako yote! Kuna historia nzr na za kurithi siyo hizi!! Kila jema!