Msamehe bure,uzee umemfanya asahau mengi
KAULIZA MWENYE KUULIZA ITAKUWAJE HISTORIA MPYA INAYOANDALIWA IKIFANANA NA HII HISTORIA YA SASA?
Historia ya Tanganyika na kwa makusudi nataka nianze na hii kwa kuwa mimeitafiti na kuandika kitabu ambacho naamini sote tunakifahamu.
Umuhimu wa historia hii unasimama kwenye historia ya kudai uhuru chini ya TANU.
Chuo Cha CCM Kivukoni kilichapa kitabu cha historia ya TANU mwaka wa 1981.
Kitabu hiki kilichapwa baada ya Abubakar Ulotu kuandika historia ya TANU kutoka mswada ulioanza kuandikwa na Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu labda mwaka wa 1962.
Uandishi wa kitabu hiki uliingia katika matatizo na Abdul Sykes akajitoa kazi ikakamilishwa na Dr. Kleruu peke yake.
Tatizo katika utafiti huu lilikuwa kwanza nafasi ya baba yake Abdul, Mzee Kleist Sykes katika uasisi wa African Association mwaka wa 1929.
Tatizo jingine likawa nafasi ya Abdul Sykes katika TAA baada ya kifo cha baba yake mwaka wa 1949.
Halafu pakawa na tatizo la Julius Nyerere.
Nini mchango wake katika kuunda TANU?
Abdul alipojitoa katika uandishi wa historia hii ikawa kwa uamuzi ule umetoa fursa kwa waliobakia kuandika historia waliyoitaka wao.
Abdul Sykes akafutwa kwenye historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Mswada huu haukuchapwa na ukawa Maktaba ya TANU Mtaa wa Lumumba na hivi ndivyo ulivyoangukia mikononi kwa Abubakar Ulotu na yeye akachapa kitabu kwa jina lake.
Historia iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni haina tofauti na ile "aliyoandika," Abubakar Ulotu.
Miaka ikapita.
Mwaka wa 1998 mimi nikachapa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kitabu kilichoeleza historia ya TANU na harakati za kudai uhuru.
Kitabu hiki kilipindua historia ya TANU juu chini.
Kitabu kilimleta Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kama chanzo cha kuundwa kwa TANU na harakati za uhuru.
Kadhalika kitabu katika hili kitabu kikamleta Chief David Kidaha Makwaia katika juhudi za kutafuta kiongozi wa kuongoza harakati za kudai uhuru.
Kuna watu hawakuridhika na kitabu hiki hasa kwa kuwa kilionyesha mchango mkubwa wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Watu hawa wakataka kiandikwe kitabu kuonyesha mchango wa Julius Nyerere katika kuunda TANU.
Kitabu hiki kipo sokoni hivi sasa.
Swali la kujiuliza ni hili.
Je kuna mapya ndani ya kitabu hiki ambayo yanabadilisha yaliyomo kwenye historia ya TANU iliyokwisha andikwa?
Tutegemee nini katika historia hii mpya inayotayarishwa hivi sasa?
Gide...
Katika makala hiyo hapo juu umeona dalili la mtu aliyepotemza utambuzi?
Hii makala iko hapa JF nimeiweka muda mfupi uliopita.