Hii vita ya
Kenya dhini ya
Al- Shabab ni kama vile mpango maalum wa kuwafanya wananchi wa Kenya kuacha kuwaza juu ya masuala ya
Ocampo dhini ya viongozi wa juu wa Kenya waliosababisha
maafa baada ya uchaguzi huku wananchi wengi wakiwa wakimbizi wa ndani (IDP).
Vyombo vya usalama vinaweza kuanzisha
mkakati mkubwa wa kuwanasua viongozi wenye kashfa mbaya mfano mauaji ya halaiki kwa kutafuta 'kitu' cha kuwaunganisha wa-Kenya wasahau madhila yaliyowakumba baada ya uchaguzi na pia
serikali ya Kenya kutafuta huruma toka kwa mataifa makubwa yapunguze mbinyo dhini wa wanaotuhumiwa na
Ocampo kwa vile wanashiriki ktk
vita dhini ya ugaidi.
Kuna movie (sinema) moja iitwayo
'Wag The Dog' ambapo De Niro anakuwa
'spin-doctor' wa serikali
kumwokoa Rais dhini ya kashfa ya ngono kwa kuzua uongo kuwa USA inakabiliwa na ghaidi wa
'suite case bomb' toka ka-nchi cha
Albania Wag the Dog - Wikipedia, the free encyclopedia.
Ukiangalia hiyo sinema ya Wag The Dog na
mlolongo matukio ya watalii kutekwa, mara gari kulipuliwa na polisi jijini Nairobi mara baa yenye watu 12 kutupiwa gurunedi au kuivamia Somalia kumfukuza gaidi asiyeonekana Al Shabab yote inapelekea kuuliza maswali mengi juu ya maamuzi ya viongozi wa kisiasa wa Kenya. Na utaona mawaziri wa Kenya wanatoa ufafanuzi-tata mara tulikuwa Mogadisho tukakubaliana na serikali ya mpito ya Somalia juu ya vita hii na baada ya siku chache
Raisi wa Somalia analaani uvamizi wa Kenya n.k
Katika mjadala wa Bunge la Kenya kuhusu mantiki ya Kenya kuivamia Somalia, tulisikia
Naibu Waziri wa ulinzi wa Kenya akidai kuwa
Kichwa cha Al Shabab kipo ktk kitongoji cha Eastleigh jijini Nairobi na mkia upo huko porini Somalia. Huu msemo unafanana sana na 'Spin Doctor" ktk sinema ya Wag The Dog.
Sasa ukiukata mkia wa zimwi uliopo Somalia ndiyo ufumbuzi? au ukitaka kuliua zimwi basi kata kichwa kilichopo ktk kitongoji cha Eastleigh ndani ya jiji la Nairobi, ndiyo ufumbuzi wa vita dhini ya pirate wa baharini na majambazi wa utekaji watalii Kenya kwa kutumia jeshi la polisi na maajenti wa Usalama wa Taifa (National intellingency).
Tanzania na wa-Tanzania tusikubali kuingizwa mkenge 'kuwasaidia' jirani yetu kwa vile tupo ktk EAC (Jumuia ya Afrika Mashariki) ktk vita hii yenye maswali mengi juu ya dhamira halisi ya vita hii.
Ugaidi humalizwa kwa vita ya kimya-kimya yaani kutumia Usalama wa Taifa (intellingene agencies) na siyo makelele mengi ya kupeleka askari wa anga, miguu na navy nchi jirani kupigana na adui asiyeonekana, sana sana utaishia kuuwa raia wasio na hatia na hatimaye vita itakuwa ngumu kuishinda.
N.B
Msemo wa 'Wag the dog' kwa kiingereza maana yake ni nini:
Idiom Definitions for 'Wag the dog'
To 'wag the dog' means to purposely divert attention from what would otherwise be of greater importance, to something else of lesser significance. By doing so, the lesser-significant event is catapulted into the limelight, drowning proper attention to what was originally the more important issue.
The expression comes from the saying that 'a dog is smarter than its tail', but if the tail were smarter, then the tail would 'wag the dog'. The expression 'wag the dog' was elaborately used as theme of the movie. 'Wag the Dog', a 1997 film starring Robert de Niro and Dustin Hoffman, produced and directed by Barry Levinson.
Source:
http://www.usingenglish.com/reference/idioms/wag+the+dog.html