Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Upande wa Wabunge ODM wana viti vingapi mpaka sasa?

BBC wanadai ODM ina viti 53 mpaka sasa, lakini Nation Media wanaonyesha 24.

Pamoja na hayo BBC Radio wanasema kwamba Raila na Nyagah wamewa-acuse Tume ya Uchaguzi kwamba kuna njama wanataka kufanya ili kuiba kura baada ya kuona matokeo ya awali yakionyesha wazi kwamba Kibaki na watu wake wa karibu wamegalagazwa. Wanauliza kwanini matokeo yakifika Nairobi hayatangazwi na badala yake wanayakalia? Wanataka kuyafanyia nini? Kuna dalili za kufanya mpango mbaya. Naona wote wamekutana ni wajanja!
 
Upande wa Wabunge ODM wana viti vingapi mpaka sasa?

Ngoja tuulize maana prof kazidiwa na furaha.Natafuta watu wa chini kidogo pale orange house.

Confirmed Ngilu kashinda. She gona be the only NARC mp katika Bunge la 10 la Kenya.

Unajua kuna mgombea kashinda kwa kufanya kampeni siku mbili tena eneo la PNU. Jamaa alikuwa kafungwa during all time ya kampeni, tena criminal charges. Siasa za Kenya Tamu sana. Watu wakiamua wameamua
 
This is interesting! Kweli Wakenya WAMEAMUA!
hadi REDYKULASS, the "Comedy" wa Kenya naye Mbunge???
 
Vigogo watimuliwa katika kura za Kenya

Imeandikwa na Hassan Mhelela, BBC London.

Makamu wa Rais Moody Awori amepoteza kiti chake cha Funyula, magharibi mwa Kenya, baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1983 na Dr Paul Otuoma.

Bwana Awori alikuwa miongoni mwa mawaziri kadhaa katika serikali ya Rais Mwai Kibaki ambao tayari wamepigwa teke na wapigaji kura.

Wengine ni mawaziri Mutahi Kagwe wa habari, Paul Sang wa Afya, Musikari Kombo wa serikali za mitaa, na Moses Akaranga wa Huduma za Umma.

Hadi sasa chama cha ODM kimejitosa mbele katika idadi ya viti vya ubunge, kikiwa kimenyakua jumla ya wabunge 53.

Chama cha Rais Kibaki cha PNU hadi sasa kimepata viti 15, huku cha ODM Kenya, kinachoongozwa na Kalonzo Musyoka, kikiwa na viti 2.

Baadhi ya wanasiasa waliopata ushindi mkubwa ni aliyekuwa Makamu wa Rais bwana Musalia Mudavadi wa ODM.

Wengine wanaosherehekea ushindi wao ni James Orengo wa eneo la Ugenya na Dalmas Otieno kutoka Rongo.

Lakini wapigaji kura waliwakataa vigogo wengine kama vile Nicholas Biwott na Waziri Simeon Nyachae.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi haijaidhinisha matokeo haya ambayo yanawakilisha asilimia 10 tu ya kura ambazo zimeshahesabiwa.

Katika hesabu za kura ya urais, vuta ni kuvute kati ya Rais Kibaki na mpinzani wake mkali, Bw Odinga ni ya kusisimua.

Wote wawili wamepigiwa kura kwa kiasi kikubwa. Mpinzani mwingine, Kalonzo Musyoka, anaendelea kushikilia nafasi ya tatu, huku matokeo yakionyesha kwamba huenda asizue miujiza kama vile alivyokuwa akiahidi katika kampeni zake.

Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya wametoa wito kwamba muda wa kupiga kura uongezwe kuwezesha wapiga kura wote wapate fursa ya kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.

Source: BBC
 
Ngoja tuulize maana prof kazidiwa na furaha.Natafuta watu wa chini kidogo pale orange house.

Confirmed Ngilu kashinda. She gona be the only NARC mp katika Bunge la 10 la Kenya.

Unajua kuna mgombea kashinda kwa kufanya kampeni siku mbili tena eneo la PNU. Jamaa alikuwa kafungwa during all time ya kampeni, tena criminal charges. Siasa za Kenya Tamu sana. Watu wakiamua wameamua

Zitto,
Nilisoma sehemu habari za huyu jamaa, kwamba wananchi walienda kumchukulia forms na kumlipia pesa za forms.

Wananchi ndio wanajua wanamtaka nani, haya mambo ya kuzuia watu kugombea, mimi naona sio mazuri labda kama ni mwuza unga au makosa makubwa, vinginevyo waachie wananchi waamue.

Ngilu inaelekea ni bingwa wa siasa za Kenya, alifanya gamble kubwa na naona imelipa.
 
1. Hata mimi napenda sana Kibaki ashinde! Hata ikitokea Raila akishinda nitasononeka tu- sema nitamtakia tu kila la heri koungoza Kenya- I happened to be admirer of Kibaki!

2. Whoever wins- it is ok muhimu Kenya tu isonge mbele!
 
Safi sana biwott kushindwa, huyu tulimnyoshea vidole kuhusu kifo cha ouko, moi family no more politics! vipi uhuru kenyatta? Nampongeza mama Ngullu kwa ushindi wa tsunami. Mafisadi wakubali kuondoka kwa kura yasijewapata ya Bhutto.
 
mie kama kuna kitendo kilichoniudhi, ni kile cha mama kibaki kumpiga kibao mc na cha juzi majibu ya rais kwa bbc yalikuwa manyaufu.


lkn ningependa kibaki ashinde though akishindwa pia kuna la kujifunza.

uchaguzi wa kenya ulivyo n sawa na kule zanzibar.

yaani wagombea hawana raha na hukonda mpaka basi hadi kieleweke
 
Ngilu inaelekea ni bingwa wa siasa za Kenya, alifanya gamble kubwa na naona imelipa.

Alishanusa upepo na aliona uelekeo ulikuwa ni mbaya. Tatizo la PNU ni kama ilimezwa na NARC-K na hivyo alijua angejiingiza kwa Kibaki angekuwa kama akina Saitoti na Mwiraria (ambao naona kudondoka kwao kunawashangaza watu wengi).

Sasa iko wazi kwamba wananchi wa Kenya walishachoshwa na uhuni wa utawala wa Kibaki. Kibaki never acted kwenye lolote katika tuhuma zote zilizoibuka kwenye utawala wake (Anglo Leasing, Arthur Bros na madudu mengineyo). Sasa hukumu ya haki imetolewa na yeye kajionea. Hilo litakuwa fundisho kwa Rais atakayefuata kwamba akiwa na utendaji mbovu kama wa Kibaki, atakaa miaka 5 na baada ya hapo hukumu inapita, NO MATTER WHAT!

Watanzania tunatakiwa kujifunza haya, labda JK atajifunza na kujirekebisha kwenye hii miaka 3 iliyosalia ili aweze kuwa-convince watanzania wamchague tena 2010.
 
mie kama kuna kitendo kilichoniudhi, ni kile cha mama kibaki kumpiga kibao mc na cha juzi majibu ya rais kwa bbc yalikuwa manyaufu.

Hiyo couple nadhani ina matatizo, BBC nao hawakuwa na hiyana waliiweka hewani na jamaa ana-comment kwamba Kibaki ni mzoefu wa kutumia hiyo lugha. Sasa Presida mzima unatoa tusi la namna hiyo na mkeo anapiga MC kofi na alishatwanga mwandishi wa habari kofi, kweli hiyo familia ina sifa ya kuwa first family ndani ya nchi? First family ni kioo cha jamii, sasa ukisikia Rais anaongea lugha ya kihuni na matusi lazima utakata tamaa na inasikitisha sana!
 
uchaguzi wa kenya ulivyo n sawa na kule zanzibar.

yaani wagombea hawana raha na hukonda mpaka basi hadi kieleweke

Tofauti moja kubwa ni kwamba Zanzibar mna mamluki wa kukodi toka Bara ili kuongeza kura za CCM wakati kule Kenya tume yao ni huru zaidi ya hii ya kwetu.

CCM wangeacha kuiba kura Zanzibar, wangesha shindwa tokea mwaka 1995.
 
Nationmedia wamechemsha tena, au ndio wameanza kunywa wine mapema?

Naona graphs zao zimechemsha kweli kweli.
 
Tofauti moja kubwa ni kwamba Zanzibar mna mamluki wa kukodi toka Bara ili kuongeza kura za CCM wakati kule Kenya tume yao ni huru zaidi ya hii ya kwetu.

Hayo ndiyo mengineyo aliyoyasema Mtu wa Pwani, maana sometimes inakuwa ngumu ku-tally kura na idadi ya wapiga kura walio kwenye daftari na ndiyo maana matokeo huwa yanachelewa kutangazwa au wanasubiri usiku wa manane ndipo wanafanya matambiko ili kutoa miujiza ya ushindi!
 
1. Hata mimi napenda sana Kibaki ashinde! Hata ikitokea Raila akishinda nitasononeka tu- sema nitamtakia tu kila la heri koungoza Kenya- I happened to be admirer of Kibaki!

2. Whoever wins- it is ok muhimu Kenya tu isonge mbele!

Watu wa CCM wanachekesha sana. Wajue huu ni upepo wa mabadiliko Afrika nzima.. Wasubiri hakuna kurudi nyuma wanaoamua ni wananchi si wanasiasa, kwa hiyo hata waki-deal na wanasiasa wajue wananchi wakiamua hakuna cha kushindikana. Nilicheka sana m-CCM mmoja mnene aliponambia kwamba Kalonzo atashinda.. sasa sijui atasemaje
 
Waheshimiwa,

Kazi kweli. Huku tunaanza kushikwa na gadhabu kwanini ECK wanachelewa kutoa hesabu rasmi ilhali waafisa watume hii mashinani wameshakabidhi vyombo vya habari matokeo na wakenya kufahamishwa? Sasa mbona wasikubali tu kwamba aisyekubali kushindwa si mshindani? Si hata huyu mzee Moi alishindwa na akaenda retire?

elec2712074.jpg


Haya tuwachane na hasira tuendelee na dondooz


1. Mawaziri wengine wawili na msaadizi waziri mmoja wa Kibaki wameonyeshwa kadi nyekundu na ODM kunyakua kura zote sehemu hizi.

a)Mohamed Abdi Mohamed - Livestock
b)Moris Dzoro - Utalii
c) Suleiman Shakombo - Uhifadhi wa Utamaduni


Wengine watatu ambao wako kwenye kuvuta mkia lakini bado kura hazijamalizika kuhesabika ni:

a) Joseph Munyao - Livestock and Fisheries
b) Kivutha Kibwana - Lands
c) Mutua Katuku - Ntachunguza ministry yake

na Chirau Ali Makwere - Transport


HAYA KTN 2.45PM

MWAI KIBAKI / RAILA ODINGA / KALONZ0 MUSYOKA

Nairobi 84,283 / 103,847 /14,965
Eastern 57,448 / 11,687 / 144,485
Nyanza 20,866 / 865,564 /691
Coast 53,378 / 80,295 / 5,614
Central 803,028 / 8,959 /2,126
North Eastern 20,501 / 25,391 / 4,235
Western 81,963 /271,911 /2,530
Rift Valley 288,918 / 757,901 / 19,772

Total 1,410,385 /2,125,555 /194,418





MAONI YANGU: NATION MSIIAMINI SANA. WAMEKUWA MSTARI YA MBELE KUIPIGIA SERIKALI YA KIBAKI DEBE KWENYE KAMPENI. FUATENI HIZO GRAFU LAKINI MFANYE CROSS-CHEKING NA INFOMESHEN TOKA PANDE ZINGINE.

[/B][/COLOR]
 
Sasa hizi graphs za Nation zinazoonyesha "negative" maanake ndio nini?
 
Sasa naona wanaonyesha cutoff za majimbo kwa kura zilizokwisha hesabiwa
 
Nilicheka sana m-CCM mmoja mnene aliponambia kwamba Kalonzo atashinda.. sasa sijui atasemaje


Huyo naye, yaani yupo usingizini kiasi hicho! Hawa watu wa CCM nani aliwaloga hadi wakawa wajinga kiasi hiki?
 
Ndg Zangu

Nawasliana na mtu from Orange ni repoter wetu ila from what i can see ODM watapata viti vingi vya ubunge my worrie ni kura za urais bcs margin ya ubunge ni tofauti na margin za urais this means wapiga kura wanachagua ODM ubunge but not wote wamechagua Rais.

Inanipa mashaka kidogo na as the day walikuja TZ Prof;Anyang'nyong na Joe niliona wasiwasi flani ambao walionyesha juu ya voters na mbinu sasa hivi GOOD WISHERs wote wa ODINGA tunafurahia anavo ongoza lakini its only btn 10 to 15% ya kura jamaa asije akawa anatutanguliza na baiskeli ya mbao wakatupiga bao.
 
Zitto na wanasiasa wenzangu wa Tanzania mnajifunza nini na matokeo ya uchaguzi huu wa kenya?
kwa nini wanasiasa wa bongo hasa vyama vingi wanaanza maandalizi ya uchaguzi mwaka uleule wa uchaguzi?? kama sio kununuliwa haya ya kenya yangekuwa yameshatokea kwetu kitambo sana. Mabadiliko ni muhimu ilimurdi dira ya ustawi wa taifa iwe mbele.

Ninaombea ODM wakamate usukani Kenya kwa kuwa msimamo wao ulishaanza kuonekana tangu walipokataa mabadiliko hasi ya katiba yaliyokuwa kinyume na makubaliano....
 
Back
Top Bottom