Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Wakati Kibaki anashinda uchaguzi wa 2002, Moi alichanganyikiwa kiasi kwamba hata handing over ya urais ilikuwa kama ya kulazimishana. Kama Raila kashinda basi tutegemee maajabu makubwa zaidi. Kitendo cha Kibaki kutoa tusi huku akijua kwamba anahojiwa na mwandishi wa habari wa BBC ni dalili tosha ya kuonyesha kwamba mambo yanaweza kuwa magumu sana kwenye shughuli ya kukabidhiana madaraka. (Huu ni mtazamo wangu iwapo Raila kashinda kweli)
 
hi wana jf.
kuna habari zisizopendeza, huko Mji wa Migori ni risasi tu mji mzima. nyumba za wakikuyu zinachomwa moto, magari ya wakurya nayo yanachomwa moto, watu wanauna coz wana KIbaki anaendelea kuiba kura. Eeee Mungu wasaidie wakenya bongo tumechoka kubeba wakimbizi!!!!

Kasungura unaweza kushangaa kuwa wakenya watakaokuja si wakimbizi bali watakuja nyumbani, kama Kenyan Tanzania akija atakuwa amekuja kwao, au wajaluo wakienda kwa kina Marando na Sarungi ni kwao, au wamasai wa kenya ambao wengine karibu ukoo wao mzima uko upande wa Tanzania hao huwezi kuita wakimbizi, wakenya kwa ujumla wakija Tanzania hawawezi kuwa kwenye category ya wakimbizi, labda tunaweza kusema ndugu zetu leo wamekuja kwa wingi
 
Acha unafiki wako hapa kwani kitu gani kibaya kimesemwa hapo.

Nashukuru kwa kusema mimi mnafiki, lakini unajua wazi mwenye uwezo wa kusema nani kashinda ni ECK, ndio maana hata ODM walivyoongea na Mh Zitto(MB) ni kwamba pamoja na kuona wameshinda wanasubiri ECK,,, hawakosema wanawaambia watu wao tumeshinda,,, ukitulia kidogo utaelewa,,, ukikurupuka ndio hivyo tena

Raila Odinga kesha twaa mikoba yote. Kenyans have decided.

Sina Tatizo na hili mkuu,,, mimi niko upande huo huo...
 
Mh. Zitto(MB),

Heshima mbele, Tahadhari tu mheshimiwa!!! hili si jambo rahisi!!! JF nayo ni chombo kinaangaliwa duniani kote including Kenya,,, kwa hiyo kama ODM wanavyosubiri official results from ECK, na wewe ungevumilia kidogo kufanya hivyo... hili ni jambo tete!!! Kumbuka Zanzibar (Shariff na Komandoo) na DTV

Matokeo yake si ndiyo huyu Seif akanyang'anywa ushindi, siku hizi hamna usiri mzee habari zinatoka kila kona, hata Zitto asingeweka hapa watu watazipata tu.
 
kwanini wapinzani Tanzania wasiangalie mfano wa Kenya, ndio ni muhimu sana kukosoa mikataba ya madini na makosa mengine mengi, lakini cha msingi kuepo na Tume huru ya uchaguzi.

Upinzani mngepigania hili sana maana hii ndio platform ya ushindi. angalieni kwa makini ni njia gani kura huwa zinaweza kuibiwa na kabla ya chaguzi kufika muzibe hiyo mianya. hamuezi kushughulika na sera wakati hakuna usalama wa kura.

Campaign for changes in the Tanzania electral commission setup hii ndio dawa ndugu zangu. the only way Tanzanians can speak out is through our votes. kama nyie wapinzani hamlipi kipaumbele then our voices will be unheard.

Mngeanza Kampeni sasa, ya nguvu tena. maana it is the only solution. sometimes you might think that Tanzanians huwaja amua kumbe ukawa umekosea tu.

Watanzania wanajua wanachotaka ni sauti tu hazija sikika.
 
From an Independant observer...

Msigeuze hii kuwa saisa za TZ... Kula Focus! ODM OYEEE!
Mhenwa tusubiri matokeo..Hoja zipo! ODM Oyeee!
 
Jamani mwenyekiti wa tume amechimba mkwara kwa wale wanaochelewesha matokeo...
 
_44325292_soldiers_afp203b.jpg

Isolated incidents of violence
continued after the vote

RESULTS1.jpg

Source: http://www.raila07.com/results2.cfm
 
Kasungura unaweza kushangaa kuwa wakenya watakaokuja si wakimbizi bali watakuja nyumbani, kama Kenyan Tanzania akija atakuwa amekuja kwao, au wajaluo wakienda kwa kina Marando na Sarungi ni kwao, au wamasai wa kenya ambao wengine karibu ukoo wao mzima uko upande wa Tanzania hao huwezi kuita wakimbizi, wakenya kwa ujumla wakija Tanzania hawawezi kuwa kwenye category ya wakimbizi, labda tunaweza kusema ndugu zetu leo wamekuja kwa wingi

BONGOLANDER NAKUBALIANA NA WEWE KABISA, MAANA PIA KUNA AKINA SISI TULIOZALIWA KWASABABU WAZAZI WETU WALIKUWA EAST AFRICAN COMMUNITY KOTE KOTE TUPO.
 
Naona mwenyekiti wa tume anamsema Kibaki indirect....anasema He can understand why people can't accept defeat
 
...hahahaaaaa, kila baada ya sekunde chache watu wanarefresh page. Jamani hamna kazi nyingine, au kihoro?
 
Naona mwenyekiti wa tume anamsema Kibaki indirect....anasema He can understand why people can't accept defeat

Hivi Mwenyekiti wa Tume, hana mamlaka ya akiona vituo vichache vina mizengwe(kura za kupigwa au kuchelewesha kwa makusudi) azi-ignore kura hizo na vituo hivuo,,, kwa kusema uchelewesha wa kura unaliweka taifa mahali pabaya hivyo anatangaza mshindi mapema na mchezo unaisha?

Naota tu!
 
Mnasubiri hadi CNN au BBC? Mh. Zito ameitoa hapa LIVE kwanza toka jikoni wengine wanafuata. KUDOS JF.
 
Odinga's Orange Democratic Movement party said the government is deliberately delaying results.

We'd like the ECK (Electoral Commission of Kenya) to announce the results in order to ensure that the political temperature does not go up"

Source:AP
 
Kasungura unaweza kushangaa kuwa wakenya watakaokuja si wakimbizi bali watakuja nyumbani, kama Kenyan Tanzania akija atakuwa amekuja kwao, au wajaluo wakienda kwa kina Marando na Sarungi ni kwao, au wamasai wa kenya ambao wengine karibu ukoo wao mzima uko upande wa Tanzania hao huwezi kuita wakimbizi, wakenya kwa ujumla wakija Tanzania hawawezi kuwa kwenye category ya wakimbizi, labda tunaweza kusema ndugu zetu leo wamekuja kwa wingi

Wee😡 sasa naona we unafaa kwenda kigoma.😀 Nini hii? Ukabila? enda mbali
 
Wee😡 sasa naona we unafaa kwenda kigoma.😀 Nini hii? Ukabila? enda mbali

Mzee Sounds like ukabila lakini ni ukweli wa mambo huo. Kuna wamasai wengi kutoka Kenya wanavuka kuingia Tanzania na wengine wanavuka kwenda Kenya bila passport wanaulizwa Jambo ndugu. Lakini Mkikuyu,mkamba au mchaga,mpare anaulizwa onesha passport yako. Inachekesha sana, it looks like people have tacitly agreed on this at our border crossings!
 
Back
Top Bottom