Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilitegemea kunywa bia yangu naona nitakunywa soda tu kwa leo
UCHAGUZI UMEKWISHA NA KIBAKI NDIO MBABE KWA MARA YA PILI SASA WAKENYA TUJENGE NCHI YETU YA WAKENYA
KUNA HII NYIMBO http://www.youtube.com/watch?v=67GoueWZXG8 KARIBUNI KENYA BY SAFARI SOUND
NAFIKIRI UTAIFUTAHIA
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!
2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!
3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!
Imeandikwa na Hassan Mhelela said:
Tume ya uchaguzi ya Kenya imemtangaza Mwai Kibaki kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 27 Disemba.Raila Odinga ameshika nafasi ya pili.Mwai Kibaki wa chama cha PNU ameshinda jumla ya kura 4,584, 721 akifuatiwa na Raila Odinga wa Orange Democratic Movement aliyepata kura 4,352,993 na Kalonzo Musyoka wa ODM-Kenya ambaye amepata kura 879, 903.
Tangazo hilo lilitolewa baada ya mgombea wa ODM, Raila Odinga kumshutumu Kibaki kwa kufanya hila ya kuvuruga matokeo ambapo alitoa wito kutaka tathmini ifanyike kupitia upya matokeo yote.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Samuel Kivuitu, akionekana kupitia televisheni taifa - KBC TV, alisoma moja kwa moja hewani baada ya vyombo vingine vya habari kutimuliwa kutoka makao makuu ya tume ya uchaguzi.
Alisema kwamba Kibaki amembwaga Raila Odinga kwa kura tofauti ya 231,728 votes. "Hii ina maana kwamba mheshimiwa Mwai Kibaki ndiye mshindi," Bw Kivuitu alieleza. Bw Odinga alikuwa akiongoza tangu shughuli ya kuhesabu kura ilipoanza, lakini idadi ya kura zake ikianza kumezwa pole pole na zile za mpinzani wake.
Shughuli ya kuhesabu kura ilicheleweshwa, na kuchochea ghasia katika maeneo mbali mbali ambapo watu kadhaa wameuawa.
Mkuu kilitime, hii haiwezi kutulizwa kwa bia ya Tusker, hapa inabidi kutafuta chang'aa ile namba wani. Yaani ghafla nimejisikia kama nimesimamia shingo...!!!Mwambie mh. Zitto(MB) Kama anapata Kinywaji apige Tusker Mbili baridi,,, maana nadhani mishipa imekaza sana sasa hivi!!!
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!
2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!
3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!
Ole,
Vipi sasa kuhusu ushauri wangu wa kufanya compilation ya posts zilizoko kwenye hii thread, halafu JF itoe kitabu cha yaliyojiri kwenye Kenya elections 2007?
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!
2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!
3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!
Naomba kuwakumbusha kitu kimoja chaguzi nyingi za Kiafrika and probably nyingi au zote zilikuwa hivi hivi,,, tofauti ilikuwa huko nyuma hapakuwa na maendeleo ya ICT ambayo yalisaidia kupekua pekua kama chokora mambo ya Kura zimeibiwa mara zimeongezwa... wakati wa nyuma ulikuwa unaongeza kura unazotaka kama unamsukuma mlevi vile!!!
Kwa hiyo hapa ni technologia tu ndio imewasaidia kuwaambia mambo yalikuwa hivi siku zote kwenye chaguzi zetu za Kiafrika...
Mungu Ibariki Kenya, Mungu Ibariki Tanzania,,, Mungu Ibariki Afrika..
Raila waiting for plan B... kibaya sasa hivi watasema wewe ndio mkorofi,,, itategemea wajomba zetu wa USA, EU nk. wataegemea upande gani?
Hivi ushauri tunautoa kwa nani? na ninani atafanya hiyo compilation? Alafu itatolewa/kuchapishwa wapi? Otherwise mimi ninaona kuna mambo mengi mazuri kwenye hii thread ..ingwafaa watu wengi wasiopitia mitaa hii ya JF!