Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Aibu sana kwa watawala wetu... Kwa nini mtu ung'ang'anie kuwaongoza watu wasiokutaka. Selfish shameless old man!!!!
 
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!

2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!

3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!
 
Ole,

Vipi sasa kuhusu ushauri wangu wa kufanya compilation ya posts zilizoko kwenye hii thread, halafu JF itoe kitabu cha yaliyojiri kwenye Kenya elections 2007?
 
Naomba kuwakumbusha kitu kimoja chaguzi nyingi za Kiafrika and probably nyingi au zote zilikuwa hivi hivi,,, tofauti ilikuwa huko nyuma hapakuwa na maendeleo ya ICT ambayo yalisaidia kupekua pekua kama chokora mambo ya Kura zimeibiwa mara zimeongezwa... wakati wa nyuma ulikuwa unaongeza kura unazotaka kama unamsukuma mlevi vile!!!

Kwa hiyo hapa ni technologia tu ndio imewasaidia kuwaambia mambo yalikuwa hivi siku zote kwenye chaguzi zetu za Kiafrika...

Mungu Ibariki Kenya, Mungu Ibariki Tanzania,,, Mungu Ibariki Afrika..

Raila waiting for plan B... kibaya sasa hivi watasema wewe ndio mkorofi,,, itategemea wajomba zetu wa USA, EU nk. wataegemea upande gani?
 
next nchi haitawaliki hilo ndio suluhisho.

mtu akijitia wehu kumwaga mboga wewe ilobaki ni kumwaga mlo nyote mkae na njaa.

si kila wakati amani inakuja kwa njia ya amani.

sisi zanzibar huwa tunamsemo unasema ukiujua huu na ss tunaujua huu.
 
Now time again to show that even in Africa there can be civilisation and civilised way of solving poltical problems.

Uchaguzi huu ulikuwa closely contested na yeyote kati ya hawa wawili alikuwa anatarajiwa kushinda. Hakuna shaka huyu bwana ameiba kura ili apate ushindi. Pamoja na machungu waliyo nayo ODM wakiongozwa na jemadari wao Raila (kama ambavyo sisi hapo tulivyo), nafikiri ni muhimu sasa wakae haraka baada ya matokeo haya kutangazwa na kuona the right course. The first course should be to try with all their efforts, as they did in luring the support they got, to cool down the people's anger. Kuingia mtaani liwe ni jambo la mwisho. Watumie options za mezani kwanza kwa kuanzia na mahakana, na madamu wana the majority bungeni wajipange huko na wana nafasi ya kufanya vizuri sana katika kurekebisha mfumo uliosababisha waibiwe kura. Inawezekana Raila asipate nafasi tena ya kuwa Rais wa Kenya, lakini ana nafasi kubwa, kupitia wabunge wake huko bungeni, ya kuitengeneza Kenya ikawa the best model of democracy in Africa.

Mhe Zitto, mimi nafikiri kama unaweza ukatumia ushawishi wako kwa hawa ndugu zetu wa ODM wakaweza kuwatuliza wafuasi wao na wao kupanga mashambulizi ya kiakili upya badala kuingiza watu barabarani litakuwa jambo la maana sana.
 
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!

2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!

3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!

propaganda kama anazozitoa yule prof mkikuyu kwenye kbc.

yaani watu waibe kura kisha wanakuambie uende mahakamani ambako jaji mkuu ni rafiki ya mwizi wa karibu.

Huu mfano wa marekani ni mbovu kabisa. Rais wa marekani hana power kwenye domestic issues kama vile rais wa nyumbani so hapa ni mambo mawili tofauti.

kuvumiliana wakati mwenzako hataki kukuvumilia?

goooosh
 
Mwai Kibaki atangazwa rais wa Kenya

Imeandikwa na Hassan Mhelela said:

Tume ya uchaguzi ya Kenya imemtangaza Mwai Kibaki kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 27 Disemba.Raila Odinga ameshika nafasi ya pili.Mwai Kibaki wa chama cha PNU ameshinda jumla ya kura 4,584, 721 akifuatiwa na Raila Odinga wa Orange Democratic Movement aliyepata kura 4,352,993 na Kalonzo Musyoka wa ODM-Kenya ambaye amepata kura 879, 903.

Tangazo hilo lilitolewa baada ya mgombea wa ODM, Raila Odinga kumshutumu Kibaki kwa kufanya hila ya kuvuruga matokeo ambapo alitoa wito kutaka tathmini ifanyike kupitia upya matokeo yote.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Samuel Kivuitu, akionekana kupitia televisheni taifa - KBC TV, alisoma moja kwa moja hewani baada ya vyombo vingine vya habari kutimuliwa kutoka makao makuu ya tume ya uchaguzi.

Alisema kwamba Kibaki amembwaga Raila Odinga kwa kura tofauti ya 231,728 votes. "Hii ina maana kwamba mheshimiwa Mwai Kibaki ndiye mshindi," Bw Kivuitu alieleza. Bw Odinga alikuwa akiongoza tangu shughuli ya kuhesabu kura ilipoanza, lakini idadi ya kura zake ikianza kumezwa pole pole na zile za mpinzani wake.

Shughuli ya kuhesabu kura ilicheleweshwa, na kuchochea ghasia katika maeneo mbali mbali ambapo watu kadhaa wameuawa.

Kama ni matokeo halali kwa nini vyombo vingine vya habari wafukuzwe? Je, ametishiwa maisha yake au familia yake?
 
Mzalendohalisi,
Haki lazima ionekane inatendeka. Just because you were on Kibaki's side it is easier for you kusema tusonge mbele wakati inajulikana bayana kwamba mafisadi wamehujumu haki. As for the US at least the Supreme Court intervened to legitimize Bush. There is no comparison.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 110 (51 members and 59 guests)
Nzokanhyilu, Mtanzania, mfwatiliaji, Rufiji, Azimio Jipya, kilitime, mkamap, ngereja, green29, Jembajemba, Invincible, MAJIMOTO, COMRADE44, Mtu Mzima, nampula, tanzactive, Jasusi, kapinga, Nurujamii, mwafrika, Rwabugiri, Ogah, johnshaaban, sabasaba, Dua, malila, Mtu, NakuliliaTanzania, Mtu wa Pwani, MSAUZI, Mzuzu, Wicked3, Kitila Mkumbo, shemzigwa, Mlalahoi, Kadogoo, Zitto, Masatu, Bwana Mdogo, Keil, Keen, Mtaalam, mkomboziufisadi, Kenyan-Tanzanian, Verily Verily, Halisi, ulate, KULIKONI UGHAIB, LUGASA, mtu66

Kweli, watu wanajali demokrasia. we have a lot to learn from Kenyans. Leo Siasa imehamia Kenya.
 
Mwambie mh. Zitto(MB) Kama anapata Kinywaji apige Tusker Mbili baridi,,, maana nadhani mishipa imekaza sana sasa hivi!!!
Mkuu kilitime, hii haiwezi kutulizwa kwa bia ya Tusker, hapa inabidi kutafuta chang'aa ile namba wani. Yaani ghafla nimejisikia kama nimesimamia shingo...!!!
 
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!

2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!

3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!

Mzalendohalisi,

Huu ndio ujinga wa Afrika, tunaibiwa na tunabaki kusema tuendelee mbele, utaendelea mbele vipi wakati kila kitu kinaibwa, umaskini unaongezeka na walio nacho wanaendelea kuwa matajiri kwa gharama ya mamilioni ya watu wengine?

Inabidi ifike mahali Afrika tufanye kama wanavyofanya Europe, walivyofanya Yugoslovakia, Ukraine, Georgia na kwingineko.

Tutaendelea kuburuzwa mpaka lini?
 
Ole,

Vipi sasa kuhusu ushauri wangu wa kufanya compilation ya posts zilizoko kwenye hii thread, halafu JF itoe kitabu cha yaliyojiri kwenye Kenya elections 2007?

Hivi ushauri tunautoa kwa nani? na ninani atafanya hiyo compilation? Alafu itatolewa/kuchapishwa wapi? Otherwise mimi ninaona kuna mambo mengi mazuri kwenye hii thread ..ingwafaa watu wengi wasiopitia mitaa hii ya JF!
 
Kitabu, kitabu! Mimi naomba tuandike kitabu. Sorry, I am a fool!
 
1. Mimi naona Utaifa mbele kwanza- hata Bush na Al Gore- kulikuwepo na hisia kama hizi za wizi wa kura- ila kiuungwana Al Gore alikubali yakaisha-Bush akawa rais na US wakasonga mbele!

2. Kama kuna mapungufu- basi yameshatokea. ODM wanweza kwenda Mahakamani. Pia wana wabunge wengi tayari!

3. Kuvumiliana tu na kusonga mbele!

Yeap! At the end of the day, ni nchi na watu. Watumie vizuri wingi wao bungeni. Cha muhimu sasa Raila akae na wabunge wake awalishe yamini ili wasinunuliwe na Kibaki. Vilevile aanze kuwa-lobby wale wabunge wa vyama vidogovidogo ili wawe upande wa Raila. Of course kelele za kumzomea Kibaki kwamba ameiba kura hukohuko bungeni ziendelee katika muda wote atakaokuwa madarakani.
 
Naomba kuwakumbusha kitu kimoja chaguzi nyingi za Kiafrika and probably nyingi au zote zilikuwa hivi hivi,,, tofauti ilikuwa huko nyuma hapakuwa na maendeleo ya ICT ambayo yalisaidia kupekua pekua kama chokora mambo ya Kura zimeibiwa mara zimeongezwa... wakati wa nyuma ulikuwa unaongeza kura unazotaka kama unamsukuma mlevi vile!!!

Kwa hiyo hapa ni technologia tu ndio imewasaidia kuwaambia mambo yalikuwa hivi siku zote kwenye chaguzi zetu za Kiafrika...

Mungu Ibariki Kenya, Mungu Ibariki Tanzania,,, Mungu Ibariki Afrika..

Raila waiting for plan B... kibaya sasa hivi watasema wewe ndio mkorofi,,, itategemea wajomba zetu wa USA, EU nk. wataegemea upande gani?

Na hicho ndicho kibaki anategemea hapa, ameiba election kisha vurugu itatokea na yeye ataanza kusema kuwa raila ndio mleta fujo!

what a shame!
 
sasa hiyo nyimbo inazungumzia zanzibar yetu hakuna matata inahusiana vipi na kenya? nnauliza tu maana nimeshindwa kupata picha
 
Hivi ushauri tunautoa kwa nani? na ninani atafanya hiyo compilation? Alafu itatolewa/kuchapishwa wapi? Otherwise mimi ninaona kuna mambo mengi mazuri kwenye hii thread ..ingwafaa watu wengi wasiopitia mitaa hii ya JF!

Ni ushauri kwa JF admin na site owners.
 
Back
Top Bottom