Kenya ilipigania uhuru wake. Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu

Mlipewa uhuru na Waingereza bure bila kumwaga damu. Ukweli huo haubadiliki hata ukijipiga kifua kuhusu matukio ya 1894.
 
Kwa hiyo katika vita vya majimaji Tanganyika ilipata uhuru? Hoja ya jirani yetu haiulizi mwanzo wa kukataa kutawaliwa,tulipataje uhuru?
A. Kupigana
B. Kupewa. Chagua jibu moja hapo
 
Imagine Mabeberu wange invest TZ kama walivyo invest KE, TZ ingekuwa wapi saiv maana hapo tu mshaachwa mbali kinoma na TZ
 
Tanzania haikusaidia Kenya kupata uhuru.
As early as the late 1950s Nyerere was publishing pamphlets castigating Whites in Kenya, South Africa and Rhodesia for rejecting the idea of African majority rule.[3] Nyerere and TANU continued this opposition to minority rule after Tanganyika’s independence, making it a defining feature of the government’s responsibilities. Speaking at the TANU National Conference in 1967, Nyerere declared that ‘total African liberation and total African unity are basic objectives of our Party and our Government…we shall never be really free and secure while some parts of our continent are still enslaved.’[4]
 
kinachonipa shida ni kua uwezo mdogo wa kufikiri au ndo kutoijua historia...hivi unadhani kila diplomasia lazima ifikie kwenye vita..pumbavu sana we jamaa
 
Bado una mawazo mgando kijana.... Fight is fight iwe kwa mdomo au silaha alafu kaa ukijua mdomo ni silaha kubwa sana so walaumu viongozi wako kwa kutoutumia vizuri... Over
 
Imagine Mabeberu wange invest TZ kama walivyo invest KE, TZ ingekuwa wapi saiv maana hapo tu mshaachwa mbali kinoma na TZ
Pole sana...
 
Kwa hiyo katika vita vya majimaji Tanganyika ilipata uhuru? Hoja ya jirani yetu haiulizi mwanzo wa kukataa kutawaliwa,tulipataje uhuru?
A. Kupigana
B. Kupewa. Chagua jibu moja hapo
Kwani hiyo Vita ya Mau Mau ilitoa uhuru kwa Kenya?!

Au unatakiwa kukumbushwa kwamba Mau Mau Uprising iliisha somewhere in 1956-1957 wakati Kenya Ilipata uhuru wake 1963?!
 
Kasome historia vzr,Tanganyika ilianza kupigania uhuru wake zamani sana,kulikuwa na vita ya majimaji,tulimchapa mjerumani,akashika adabu,je unawajua mtemi Isike,Milambo,wote Hawa walipigana kudai uhuru kwa nyakati tofauti.
Je unmjua Lucy Lameck,mwanamama,ambaye juzi,Ujerumani imempa heshima,kwa kubadili jina la mtaa mmoja,na kuuita kwa jina lake?
Shwaini mkubwa?!
 


HAPA NDIO UJUE NYIE MLIKUWA WATUMWA NA MNAENDELEA KUWA WATUMWA TU KWA MABEBERU

NJOO TZ KAMA UTAPATA HII UJINGA???
 
Mlipewa uhuru na Waingereza bure bila kumwaga damu. Ukweli huo haubadiliki hata ukijipiga kifua kuhusu matukio ya 1894.
Issue tulipata vipi uhuru au issue ni kwamba mliendelea kukumbatia wazungu hadi walipowapiga vidole kwa kuwatoa kwenye maeneo yenu ndi mkaamka kutoka kwenye usingizi wa pono wakati Tanganyika walianza kupigana na Wakoloni hata kabla Jomo Kenyatta na Dedan Kimathi hawajazaliwa!!!

Btw, ulitaka tuzipige na Mwingereza wakati hakuwa na hadhi ya ukoloni kwenye taifa letu?! Hivi huko shule huwa mnasomea ujinga, au?! Ikiwa tuliweza kupigana na Gaidi Mjerumani, tungeshindwa nini kupigana na Miwngereza endapo angeleta ule ushenzi aliowafanyia Wakenya wa kuwanyang'anya ardhi?!

Machungu ya kunyang'anywa ardhi na mkoloni hadi leo yapo Kenya kwa sababu most of ordinary Kenyans hawamiliki ardhi ya kutosha, not kwa sababu hawana hiyo passion bali ardhi yenu bado ipo kwa mabwenyenywe!!!

All in all, technically hata Kenya ilipewa uhuru bila kumwaga damu kwa sababu kuchapwa kwenu kwenye Vita vya Mau Mau hakukufanya mpate uhuru kama ambavyo kuchapwa kwa Tanganyika kupitia Maji Maji War hakukufanya Tanganyika kupata uhuru!

Kimsingi Kenya ilipata uhuru pale Mwingereza alipoamua kufungasha virago na kuondoka Afrika mashariki, na ndio maana, the whole of East African Protectorate ilipata uhuru kwa kufuatana!! And that also explains why hadi kufikia 1956 Mau Mau Fighters walishaufyata lakini uhuru hamkupata hadi mwishoni mwa 1963!!!
 
Mlipewa uhuru na Waingereza bure bila kumwaga damu. Ukweli huo haubadiliki hata ukijipiga kifua kuhusu matukio ya 1894.
tanzania ilkua chini ya un yani United nations trust territory kuanzia mwaka47 mwengereza altupa uhuru like how?

ivi tulpata uhuru toka un au Britain?
Chige
 
Ati "Kenya was" a settler economy,kwani family ya Lord Delamere hawana mashamba mpaka Sasa hivi huko Kenya?hivi nyinyi mlipapta Uhuru,au mlipandisha benders yenye rangi nne eti mmepata Uhuru?mpaka Sasa hivi mnapokea amri kutoka kwa wazungu kuhusu maswala ya nchi yenu,huo ni Uhuru?Nchi za kigeni Zina kambi za kijeshi kwenye ardhi yenu,mna uhuru gani?
 
Diplomasia ya Tanzania is way greater than ile ya Kenya; sisi tulihitaji KUZUNGUMZA TU tukajinyakulia uhuru wetu. Jamaa wao ilibidi mpaka waunde MAUMAU Resistance. It is safe to say, Tanzania siyo tu KISIWA CHA AMANI, bali pia KITOVU CHA DEMOKRASIA & DIPLOMASIA.

"It is high time for African continent to think for herself the true meaning of democracy in her own context and culture, taking into consideration her historical background. Limitation of multipartism, periodic elections, and term limits for leaders in responsible positions is not only impractical but also feasibly ineffective!" -- Prof. Patrice Lumumba.
 
Wasamehe hawa majirani, hawana ufahamu wowote kuhusu vita vya Mau Mau na ukombozi wa Taifa la Kenya kutoka kwa minyororo ya mkoloni. Isipokuwa vita vya makaburu SA dhidi ya muingereza(Boer Wars) na vita vya kuikomboa India hakuna vita vyovyote vingine duniani ambavyo vilimpa mkoloni wakati mgumu kama vya Mau Mau. Mkoloni alidondosha hadi mabomu kwa kutumia ndege za kivita kwenye maficho ya wapiganaji wa Mau Mau maeneo ya Ml. Kenya na Abardares. Wenyeji wa Ml. Kenya karibia milioni moja walihamishwa makwao na kufungiwa kwenye 'concentration camps' kama za Hitler/NAZI. Kisa eti mkoloni alisema kwamba wote walikuwa wamekula kiapo cha Mau Mau. Babu yangu alikuwa mpiganaji mashuhuri wa Mau Mau. Ukiona rangi nyekundu kwenye bendera ya Kenya jua kwamba damu ilimwagika kweli sio mzaha. Alafu kwa historia kama hiyo eti ndio leo tujifananishe na watu ambao waliketi kwenye meza moja wakinywa chai na mabeberu na kujadiliana kuhusu uhuru wao. Ní urímú!
 
maumau iliwapa uhuru?
je mlishinda vita vya maumau?
 
Majimaji walipigana zamani sana tena walikuwa wanapigana dhidi ya Wajerumani. Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Ujerumani ndio alikuwa mkoloni sasa, English wao walishikizwa na UN baada Ya Germany kushindwa ile 2nd WW
 
maumau iliwapa uhuru?
je mlishinda vita vya maumau?
Ndio, vita vya Mau Mau ndio viliipa Kenya Uhuru. Mkoloni alilazimika kuwakubalia waafrika weusi wajipange kisiasa kupitia vyama vyao kwasababu ya vita vya Mau. Chama cha KADU kiliamrishwa kitengeneze serikali kabla ya Uhuru. Kama njia ya mkoloni kujaribu kuingiza migawanyiko na usaliti kwa chama cha KANU ila wakaibuka na kauli kwamba lazima Kenyatta na wenzake(Kapenguria Six) waachiwe huru kwanza. Vita vya Mau Mau vilikuwa 'Guerilla War', yaani kama vya waasi ambao huwa wanampiga adui yao kisha wanarudi mafichoni. Harasa ilikuwa ni kwa mkoloni, kihali, kimali, kiraslimali kupitia usumbufu ambao ulifanya koloni lake liendeshwe kijeshi, bila mpangilio, bila amani, bila faida.
 
Hata Kenya ilipewa pia acheni kujidanganya, Muzungu aliondoka Kenya na Afrika kwa hiari, ...
 
kinachonipa shida ni kua uwezo mdogo wa kufikiri au ndo kutoijua historia...hivi unadhani kila diplomasia lazima ifikie kwenye vita..pumbavu sana we jamaa
Ninarudia tena. Tanzania haikusaidia Kenya kupata Uhuru. Tuliunyakua uhuru wenyewe kutoka kwa mikono ya beberu kwa kupigana hadi kufa. Tulimwaga damu ili tupate uhuru wetu. Nyie hamkutusaidia kwa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…