Kenya ilipigania uhuru wake. Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu

Wewe ni mjinga sana kama unaamini kushinda vita ina maanisha kuuwa mzungu kabisa na kumuangamiza. Una akili finyu hadi nasita kudebate na wewe. Kwa hivyo tunaposema Algeria alipigania uhuru kutoka kwa Wafaransa na kunyakua uhuru unadhani Algeria alimuangamiza kabisa Mfaransa? Hizi ni resistance movements na lengo lao haikuwa kumuangamiza kabisa Mzungu bali kufanya utawala wake uwe mgumu. FLN waliuwa natives waliokuwa wanacollaborate na Wazungu. Algeria walikuwa wanalipua hadi mighahawa ya wazungu. Vile vile Mau Mau walikuwa wanauwa waafrika wanaoshirikiana na wazungu. Hii haikuwa conventional warfare bali iliiuwa guerilla warfare. Sasa kati ya Vietnam na Marekani ni nani alishinda hio vita? Kumbuka Marekani aliuwa watu wa Vietnam wengi sana lakini kwa vita hatuhesabu sana idadi ya watu waliouawa. Tunahesabu nani alifikia malengo yake na nani alishindwa kufikia malengo yake. Kumbuka Marekani alishindwa kufikia malengo yake ya kufaya South Vietnam iendelee kuwa an independent capitalist country. North Vietnam ndio ilishinda vita kwa sababu ilifikia malengo yake ya kuunganisha North Vietnam na South Vietnam kuwa nchi moja japo walipoteza watu wengi sana kwenye hio vita. Wewe unadhani kushinda vita ni lazima uangamize adui yako. Una ushamba nyingi
 
Hata tubishe kiasi gani huo utabaki kuwa ndo kwelj....na hata tofauti yetu ya kimaendeleo huwa inaaanzia hapo....yn happy ndo kwenye mizizi ya tofauti ya kimaendeleo Kati ya nchi hizi mbili.....


Mkichukue comment yangu Basi mnipige tu.
 
Binafsi sidhani kama kenya ni nchi huru,maana mpaka hii leo kwa afrika hamna nchi inayowasujudia watu weupe kama kenya,mkenya yuko tayari ampe hata mkewe mtu mweupe ili apate kujisifu mkewe alishamegwa na mzungu
 
Kwa nini unafikiri Muzungu aliweka mkataba na China na siyo Kenya ? Au Kenya pia kulikuwa na Mkataba ?
Wewe ulitaka kumaanisha kuwa Muingereza anafanya akitakacho. Anapatia watu uhuru wakati yeye mwenyewe anapenda. Mimi nikakuweka sawa nikakueleza kuwa mzungu hakupatia Hong Kong Uhuru kwa hiari yake bali alilazimishwa na mkataba aliyokuwa ametia saini hapo awali. Mzungu hawezi kupatia mtu yeyote uhuru bila kushurutishwa aidha kisheria kupitia mkataba kwa mfano Hong Kong au kivita. Na akipatia nchi uhuru bila vita basi hio nchi itakuwa haina umuhimu kwake kama Zambia au Uganda.
 

Sasa ungesema kwamba resistance ilipelekea Muzungu kuipa Kenya uhuru wake, kama ni hivyo resitance ilikuwepo kila mahali, ila kama nilivyosema nchi za Kiafrika hazikupewa uhuru kwa sababu walishinda Vita dhidi ya Wakoloni la hasha, bali muda wa Ukoloni ulikuwa umekwisha baada ya WW 2 Dunia mpya ilianza chini ya USA na UN 1945, kwa Makoloni ya Uingereza alianza India 1947, kwa Afrika alianza Ghana 1957 na kufwatia wengine miaka 60 'mwanzoni na sababu ilikuwa ni kwamba Dunia ilikuwa imebadilika, hata French colonies pia walipata Uhuru wao miaka ya sawa i.e 1960's na English colonies unafikiri hiyo ilitokea tu ?
 
Huu utopolo ulioandika sasa utasema kuwa Zimbabwe walipewa uhuru bure wakati Ian Smith alitangaza uhuru wa nchi ya Zimbabwe kutoka Uingereza lakini Uhuru huo ulikuwa wa wazungu pekee. Ilibidi waafrika akina Mugabe waingie kwenye misitu kunyakua uhuru wao kutoka kwenye mikono ya wazungu watukutu kama akina Ian Smith. Wazungu hawawezi kupeana uhuru ovyo ovyo tu. Kwanza settler colonies Kenya, Zimbabwe na South Afrika zilikuwa settler colonies za Waingereza. Mozambique na Angola zilikuwa settler colonies za Wareno na wareno hangepeana uhuru bila vita maana walikuwa wanaishi huko. Tanzania wazungu hawakuwa wanaishi huko ndio maana mlipewa uhuru bila vita
 
Amini unachotaka.
 

Unachanganya mambo, Zimbabwe hakuwa hivyo unafikiria wewe, ngoja nikupe shule kidogo kuhusu kilichotokea Zimbabwe, Muzungu wa Zimbabwe aligoma kuwa chini ya English monarchy na kutaka kujitenga ili Zimbabwe iwe kama AK, Muzungu london akagoma, Muzungu akasapoti gorrilla communist ambao ni akina Mugabe dhidi ya Muzungu Zimbabwe akina Ian Smith, kwa kifupi ilikuwa ni vita kati ya Waasi wa Kizungu akina Ian Smith vs English Monarchy, na Mugabe alitumiwa na Muzungu London kama proxy, na ndio maana Mugabe alikuwa na deni na British Government hata ile kuchukuwa na mashamba ya Muzungu hiyo ilikuwa ni moja ya sababu, English monarchy walimuahidi Mugabe baada ya vita kuna vitu angepata kutoka kwa akina Ian Smith, ...
 
Una evidence ya huu utopolo ulioandika ama unadhani hapa ni vijiweni? Tangu lini Muingereza aanzishe vita dhidi ya muingereza mwenzake kwa kusapoti mwafrika(Mugabe)?
 
Una evidence ya huu utopolo ulioandika ama unadhani hapa ni vijiweni? Tangu lini Muingereza aanzishe vita dhidi ya muingereza mwenzake kwa kusapoti mwafrika(Mugabe)?

Ndivyo ilivyokuwa, Settlers wa Zimbabwe walitaka kujitenga na English Monarchy wawe na nchi yao ya Rhodesia, English monarhy akakataa, na ndipo vita ilipoanza English monarchy akasapoti communist Mugabe dhidi ya Rhodesian, unaweza kujisomea iko wazi kila mahali.

Mugabe alisaidiwa na English Monarchy dhidi ya Settlers, ilikuwa ni proxy war, soma kuhusu Lancaster agreement kama ukipenda utapata mwanga wa kilichotokea, ilikuwa ni Vita kati ya White Rhodesian vs English Monarchy ambao walimtumia Mugabe kupigana, ...
 
Kama unadhani hayo yalifanyika kwa ajili ya Mau Mau War, ulishawahi kujiuliza ni kwanini Uingereza iliachia makoloni kibao tu kwenye miaka ya ya 50 na 60?!

Ukweli ni kwamba, baada ya World War II, British Empire ikajikuta ina mzigo wa makoloni ambayo ilikuwa ni very expensive kuyaendesha. Na wakati hayo yanatokea, British Empire pia ilifahamu kulikuwa na vuguvugu la kutaka kujitawala kutoka kwenye makoloni karibu yote duniani!

Aidha, Wakoloni hawa tayari walifahamu ni wenyeji wa makoloni yao ndio hao hao walipigana Vita vya II na ya II ya dunia, na hivyo kuwa red flag kwa kufahamu tayari baadhi ya wenyeji kwenye makoloni yao walishakuwa na uzoefu wa kivita, na kwamba hilo lilikuwa ni bomu lililosubiri kuwaripukia muda wowote!!

Ni kutokana na combination ya yote hayo ndipo British Empire ikatengeneza Decolonization Policy and Roadmap! Wakaanza kujiondoa nchi za Asia kutoka nchi moja hadi nyingine, kisha roadmap ikaingia Africa!! Na ukiangalia, nchi nyingi za Afrika zilipata uhuru kwa kufuatana! Kenya nayo ikapata uhuru wake kama walivyopata Uganda, Zanzibar, Sudan n.k!

Vita vya Mau Mau was just a good timing lakini hata kama vita vile visingekuwepo bado Mwingereza angeondoka tu kama ambavyo aliondoka Zanzibar, Uganda, Sudan, na mataifa mengine kadhaa!!!
 
Definately
 
Waambie manyang'au hayo mpaka leo hayajui siasa. Bado yanaongozwa kwa remot from abroad. Sisi wazee wetu akina Nyerere walijua kujenga hoja from the begining na ndio uhuru wa bila kumwaga damu. Tanzsnia ni baba wa diplomasia in East Africa, weather you like or not.
 


Mkuu unaturudisha darasani 😁😁😁

Kiukweli huwa najiuliza Kenya kulikuwa na tawala zenye nguvu ama jamii zilizoendela kabla ya mkoloni ngapi zenye level za Hehe ama Nyamwezi ???...

Maana Uganda tunajua kulikuwa kuna Buganda na Bunyoro ila Kenya sijawahi kusikia labda unijuze mkuu

Kingine sababu mojawapo ya kuanzisha settler economy ni kupata less resistance kutoka kwa wazawa which means walikuwa weak sana kutoa upinzani wa namna yoyote hivyo, Ukitoa maumau kulikuwa kuna vita nyingine yoyote ile Kenya maana kwetu ukiitoa majimaji bado zilikuwepo nyinginezo
 
Wonderful, tangu lini Kenya ikawa huru ?
 
Usitutajie habari za resistance, tutajie vita mlizopigana kabla Mkoloni Mwingereza hajawafundisha jinsi ya kupigana!!!

Usisahau, Mau Mau ilianza 1952... matunda ya Mwingereza kuwafundisha jinsi ya kupigana kwa sababu hapo kabla mlikuwa mnaendeshwa kama misukule tu kwenye mashamba ya chai, huku wengine wengi wakitimuliwa kwenye ardhi zao!!!
 
You're 100% RIGHT... Kenya hakukuwa na dola lolote la kumtisha Mkoloni kama ilivyokuwa Dola la Nyamwezi, Hehe, na madola mengine kadhaa yaliyokuwa chini ya Machifu na Watemi mbalimbali Tanganyika kabla ya ukoloni!

Ni kutokana na hilo, ndio maana haishangazi kuona vita yao ya kwanza kueleweka ni ile ya Mau Mau ambayo kimsingi, ni matunda ya Askari wa Afrika waliokuwa wamepigana kwenye Vita Kuu ya I na ya II lakini sio askari kama wa Mkwawa au Kinjekitile ambao completely local with no any modern military training lakini wakazichapa na Mwingereza huku Wakenya wakilimishwa kwenye mashamba ya chai na wengine wakitimuliwa kutoka kwenye ardhi zao!!!!
 
Usitutajie habari za resistance, tutajie vita mlizopigana ambazo Tanganyika hawakupigana! Hizo resistance zipo na zitaendelea kuwepo!!
Unajua maana ya resistance/rebellion au unakariri tu? Kwani kulikuwepo na 'full-blown' war ingine wakati wa mkoloni isipokuwa vita vya Mau Mau?
 
Majimaji walipigana zamani sana tena walikuwa wanapigana dhidi ya Wajerumani. Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Tanganyika haikuwa koloni la Waingereza bali ilikuwa koloni la Wajerumani lakini baada ya Vita ya Pili ya Dunia Wajerumani walinyang'anywa Tanganyika ikiwa ni mojawapo ya adhabu waliyopewa Wajerumani ambapo walinyang'anywa makoloni yao yote duniani na Tanganyika walipewa Waingereza kuisimamia tu ikingojea kupata uhuru kamili kwa kuwa Tanganyika ilionekana tayari imeshakuwa civilized zaidi ya Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…