Kenya ilipigania uhuru wake. Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu

Unajua maana ya resistance/rebellion au unakariri tu? Kwani kulikuwepo na 'full-blown' war ingine wakati wa mkoloni isipokuwa vita vya Mau Mau?
In short umeshindwa kujibu, na ndo matatizo ya kubishana na kizazi ambacho babu zao walikuwa wanaogopa Wazungu hadi wakaishia kunyang'anywa ardhi zao huku wakiangalia tu!!!

Hebu wasome Wakenya wenzako Nairobi Wire:-
Again,:-
Yaani hata baada ya Mkoloni kuwapa ujanja wa kupigana na hatimae Babu zenu wakatoka usingizini na kujiripua kupitia Vita ya Mau Mau lakini bado ardhi yenu mmeiacha kwenye mikono ya Wazungu!!! Hivi mpo timamu kweli nyie?! Sasa mlikuwa mnapigania nini?
 

Hujaijua historia wewe. Hebu tulia. Kupigania uhuru haikuwa event, bali ni process. Na ilianza kipindi cha akina Isike, Mkwawa, Kinjeketile ngwale et al.
Pia usiongee habari za kupigania uhuru, kipindi cha baada ya Berlin Conference.
 
Majimaji walipigana zamani sana tena walikuwa wanapigana dhidi ya Wajerumani. Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Muingereza hakutawala Tanganyika kama colony...baada ya mjerumani kuondoka Tanganyika ilikua tu protectorate haikua tena colony na Muingereza alipewa majukumu ya kusimamia nchi hadi pale watu wake wakiweza kujitawala wenyewe...kama kupigana tulishapigana sana kuanzia Majimaji hadi wakina Mkwawa....nenda kawaulize wajerumani Mkwawa ni nani wakupe jibu
 
Unatapatapa tu bila formular. Ulianza kwa kusema kwamba mlipewa uhuru wenu kwasababu tofauti yenu na wakenya ni kwamba mlianza vita dhidi ya mkoloni mapema sana. Nikakutajia Nandi Resistance, Giriama Resistance ya Mekatilili wa Menza na vita vya Waiyaki wa Hinga na wenzake, vyote ambavyo vilitokea late 1800s- early 1900s. Sasa baada ya kuchanganyikiwa na neno 'resistance' umeanza kutupia caption kutoka Nairobi Wire. Nigga are you sober? 😁
 
Kama kweli kenya ilimwaga damu na kujitapa kuwa mlipata Uhuru kwa kupigana mbona kuna mkanganyiko??
maana mimi naona hao (watanzania) mnaowaita ni lele mama walipata Uhuru kwa kupewa iweje wawe na kauli za kishujaa kwa hao waliowapa Uhuru bure, kuliko nyie ambao mnajiita mashujaa mlio mwaga damu mpaka leo bado amuwezi kumtunisia misuli mzungu ata iweje naludia tena ata iweje......

Aibadilishi ukweli kuwa kisa atukumwaga damu basi Tanzania haitotambulika kama nchi shujaa iliyosaidia nchi kazaa afrika kupata Uhuru wao.



Kwa nionavyo mimi Kenya inaweza kuwa huru kama wataanza na sheria ya umiliki ardhi kama upande wa Tanzania.
Linaweza kuonekana ni suala dogo ila ukiliangalia kwa undani na umakini uwenda matatizo yote huanzai apa kuanzia ukabila,rushwa,ajira nk.
Mpaka Leo hii mzungu ndo amemiliki ardhi yenye lutuba,selikali hutumia pesa nyingi kwenye kuleta maendeleo ya uma mfono, nilishangaa kuna uzi niliuona unasema Mombasa nzima akuna stendi ya mabasi, kwa sabau akuna eneo la Kuweka stendi ili kuwe na stendi itabidi selikali itumie pesa nyingi kwa kuwalipa wananchi wanaomiliki hiyo ardhi hiyo.
Ambapo uku tanzania ulipwa tu fidia kwa sababu mwisho wa siku si wewe tuu utakao faidika ni jamii nzima
 
Shukrani sana,umeelezea vizuri.Kama ni mwalimu,nina hakika wanafunzi wako ni wa grade A tupu.
 
Walio pigania Uhuru wa Kenya ni wakikuyu wajaluo walikua na wazungu
 
Unaposema wazungu unajumuisha kundi kubwa sana, sema Waingereza kwasababu hata wajerumani walioifanya Tanganyika yao, nao pia ni wazungu. Tena wajerumani waliokaa Tanganyika chini ya miaka 30 tuu, walijenga mtandao mkubwa wa reli kuliko ule waliojenga waingereza Kenya kwa kukaa miaka 75.
Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Haujui unachokisema, Waingereza hawakutupa uhuru, kwa kuwa sisi hatukuwa koloni lao. Kama waliputa (kama unavyodai), ni kwa nini Mwl Nyerere alienda New York kudai uhuru badala ya London?
 
tanzania ilkua chini ya un yani United nations trust territory kuanzia mwaka47 mwengereza altupa uhuru like how?

ivi tulpata uhuru toka un au Britain?
Chige
Bro, kabla ya hapo tulikuwa chini ya the league of nations 1920, ambayo ndiyo ilikuja kuwa UNO (1945).
 
Papara za nini wewe, kama ungenisoma vizuri ungekumbuka pale niliposema Wajerumani walikaa miaka 30 tuu Tanganyika wakati Waingereza walikaa miaka 75.

Na siyo tuu walijenga reli bali miji mingi tuu walisanifu wao, ikiwemo Dar (CBD na Kariakoo), Tanga, Bagamoyo, Tabora, Kigoma, Moshi, n.k (miaka 30 tuu). Huwezi fananisha miak 30 na 75.
Hapo umedandia treni kwa mbele, nilikuwa namjibu Tony254 ila kwasababu unaonekana uko safarini (nigga, you must be trippin' on some shrooms), nitakuacha uendelee na safari yako.
 
so mkuu sie uhuru tuliupata uno na sio uengereza kama mleta mada alivosema?
vipi unakubali tuliupata bwerere pasipo kuupigania? refer machifu waliopigana mfn:isike mkwawa na nk
 
Waingereza hawakukaa Tanzania kwa miaka 75. Mbona unavuta bangi kijana? Kufanya hesabu kidogo hivi imekushinda?
 
Punguza dozi ya uyoga wewe, ni wapi nimesema walijenga? Nilisema walisanifu nikimaanisha wao ndio walioichora CBD na Kariakoo. Wewe utakuwa ni wakuja, kudhani kariakoo ilianza '74.
 
Isitoshe hilo jitu linadanganya kuwa Waingereza walitawala Tanzania kwa miaka 75. Jamaa hata hajui historia yake.
 
Waingereza hawakukaa Tanzania kwa miaka 75. Mbona unavuta bangi kijana? Kufanya hesabu kidogo hivi imekushinda?
Na wewe miraa imeanza kukupeleka peleka, nioneshe niliposema Waingereza walikaa Tanzania miaka 75?
 
Soma mahali ambapo nimehighlight na rangi nyekundu. Ndio ujue kwamba wewe ni wazimu. Hujui unachozungumzia.
 
Soma mahali ambapo nimehighlight na rangi nyekundu. Ndio ujue kwamba wewe ni wazimu. Hujui unachozungumzia.
Ndiyo matatizo ya kuwa na mihemeko haya, hapa nilikuwa namjibu mwenzako, ikiwa ni muendelezo kutoka posti #92, hii hapa chini.

 
maswali langu la msingi ni je tulipigana au la?
kama tulipigana what was the motive of the war?
je kwa maelezo yako apo juu utaungana nami kusema africa yote kutoa Ethiopia tulpata uhuru wa bwerere maana hatukuwashinda wazungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…