Kenya ilipigania uhuru wake. Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu

Kenya ilipigania uhuru wake. Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu

Unajua maana ya resistance/rebellion au unakariri tu? Kwani kulikuwepo na 'full-blown' war ingine wakati wa mkoloni isipokuwa vita vya Mau Mau?
In short umeshindwa kujibu, na ndo matatizo ya kubishana na kizazi ambacho babu zao walikuwa wanaogopa Wazungu hadi wakaishia kunyang'anywa ardhi zao huku wakiangalia tu!!!

Hebu wasome Wakenya wenzako Nairobi Wire:-
A few families, stretching from colonial times, to this day control thousands upon thousands of acres. The one place they’ve been able to acquire endless tracts of land is Laikipia.

Laikipia plateau is estimated to be about 10,000 sq km or roughly 2.5 million acres. It has the biggest number of white landowners concentrated in one place, in Kenya. The plateau stretches from Mt Kenya in the east to the Rift Valley in the west.
Again,:-
The Maasai community here numbers less than 50,000. They are squashed on different patches of the land, which totals 281,587 acres. The rest (more than 2 million acres) is owned by a foreigners comprising mostly the British and American “aristocratic” class and a few white natives.
Yaani hata baada ya Mkoloni kuwapa ujanja wa kupigana na hatimae Babu zenu wakatoka usingizini na kujiripua kupitia Vita ya Mau Mau lakini bado ardhi yenu mmeiacha kwenye mikono ya Wazungu!!! Hivi mpo timamu kweli nyie?! Sasa mlikuwa mnapigania nini?
 
Watanzania huwa wana kiburi ya hali ya juu sana maana wanaamini kuwa wao ndio waliikomboa Afrika kutoka kwa Mabeberu. Ukiona waziri wao akifoka jinsi waliikomboa Afrika hadi mate inamtoka mdomoni na mishipa kuvimba kichwani ndio utajua kwamba hii propaganda ya CCM ni nzito sana.

Ukweli wa mambo ni kuwa nchi chache sana hapa Afrika zilipigania uhuru wao. Nchi zilizopigania uhuru kwa kumwaga damu hazijapita 12 hapa Afrika. Nitataja baadhi yao: Kenya, Guinea Bissau, Mozambique, Zimbabwe, South Africa, Angola, Algeria na zingine chache. Nchi nyingi za Afrika zilipewa uhuru wao bure bila vita. Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizopewa uhuru bure kabisa na beberu bila Watanzania kuingia msituni kumenyana na Mzungu. Hamkumwaga damu ili kupigania uhuru wenu.

Kama nyie ni wakombozi wa Afrika mbona hamkuikomboa Kenya kutoka kwa mabeberu? Mabeberu waliua Wakenya karibia laki moja wakati wa state of emergency 1952 wakati wanapigana na Maumau. Wamama na watoto wakapelekwa kwenye concentration camp ambapo wengi walikufa kwa njaa. Wanaume walipelekwa gerezani na kuteswa na kuuawa.

Hata nchi ya Uingereza imeomba msamaha kwa ushetani waliotufanyia na kutoa pesa kama fidia. Mbona nyie hamkutusaidia? Mbona sisi tulijipigania uhuru wenyewe na kufa kwa wingi ili tupate uhuru wetu? Hakuna nchi yoyote ya Afrika iliyotusaidia kupata Uhuru. So nyamazeni. Hata hamkupigania uhuru wenu mlipewa bure. We don't owe you anything. Hatuna deni lenu maana nyie hamkutusaidia.

Hujaijua historia wewe. Hebu tulia. Kupigania uhuru haikuwa event, bali ni process. Na ilianza kipindi cha akina Isike, Mkwawa, Kinjeketile ngwale et al.
Pia usiongee habari za kupigania uhuru, kipindi cha baada ya Berlin Conference.
 
Majimaji walipigana zamani sana tena walikuwa wanapigana dhidi ya Wajerumani. Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Muingereza hakutawala Tanganyika kama colony...baada ya mjerumani kuondoka Tanganyika ilikua tu protectorate haikua tena colony na Muingereza alipewa majukumu ya kusimamia nchi hadi pale watu wake wakiweza kujitawala wenyewe...kama kupigana tulishapigana sana kuanzia Majimaji hadi wakina Mkwawa....nenda kawaulize wajerumani Mkwawa ni nani wakupe jibu
 
In short umeshindwa kujibu, na ndo matatizo ya kubishana na kizazi ambacho babu zao walikuwa wanaogopa Wazungu hadi wakaishia kunyang'anywa ardhi zao!!! Hebu wasome Wakenya wenzako Nairobi Wire:-Again,:-Yaani hata baada ya Mkoloni kuwapa ujanja na hatimae Babu zenu wakatoka usingizini na kujiripua kupitia Vita ya Mau Mau lakini bado ardhi yenu mmeiacha kwenye mikono ya Wazungu!!! Hivi mpo timamu kweli nyie?! Sasa mlikuwa mnapigania nini?
Unatapatapa tu bila formular. Ulianza kwa kusema kwamba mlipewa uhuru wenu kwasababu tofauti yenu na wakenya ni kwamba mlianza vita dhidi ya mkoloni mapema sana. Nikakutajia Nandi Resistance, Giriama Resistance ya Mekatilili wa Menza na vita vya Waiyaki wa Hinga na wenzake, vyote ambavyo vilitokea late 1800s- early 1900s. Sasa baada ya kuchanganyikiwa na neno 'resistance' umeanza kutupia caption kutoka Nairobi Wire. Nigga are you sober? 😁
 
Kama kweli kenya ilimwaga damu na kujitapa kuwa mlipata Uhuru kwa kupigana mbona kuna mkanganyiko??
maana mimi naona hao (watanzania) mnaowaita ni lele mama walipata Uhuru kwa kupewa iweje wawe na kauli za kishujaa kwa hao waliowapa Uhuru bure, kuliko nyie ambao mnajiita mashujaa mlio mwaga damu mpaka leo bado amuwezi kumtunisia misuli mzungu ata iweje naludia tena ata iweje......

Aibadilishi ukweli kuwa kisa atukumwaga damu basi Tanzania haitotambulika kama nchi shujaa iliyosaidia nchi kazaa afrika kupata Uhuru wao.

Kwa nionavyo mimi Kenya inaweza kuwa huru kama wataanza na sheria ya umiliki ardhi kama upande wa Tanzania.
Linaweza kuonekana ni suala dogo ila ukiliangalia kwa undani na umakini uwenda matatizo yote huanzai apa kuanzia ukabila,rushwa,ajira nk.
Mpaka Leo hii mzungu ndo amemiliki ardhi yenye lutuba,selikali hutumia pesa nyingi kwenye kuleta maendeleo ya uma mfono, nilishangaa kuna uzi niliuona unasema Mombasa nzima akuna stendi ya mabasi, kwa sabau akuna eneo la Kuweka stendi ili kuwe na stendi itabidi selikali itumie pesa nyingi kwa kuwalipa wananchi wanaomiliki hiyo ardhi hiyo.
Ambapo uku tanzania ulipwa tu fidia kwa sababu mwisho wa siku si wewe tuu utakao faidika ni jamii nzima
 
Na hapo ndo uone tofauti kati ya Tanganyika na Kenya!!!

A moment colonists set their feet in Tanganyika, Mababu zetu waka-react!!

Mwaka 1891, miaka 6 tu baada ya Mkoloni Mjerumani kuanzisha utawala wake, Wahehe wakiongozwa na Mkwawa wakapigana na Mjerumani!!! Kumbukumbu zinaonesha, battalion ya kwanza ya Mkoloni Mjerumani ilifyekwa na wakalazimika kutimua mbio!!

Mwaka 1994 Wajerumani wakapeleka battalion nyingine... Wahehe wakapigana na mkoloni kwa miaka 4 hadi 1898.

Miaka 7 baadae, yaani mwaka 1905, Mkoloni wa KIjerumani akakumbana na mtiti mwingine sehemu ya Pwani ya Tanganyika kuelekea kusini!! Ingawaje Wazee wetu hawakuwa na zana zozote za maana za kivita, lakini mtiti uliendelea kwa miaka 2 hadi 1907!!

Unlike Kenya through Mau mau ambapo baada ya kukamatwa kwa kiongozi wake tu Wakenya wakaanza kufyata mkia, lakini kukamatwa mapema kwa Kinjektile Ngwale kiongozi wa Vita vya Maji Maji hakukufanya vita hivyo kuishia hapo kwa sababu ndo kwanza vita vikazidi kuenea kutokea Kilwa ilikoanzia hadi Morogoro na Ruvuma!!!

Kwahiyo ni kukosa maarifa kudhani Mau Mau Uprising ni tofauti na Maji Maji wakati vita vyote vilikuwa ni dhidi ya mkoloni!

Ni ukosefu wa Maarifa kui-rate Mau Mau kwa sababu tu ilichelewa kuanza wakati kimsingi uchelewaji huo inaonesha ni namna gani mlivyokuwa waoga kupambana na mkoloni!!

Yaani tangia 1885 mlikuwa kwenye usingizi wa pono hadi 1952 wakati Tanganyika kwa wakati huo tulikuwa tayari tumeshaonesha hatutaki ujinga miaka kadhaa iliyopita, kabla hata Wapiganaji wa Mau Mau hawajazaliwa!!!!

Na lau kama Mwingereza angeendeleza ubabe wa Kikoloni, bado Mababu ya Kitanganyika yangesimama against that colonist that was being entertianed in Kenya kwa zaidi ya miaka 60!!!!

That's TANGANYIKA, the father of TANZANIA... the same son who never bowed down even to the Boers you used to bed with!!!
Shukrani sana,umeelezea vizuri.Kama ni mwalimu,nina hakika wanafunzi wako ni wa grade A tupu.
 
Watanzania huwa wana kiburi ya hali ya juu sana maana wanaamini kuwa wao ndio waliikomboa Afrika kutoka kwa Mabeberu. Ukiona waziri wao akifoka jinsi waliikomboa Afrika hadi mate inamtoka mdomoni na mishipa kuvimba kichwani ndio utajua kwamba hii propaganda ya CCM ni nzito sana.

Ukweli wa mambo ni kuwa nchi chache sana hapa Afrika zilipigania uhuru wao. Nchi zilizopigania uhuru kwa kumwaga damu hazijapita 12 hapa Afrika. Nitataja baadhi yao: Kenya, Guinea Bissau, Mozambique, Zimbabwe, South Africa, Angola, Algeria na zingine chache. Nchi nyingi za Afrika zilipewa uhuru wao bure bila vita. Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizopewa uhuru bure kabisa na beberu bila Watanzania kuingia msituni kumenyana na Mzungu. Hamkumwaga damu ili kupigania uhuru wenu.

Kama nyie ni wakombozi wa Afrika mbona hamkuikomboa Kenya kutoka kwa mabeberu? Mabeberu waliua Wakenya karibia laki moja wakati wa state of emergency 1952 wakati wanapigana na Maumau. Wamama na watoto wakapelekwa kwenye concentration camp ambapo wengi walikufa kwa njaa. Wanaume walipelekwa gerezani na kuteswa na kuuawa.

Hata nchi ya Uingereza imeomba msamaha kwa ushetani waliotufanyia na kutoa pesa kama fidia. Mbona nyie hamkutusaidia? Mbona sisi tulijipigania uhuru wenyewe na kufa kwa wingi ili tupate uhuru wetu? Hakuna nchi yoyote ya Afrika iliyotusaidia kupata Uhuru. So nyamazeni. Hata hamkupigania uhuru wenu mlipewa bure. We don't owe you anything. Hatuna deni lenu maana nyie hamkutusaidia.
Walio pigania Uhuru wa Kenya ni wakikuyu wajaluo walikua na wazungu
 
Hili swali tulilifanya O' Level kwenye somo la History.

Ni rahisi kabisa

Kenya was designed to be Mzungu's country kabisa kama ilivyo Australia au South Africa au United States kabisa, sio iwe ni ya kuchukua mali na kuondoka

Wazungu walitaka Kenya iwe nchi yao ya kuishi moja kwa moja, shida ni kwamba walikuja ila idadi ikawa ndogo

Tanzania wazungu walikua hawataki kuishi humo moja kwa moja, walidizaini kama ni eneo la kuchukua raw materials tu na sio kuishi moja kwa moja

Uhuru wa Tanzania ilikua ni very easy maana hata ule mkataba wa Wakoloni ulikua very loose maana ilikua ni kama shamba tu wala mzungu hakuitaka kiivyo

Kenya ilikua tofauti, Kenya was Mzungu's native ardhi ya kuishi moja kwa moja

Hili swali tulilifanya na marks zake zilikua 25% na watoto walifaulu hili swali

Tanzania was no appealing to the whites, sababu ya hali ya hewa, culture, magonjwa, resistance kutoka kwa locals maana walikua wanaunganishwa na Kiswahili, etc
Unaposema wazungu unajumuisha kundi kubwa sana, sema Waingereza kwasababu hata wajerumani walioifanya Tanganyika yao, nao pia ni wazungu. Tena wajerumani waliokaa Tanganyika chini ya miaka 30 tuu, walijenga mtandao mkubwa wa reli kuliko ule waliojenga waingereza Kenya kwa kukaa miaka 75.
Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Haujui unachokisema, Waingereza hawakutupa uhuru, kwa kuwa sisi hatukuwa koloni lao. Kama waliputa (kama unavyodai), ni kwa nini Mwl Nyerere alienda New York kudai uhuru badala ya London?
 
tanzania ilkua chini ya un yani United nations trust territory kuanzia mwaka47 mwengereza altupa uhuru like how?

ivi tulpata uhuru toka un au Britain?
Chige
Bro, kabla ya hapo tulikuwa chini ya the league of nations 1920, ambayo ndiyo ilikuja kuwa UNO (1945).
 
Mkuu unakua disingenuous tu....Wazungu wa Kenya nazungumzia Waingereza.....Unajua sema umeamua kuzengua tu

Waingereza walienda kwa dhumuni la kukaa moja kwa moja na sio kwenda na kuondoka...

Kuhusu kujenga reli TZ,umechukua mfano mmoja tu wa reli,ambapo ni kweli Wajerumani walijenga zaidi reli...Unasahau Waingereza waliijenga Kenya ikawa modern country zaidi ya nchi yeyote East Africa nzima kwenye miundombinu mingine,not necessarily reli tu....

Hapa nasemea airports,Nairobi was the modern city,Mombasa port and other miundombinus.

Hawa walifanya hiki wale wakafanya kile,ila kwa kifupi Kenya ilikua modern and well built than anybody here.
Papara za nini wewe, kama ungenisoma vizuri ungekumbuka pale niliposema Wajerumani walikaa miaka 30 tuu Tanganyika wakati Waingereza walikaa miaka 75.

Na siyo tuu walijenga reli bali miji mingi tuu walisanifu wao, ikiwemo Dar (CBD na Kariakoo), Tanga, Bagamoyo, Tabora, Kigoma, Moshi, n.k (miaka 30 tuu). Huwezi fananisha miak 30 na 75.
Acha bangi wewe,uhuru haudaiwi London,ulikua unadaiwa kwenye world organization UNO,mkoloni na anakoloniwa wanaitwa kila mtu anajenga hoja zake na UNO kama independent board ndio inatoa maamuzi

Eti uende London,mkoloni anarudisha koloni bila kulazimishwa na external force?Acha ubwege wewe

Uingereza alilazimishwa kutupa uhuru sababu alishindwa hoja na mkataba wake wa koloni aliochukua kutoka kwa Mjerumani baada ya kumshinda WW1 ulikua umekaa vibaya,ulikua unasema ni koloni la kushika tu

Unajitia unajua sana ila naona u narukaruka tu....nimechoka kumbe hata ulikua hujui hearing program ya UNO ya decolonization worldwide..hujui lolote....Na kujifanya eti uhuru unadaiwa London ndio nimekuona mpumbavu zaidi,maana huwezi kwenda kwa oppressor kutaka kumnyang'anya koloni lake bila external force,eti ukaongee na kunegotiate nae....nonsense

UNO ndio ilisaidia decolonization,otherwise ingekua ni vita mwanzo mwisho
Hapo umedandia treni kwa mbele, nilikuwa namjibu Tony254 ila kwasababu unaonekana uko safarini (nigga, you must be trippin' on some shrooms), nitakuacha uendelee na safari yako.
 
so mkuu sie uhuru tuliupata uno na sio uengereza kama mleta mada alivosema?
vipi unakubali tuliupata bwerere pasipo kuupigania? refer machifu waliopigana mfn:isike mkwawa na nk
 
Papara za nini wewe, kama ungenisoma vizuri ungekumbuka pale niliposema Wajerumani walikaa miaka 30 tuu Tanganyika wakati Waingereza walikaa miaka 75.

Na siyo tuu walijenga reli bali miji mingi tuu walisanifu wao, ikiwemo Dar (CBD na Kariakoo), Tanga, Bagamoyo, Tabora, Kigoma, Moshi, n.k (miaka 30 tuu). Huwezi fananisha miak 30 na 75.

Hapo umedandia treni kwa mbele, nilikuwa namjibu Tony254 ila kwasababu unaonekana uko safarini (nigga, you must be trippin' on some shrooms), nitakuacha uendelee na safari yako.
Waingereza hawakukaa Tanzania kwa miaka 75. Mbona unavuta bangi kijana? Kufanya hesabu kidogo hivi imekushinda?
 
Sio papara wewe ndio hujui chochote

Nimefika hapo unaposema Kariakoo ilijengwa na Wajerumani nikaacha kusoma kabisa

Jitu zima lina mvi hadi matakoni linadanganya waziwazi....Kariakoo imejengwa mwaka 1974,juzi kabisa...Hadi jina Kariakoo limetokana na British "Carrier Corps"

Eti Mjerumani kajenga Kariakoo....muongo kama shetani...hata sisomi going forward....

Naomba usinijibu,lets close this conversation here,unakua liongo mno
Punguza dozi ya uyoga wewe, ni wapi nimesema walijenga? Nilisema walisanifu nikimaanisha wao ndio walioichora CBD na Kariakoo. Wewe utakuwa ni wakuja, kudhani kariakoo ilianza '74.
 
Sio papara wewe ndio hujui chochote

Nimefika hapo unaposema Kariakoo ilijengwa na Wajerumani nikaacha kusoma kabisa

Jitu zima lina mvi hadi matakoni linadanganya waziwazi....Kariakoo imejengwa mwaka 1974,juzi kabisa...Hadi jina Kariakoo limetokana na British "Carrier Corps"

Eti Mjerumani kajenga Kariakoo....muongo kama shetani...hata sisomi going forward....

Naomba usinijibu,lets close this conversation here,unakua liongo mno
Isitoshe hilo jitu linadanganya kuwa Waingereza walitawala Tanzania kwa miaka 75. Jamaa hata hajui historia yake.
 
Waingereza hawakukaa Tanzania kwa miaka 75. Mbona unavuta bangi kijana? Kufanya hesabu kidogo hivi imekushinda?
Na wewe miraa imeanza kukupeleka peleka, nioneshe niliposema Waingereza walikaa Tanzania miaka 75?
 
Papara za nini wewe, kama ungenisoma vizuri ungekumbuka pale niliposema Wajerumani walikaa miaka 30 tuu Tanganyika wakati Waingereza walikaa miaka 75.

Na siyo tuu walijenga reli bali miji mingi tuu walisanifu wao, ikiwemo Dar (CBD na Kariakoo), Tanga, Bagamoyo, Tabora, Kigoma, Moshi, n.k (miaka 30 tuu). Huwezi fananisha miak 30 na 75.

Hapo umedandia treni kwa mbele, nilikuwa namjibu Tony254 ila kwasababu unaonekana uko safarini (nigga, you must be trippin' on some shrooms), nitakuacha uendelee na safari yako.
Soma mahali ambapo nimehighlight na rangi nyekundu. Ndio ujue kwamba wewe ni wazimu. Hujui unachozungumzia.
 
Soma mahali ambapo nimehighlight na rangi nyekundu. Ndio ujue kwamba wewe ni wazimu. Hujui unachozungumzia.
Ndiyo matatizo ya kuwa na mihemeko haya, hapa nilikuwa namjibu mwenzako, ikiwa ni muendelezo kutoka posti #92, hii hapa chini.

Screenshot_2020-12-04 Kenya ilipigania uhuru wake Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu.png
 
Ule wa kupigana ilikua majorly ni kumpiga vita Mjerumani....na pia hatukufua dafu....

Sisi tulikua ni weaker society,mzungu alikua ni stronger na alikua na zana za kisasa,huwezi shindana na automatic weapons kwa marungu na mshale

Kwa resources na jamii tuliyokua nayo kipindi kile,tusingeweza kufua dafu kwa mzungu alipokuja,ndio maana machifu walikua wakishikwa na kuchinjwa mbele ya soko wananchi wakiangalia..

Koloni la Kenya lilikua ni protectorate colony of the British Empire.....ni kazi sana kupata uhuru kwa type hii ya koloni.

Ila Tanganyika mwaka 1947 ikawa ni United Nation Trust Territory under British administration,ikawa rahisi sana kwenda UN na kuomba kujitawala,British akanyang'anywa administration wakapewa wazawa wajifanyie-administration wenyewe...

Kenya ni tofauti,ilikua mali ya UK 100%!
maswali langu la msingi ni je tulipigana au la?
kama tulipigana what was the motive of the war?
je kwa maelezo yako apo juu utaungana nami kusema africa yote kutoa Ethiopia tulpata uhuru wa bwerere maana hatukuwashinda wazungu?
 
Back
Top Bottom