Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Wao wenyewe huko Kenya wanalia, hivi unadhani vita hivi ni mchezo?

'Cartels' wanacheza na uchumi wa kenya, halafu wewe unasema waTanzania wanalialia?

Subiri utakaposhuhudia 'full blast' ya 'tenderpreneurs' itakapohamia hapa ndipo utaelewa vizuri.

Ninajua nakujibu wewe mkuu 'Mkaruka', naelewa mara nyingi hatujawahi kuwa pembe tofauti kimtazamo kama leo.
Muhimu ni ushindani. Na kwenye dunia kama hii huwezi kukwepa ushindani kwasababu ndicho kichocheo cha ubora.

Mfano kwenye tenders, watanzania wangapi wanapata?

Ukiwapa wabongo, ndio hao kama kina Lugumi.

Tender nyingi hasa za ujenzi wachina wanachukua, sasa kuna tofauti yeyote hata wakipata wakenya?

Mfano: Kwenye banking sector, nini kinafanya banks kubwa na kongwe kama NMB, NBCna CRDB kushindwa kufungua matawi hata Kenya huko?

Huduma mbovu balaa.

Tanzania hapa kuna mabenki ya Kenya kibao: KCB, Equity,

Sisi tumebaki kulalamika tu. Ukimwajiri mbongo yaani Jumatatu anaumwa, Jumanne, kafiwa na bibi yake, Jumatano baba yake wa babu yake ana birthday, Alhamisi amepata dhatula mke wake anaumwa, Ijumaa akijitahidi atakuja kazini lakini ataomba ruhusa saa 4 asubuhi.

Wakati huo atakuwa analalamika sana mshahara hautoshi.

Wabongo tubadilike, hatuwezi kuishi hivi siku zote.

Tumekuwa kama Wazulu wa South Africa.

Unabagua kazi za kufanya, akizifanya mtu mwingine unaona wivu na chuki.
 
Watu wanashangilia kitu kitakachokuja kuwagharimu siku za usoni bila wao kujua! Majamaa yata lobby, yatafanya kila aina ya mbinu aggressively kushika usukani na tabia yao ya rushwa ile ikipandikizwa vizuri nchini tutaimba na kucheza nyimbo moja!

Barabara kampuni za kikenya! Madini kampuni za Kikenya! Supplies kampuni za Kikenya maana smartness wametuzidia na ni sababu kwao ku survive inahitaji akili nyingi sio mtori mtori kama sisi huku! Sehemu pekee tutakula nao sawa ni mashambani tu ndio watu watafaidi kutuma mizigo mpakani ikauzwe Kenya ila itaenda nao watakuwa wananunua Mashamba bongo na kulima wenyewe hapo ndio tutajua hatujui 😂😂😂!

Mkenya na mchagga tofauti yao ni shimboni shaffo tu tena bora wachaga ni ndugu zetu wale! Hao mahuni from Nai watakuja kutunyoosha ni swala la muda tu!
Mkuu mimi nimefanya kazi na wakenya.

Wana strength zao na weakness zao lakini siyo kwamba hatuwaezi.

Tuachane na hii inferiority complex.

Imagine, bongo fleva ime take over Kenya na kila wanavyojaribu kujinasua imeshindikana, kwanini tuwaogope kwa vitu vingine?

Ukiachana na uthubutu na kuongea kiingereza Wakenya hawana jipya.

Hivi kama tukiwaogopa wakenya, wanigeria tutawaweza?

Kama ni rushwa, hakuna mabingwa wa rushwa kama wachina na wahindi ila tunaishi nao humu humu.
 
Mkuu mimi nimefanya kazi na wakenya.

Wana strength zao na weakness zao lakini siyo kwamba hatuwaezi.

Tuachane na hii inferiority complex.

Imagine, bongo fleva ime take over Kenya na kila wanavyojaribu kujinasua imeshindikana, kwanini tuwaogope kwa vitu vingine?

Ukiachana na uthubutu na kuongea kiingereza Wakenya hawana jipya.

Hivi kama tukiwaogopa wakenya, wanigeria tutawaweza?

Kama ni rushwa, hakuna mabingwa wa rushwa kama wachina na wahindi ila tunaishi nao humu humu.
Wacha tukomae nao tuone
 
Swadakta kabisa mkuu, kinachoigharimu Tz yetu ni mifumo ya hovyo na ujanja² wa kiswahili. Mtoa mada + MATAGA wanahangaika sana kulinda legacy ya Jiwe, hawataki kusema ukweli kwamba uchumi wa Tz kudorora ni matokeo ya;
  • Sheria kandamizi
  • siasa chafu
  • ulimbukeni wa viongozi
  • visasi
  • wivu wa kitoto kwa wenzetu n.k n.k
Hamna cha ujasusi wala nini.
Nani kakwambia uchumi wa Tanzania umedorola kipindi cha JPM? JPM kaitoa hii Nchi shimoni na mumshukuru sana.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Wajamaa wana roho za utu tofauti na mabepari ambao wapo tayari kuua kwa sababu ya mali ambazo akina Bush Sr. wamekufa wameacha.

Wajamaa wanapambana kiungwana na kwa askili nyingi. Jaribu kulinganisha REPUBLICANS na DEMOCRATS kwa kule Marekani.
Utu hauhusiani na ujamaa. Ni roho ya mtu tu.

Ndio maana mnaojiita wajamaa hamkuona utu kwa Tundu Kussu, Azory Gwanda, Akwilini na wengine.

Labda kama cult personality ndio imekuwa ujamaa wa kisasa.
 
Asee ni vile mko mbali na systeam...hivo amuwez jua lolote...

Hakuna watu wanaopambana usiku na mchana kama Tz Intell!genc!!!!!(Tiss"""Mi"")
Mapambano yao kwa sehemu kubwa yame base kuifanya ccm kua madarakani na asilimia kidogo ndio wanawekeza kwenye ustawi wa nchi.
 
Kwani baada ya kumkataa Sylivia Mulinge kuna mtanzania anayeendesha VodaCom kama CEO au shida ni Mkenya ??

Ziara ya Rais Samia ni kubwa na imechukuliwa kwa ukubwa sana na wakenya ila kwetu sisi,

Muda wote ni wanyonge kazi yetu ni kujishuku shuku muda wote, kujiona wanyonge tutapigwa, hatujiwezi. Aisee

Huu ni ulemavu hakika.

Ningekuwa Rais nchi hii, ningegawa passport kwa kila mtu akazurule huko nje labda unyoronyoro ungetoka.

Mbongo muda wote ni kulalamika na kuhisihisi kujiona anaonewa muda wote.

This is too much.
Vodacom haijawahi kuendeshwa na Mtanzanzia ila watu wanaona ni bora kuliko alivyopewa Mkenya !
Tatizo kubwa nadhan ni exposure pamoja na kujiona wanyonge ,
tumebaki kulalamika mama asiruhusu work permit , badala ya kujiuliza na sisi tutanufaika vipi na ujio wao hapa kwetu.
 
Ni mpumbavu tu anayeweza kuamini Vodacom Tanzania inaweza kuondoshwa katika soko la Tanzania na mkenya.
Kwanza VodaCom ni kampuni la kibeberu na limeletwa nchi hii na Rostam Aziz.

Hakuna tofauti yeyote kati ya SafariCom na VodaCom wao ndio wataamua nini wanafanya.
 
Vodacom haijawahi kuendeshwa na Mtanzanzia ila watu wanaona ni bora kuliko alivyopewa Mkenya !
Tatizo kubwa nadhan ni exposure pamoja na kujiona wanyonge ,
tumebaki kulalamika mama asiruhusu work permit , badala ya kujiuliza na sisi tutanufaika vipi na ujio wao hapa kwetu.
Kuna wengine hata hiyo Work permit hawajui ni kitu gani.

Ilimradi ni kubishana tu.
 
Sisi tumebaki kulalamika tu. Ukimwajiri mbongo yaani Jumatatu anaumwa, Jumanne, kafiwa na bibi yake, Jumatano baba yake wa babu yake ana birthday, Alhamisi amepata dhatula mke wake anaumwa, Ijumaa akijitahidi atakuja kazini lakini ataomba ruhusa saa 4 asubuhi.
Mimi huwa sielewani kabisa na wewe humu JF lakini kwa point hii ninakusifia. Umeandika point ya maana sana.
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Mkuu, je, unaamini kuwa michezo ya ujasusi wa kiuchumi huwa inafanyika sana hapa duniani?
 
Kwenye work permit mama asijaribu,huku tayari wakenya wengi sana kwenye mahoteri ya kitalii kuliko watz na sisi hawawezi kutupa ajira huko.
Ni lugha za kisiasa tu.
Tanzania na Kenya ni kama Simba na Yanga
 
Back
Top Bottom