Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Mwaka juzi wa 2019 Mwezi November, JF Member My Son drink water aliwahi kusema kwamba "Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania, nashukuru Mungu tena dakika za mwisho TISS walistukia mchezo vinginevyo VodaCom nayo ilikuwa inakufa na ingekuja kufufukia Kenya"
==========
==========
Habari zenu waungwana wa jamiiforums

FRIDAY SEPTEMBER 28, 2018: Vodacom Tanzania said on Friday the government had denied its incoming chief executive officer, a Kenyan, a work permit, and it would have to restart the recruitment process.

In April, Vodacom Tanzania named Sylvia Mulinge, at the time head of business at Kenya's biggest telecoms operator Safaricom to the post. She was meant to take up her position on June 1.
==========
==========
Kwani kama mtu alikuchangia USD 200 katika maandalizi ya harusi yako ni lazima na wewe umpe kiasi hicho hicho cha pesa yeye atakapokuwa anajiandaa kuoa/kuolewa?

Kwani kitendo cha Rais Uhuru Kenyatta kufuta work permits pamoja na Business Visas ni lazima kiwe nipe nikupe (quid pro quo) kwa taifa kubwa la Tanzania? Kuna ulazima wowote wa Tanzania nayo kufuta vibali hivyo kwa raia wa Kenya?
==========
==========
Baada ya Rais Kenyatta kufuta documents kwa wafanyakazi wa Tanzania ndio ninakumbuka maneno yaliyopo humu humu JF ya member mmoja anayetumia jina la My Son drink water kwamba;

"65% ya viwanda vilivyokufa Tanzania vilikuja kufufukia Kenya, tafsiri yake ni kwamba, Usalama wa Taifa wa Kenya, KNIA walifanya yao huku TISS yetu ikiwa imelala, na Kiwanda cha mwisho kuhamia Kenya ni cha General Tyres, yaani ajira zinakufa Tanzania kisha zinawafufukia Wakenya. Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania, nashukuru Mungu tena dakika za mwisho TISS walistukia mchezo vinginevyo VodaCom nayo ilikuwa inakufa na ingekuja kufufukia Kenya"

SWALI: Tutegemee "Sylvia Mulinge" wa Safaricom kurudi kuwa CEO wa Vodacom endapo Tanzania itafuta work permits pamoja na Business Visas kwa raia wa Kenya?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hii tabia ya Wabongo kulialia lazima ifike mwisho.
 
Ujamaa ndio asili ya uvivu wetu Kenya ubepari umewalea kwenye kupambana
Wajamaa wana roho za utu tofauti na mabepari ambao wapo tayari kuua kwa sababu ya mali ambazo akina Bush Sr. wamekufa wameacha.

Wajamaa wanapambana kiungwana na kwa askili nyingi. Jaribu kulinganisha REPUBLICANS na DEMOCRATS kwa kule Marekani.
 
Wajamaa wana roho za utu tofauti na mabepari ambao wapo tayari kuua kwa sababu ya mali ambazo akina Bush Sr. wamekufa wameacha.

Wajamaa wanapambana kiungwana na kwa askili nyingi. Jaribu kulinganisha REPUBLICANS na DEMOCRATS kwa kule Marekani.
Ujamaa ni umasikini, ujamaa ni chuki dhidi ya waliofanikiwa,ujamaa ni uvivu.
Asiyefanya Kazi na asile.Kama unatengenezewa mazingira ya kufanya kazi kwann usifanye Kazi.Lima tikiti,nyanya,hoho,bamia, muhogo soko Mkenya anafata shamba kwa bei poa kwann ukae unasubiri nn.Maji,ardhi,soko vyote vipo ni nguvu yako tu.
 
Swadakta kabisa mkuu, kinachoigharimu Tz yetu ni mifumo ya hovyo na ujanja² wa kiswahili. Mtoa mada + MATAGA wanahangaika sana kulinda legacy ya Jiwe, hawataki kusema ukweli kwamba uchumi wa Tz kudorora ni matokeo ya;
  • Sheria kandamizi
  • siasa chafu
  • ulimbukeni wa viongozi
  • visasi
  • wivu wa kitoto kwa wenzetu n.k n.k
Hamna cha ujasusi wala nini.
Acha waje wale wanachama ambao wanajifanya nchi ni yao pekee uone watakavyokucharukia kisa UKWELI HUU
 
Na
Wajamaa wana roho za utu tofauti na mabepari ambao wapo tayari kuua kwa sababu ya mali ambazo akina Bush Sr. wamekufa wameacha.

Wajamaa wanapambana kiungwana na kwa askili nyingi. Jaribu kulinganisha REPUBLICANS na DEMOCRATS kwa kule Marekani.
Ni kweli kiongoz, NDIO MAANA MAJAMAA YANATEKA WATU,MANAFIKI,MANYANG'ANYI,YANAUA WAANDISHI WA HABARI,YAKIFA YANAZIKWA BILA JENEZA,YANAPORA PESA KWENYE MIFUKO YA HIFADHI NA FAUKA YA YOTE YANAHAKIKISHA ELIMU INAYOTOLEWA NI HAFIFU ILI YATAWALE MAISHA. KIBOKO CHA MAJAMAA NI MUNGU. ANACHOMOA MMOJA MMOJA
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Huwezi kuwakwepa kwa njia yeyote kwenye ustawi wa taifa na pia kiulinzi na usalama nchi yeyote vyombo vya ulinzi kama Tiss ndiyo wenye jukumu la kuishauri selikari ktk kuenda mbele iwe kwa njia hata ya kufanya ujasusi kwenye nchi nyingine ukiona nchi inafeli ktk uchumi,kisiasa na ulinzi ujue kuna tatizo ktk chombo kama tiss
 
Kufanyaje?
Asee ni vile mko mbali na systeam...hivo amuwez jua lolote...

Hakuna watu wanaopambana usiku na mchana kama Tz Intell!genc!!!!!(Tiss"""Mi"")
 
Ni mpumbavu tu anayeweza kuamini Vodacom Tanzania inaweza kuondoshwa katika soko la Tanzania na mkenya.
 
Ni mpumbavu tu anayeweza kuamini Vodacom Tanzania inaweza kuondoshwa katika soko la Tanzania na mkenya.
Ulivyoliweka hili ni kama wewe ndiye mmiliki wa 'Vodacom', hebu tueleze ujuwayo wewe, kabla ya kuwaita wengine kuwa ni "wapumbavu".

Kwani huoni wewe unaweza ukawa mpumbavu zaidi ya hao wengine?
 
Kwani baada ya kumkataa Sylivia Mulinge kuna mtanzania anayeendesha VodaCom kama CEO au shida ni Mkenya ??

Ziara ya Rais Samia ni kubwa na imechukuliwa kwa ukubwa sana na wakenya ila kwetu sisi,

Muda wote ni wanyonge kazi yetu ni kujishuku shuku muda wote, kujiona wanyonge tutapigwa, hatujiwezi. Aisee

Huu ni ulemavu hakika.

Ningekuwa Rais nchi hii, ningegawa passport kwa kila mtu akazurule huko nje labda unyoronyoro ungetoka.

Mbongo muda wote ni kulalamika na kuhisihisi kujiona anaonewa muda wote.

This is too much.
Wao wenyewe huko Kenya wanalia, hivi unadhani vita hivi ni mchezo?

'Cartels' wanacheza na uchumi wa kenya, halafu wewe unasema waTanzania wanalialia?

Subiri utakaposhuhudia 'full blast' ya 'tenderpreneurs' itakapohamia hapa ndipo utaelewa vizuri.

Ninajua nakujibu wewe mkuu 'Mkaruka', naelewa mara nyingi hatujawahi kuwa pembe tofauti kimtazamo kama leo.
 
Wao wenyewe huko Kenya wanalia, hivi unadhani vita hivi ni mchezo?

'Cartels' wanacheza na uchumi wa kenya, halafu wewe unasema waTanzania wanalialia?

Subiri utakaposhuhudia 'full blast' ya 'tenderpreneurs' itakapohamia hapa ndipo utaelewa vizuri.

Ninajua nakujibu wewe mkuu 'Mkaruka', naelewa mara nyingi hatujawahi kuwa pembe tofauti kimtazamo kama leo.
Watu wanashangilia kitu kitakachokuja kuwagharimu siku za usoni bila wao kujua! Majamaa yata lobby, yatafanya kila aina ya mbinu aggressively kushika usukani na tabia yao ya rushwa ile ikipandikizwa vizuri nchini tutaimba na kucheza nyimbo moja!

Barabara kampuni za kikenya! Madini kampuni za Kikenya! Supplies kampuni za Kikenya maana smartness wametuzidia na ni sababu kwao ku survive inahitaji akili nyingi sio mtori mtori kama sisi huku! Sehemu pekee tutakula nao sawa ni mashambani tu ndio watu watafaidi kutuma mizigo mpakani ikauzwe Kenya ila itaenda nao watakuwa wananunua Mashamba bongo na kulima wenyewe hapo ndio tutajua hatujui 😂😂😂!

Mkenya na mchagga tofauti yao ni shimboni shaffo tu tena bora wachaga ni ndugu zetu wale! Hao mahuni from Nai watakuja kutunyoosha ni swala la muda tu!
 
Back
Top Bottom