Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Unajua wewe jamaa kuna vitu vingi sana hujui ila unajikuta mjuaji sana. Suala la kufa na kustawi inategemea mazingira peke yake? You mean people can't influence things, you mean hata hizo hujuma za USA kwa China ni mazingira ya China ndio yanaua Huawei, hakuna external influences.
Mahn, shut your mouth sumtyms and learn
Huyo jamaa Jokakuu anaendekeza ubishi usio na tija yoyote kwa taifa.
 
Unaona sasa? Unataka kuanza kusema Wakenya wanazungumza Kiswahili kizuri kuzidi sisi Watanzania.

..hapana.

..kwenye kiswahili nalinganisha matumizi ya lugha yetu wakati nakua; niko shuleni, na wakati huu wa wazalendo uchwara.

..nayaona mapungufu ya wazi kabisa ktk uandishi wa Kiswahili ktk zama hizi, jambo ambalo lilikuwa la nadra miaka ya nyuma.

..kwa mfano,.sasa hivi unaweza kukuta muandishi wa gazeti amekosea kwa kutumia " ri " mahali ambapo alitakiwa atumie " li. " Kosa kama hilo lilikuwa haliwezi kufikirika miaka yetu wakati tunakua.

..Pia ukisikiliza matumizi ya lugha wakati wa mijadala yetu unaona kuna mapungufu makubwa. Uwezo wa kujenga hoja umepungua. Pia wengi hawana maarifa na lugha ya Kiswahili, hawana uwezo wa kutumia maneno sahihi kujenga hoja zao.

..Jambo lingine ni tabia ya kujisomea vitabu imepungua sana miongoni mwa wasomi wetu. Kama tunataka kuimudu lugha yetu lazima tujenge utamaduni wa kusoma vitabu vingi vya Kiswahili kwa vijana wetu na watu wazima pia.

..Labda niulize swali: Je, mwanafunzi wa Kitanzania anaweza kusoma vitabu 50 vya hadithi vya Kiswahili kati ya darasa la kwanza na darasa la saba? Je, mwanafunzi wa darasa la saba anaweza kuandika hadithi ya Kiswahili lenye maneno 2000 au yenye kurasa 5?

..Tunaikuza vipi lugha yetu bila kuandika na kusoma vitabu vingi vya aina maudhui mbalimbali? Tutaikuza vipi lugha yetu bila kuwasuka na kuwaandaa vijana wetu kuwa washairi, wanamuziki, wana tamthilia, etc etc?

..Naiangalia Tanzania mahali ilipo na mahali ambapo naamini tunaweza kufika.

Cc Nguruvi3, Chige, Richard
 
Je, mwanafunzi wa darasa la saba anaweza kuandika hadithi ya Kiswahili lenye maneno 2000 au yenye kurasa 5?
Ninafikiri utunzi wa hadithi ni kipaji binafsi cha mtu na si kila mwanafunzi anaweza hili.
 
..Labda niulize swali: Je, mwanafunzi wa Kitanzania anaweza kusoma vitabu 50 vya hadithi vya Kiswahili kati ya darasa la kwanza na darasa la saba?
Hili linahitaji juhudi za shule pamoja na wazazi na si kufikiri kwamba serikali itaweza kufanya kila jambo kwa nguvu zake bila msaada wa wananchi.
 
..Jambo lingine ni tabia ya kujisomea vitabu imepungua sana miongoni mwa wasomi wetu. Kama tunataka kuimudu lugha yetu lazima tujenge utamaduni wa kusoma vitabu vingi vya Kiswahili kwa vijana wetu na watu wazima pia.
Kwa hili ninakubaliana na wewe 100%
 
Ninafikiri utunzi wa hadithi ni kipaji binafsi cha mtu na si kila mwanafunzi anaweza hili.

..mwanafunzi baada ya kusoma mashairi, pamoja na hadithi za maudhui mbalimbali, anatakiwa ajaribiwe kwa kile alichojifunza.

..kwa mtindo huo ndio tutapata waandishi wa vitabu vya hadithi, waandika mashairi, etc etc
 
Alichokisema JokaKuu ni kuwa;

"miaka 25 ya kuwa wanachama wa eac ninaamini ilikuwa inatosha kabisa kuwaandaa wananchi wetu kuweza kuishi popote"

Kwa hiyo kinachojadiliwa hapa ni watu na sio makampuni.
Sawasawa, lakini makampuni si yana watu au yana akina nani? Kuandaa watu ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuwa na makampuni yenye uwezo wa kuwekeza huko Kenya...I thought so
 
Ninafikiri utunzi wa hadithi ni kipaji binafsi cha mtu na si kila mwanafunzi anaweza hili.
Anachosema hapa ni kusoma kama tabia ambayo inajengwa ili kukuza ufanisi wa lugha...Kumbuka ndiyo maana tuna kiswahili fasihi na ile na structure kumsaidia mtu kujua lugha vizuri ambayo ni structured...Ila colloquial ndizo mpaka ukutane na wanaoiishi hiyo lugha
 
Anachosema hapa ni kusoma kama tabia ambayo inajengwa ili kukuza ufanisi wa lugha...Kumbuka ndiyo maana tuna kiswahili fasihi na ile na structure kumsaidia mtu kujua lugha vizuri ambayo ni structured...Ila colloquial ndizo mpaka ukutane na wanaoiishi hiyo lugha
Kwenye suala la kuandika na kusoma vitabu mara kwa mara, sina shida na mtu katika hili kwa maana hata mimi kila siku ni lazima nisome makala online pamoja na hardcopies chache ninazo hapa ninapokaa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ndugu yangu JokaKuu,

Ahsante sana kwa kunikaribisha kwenye mada hii! Kwa sasa nitachangia kidogo kwenye hoja ya Kiswahili na baadae nitachangia kwenye mada kuu ya economic espionage!!

Kwanza nianze na hoja aliyokujibu Infantry Soldier aliposema "Ninafikiri utunzi wa hadithi ni kipaji binafsi cha mtu na si kila mwanafunzi anaweza hili."

Kwa kiasi fulani, nakubaliana na yeye lakini kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe JK!

Case Study ni mimi mwenyewe!!

Siku moja nilikuwa na wana-Bongo Movie, na mjadala ulihusu uandishi wa script! Sasa mimi bila kuichunguza hadhira, nikaropoka kwamba:-

"...kwa Tanzania, ambako hakuna formal film making and screenwriting training, uandishi wa script unategemea sana kipaji! Sasa basi, kujua una kipaji, jiulize lini ulianza kuandika hadithi za kawaida! Kama unafahamu kabisa hadi unamaliza Kidato VI hukuwahi kuandika hata hadithi fupi, my friend, wewe huna kipaji kwa sababu kipaji kinaanza kuonekana mapema sana." Mwisho wa kujinukuu!

Wakuu JK na IS, baada ya kuisoma hadhira nikagundua wengi nilikuwa nimewakera sana, kwa sababu ilionesha wazi wengi walianza kuandika story baada ya kuingia kwenye tasnia ya filamu, kwahiyo kuwaambia hawana kipaji ilikuwa ni kama tusi kwao!!

Nadhani nilikuwa mbinafsi kwa kujichukulia mwenyewe kama case study kwa sababu, nikiwa Kidato cha Pili, nilishaanza kufanya attempt ya kwanza ya kuchapishiwa hadithi yangu, kwahiyo nikaamini mtu mwenye kipaji angeanza kuandika hadithi wakati akiwa na umri mdogo kama nilivyokuwa mimi!!

Inawezekana sikuwa sahihi, ingawaje hadi hivi sasa hivyo ndivyo ninavyoamini... na kwahiyo inawezekana hadi sasa sipo sahihi!

Lakini nirudi niliwazaje kuandikka hadithi na kutaka kuichapa kitabu wakati nipo 16!

Hapo ndipo ninaposema nakubaliana na wewe JK kwa kiasi kikubwa huku nikikubaliana na IS kwa kiasi fulani! WHY?

Mimi hadi nafikia Darasa la IV, vitabu vya simulizi mbalimbali pale shuleni nilikuwa nimemaliza karibu vyote, manake ilikuwa muda wa kutoka kwenda home, mimi naenda maktaba, na Ijumaa naazima kitabu/vitabu kwa ajili ya weekend!

Sikumbuki ni nani aliniambia kuhusu Tanganyika Library, basi baada ya kuifahamu, ikawa kazi ya kumsumbua sister anipeleke maktaba!

Hadi namaliza Form I, vile vitabu kama Kuli, Shida na takataka zingine hadi Hawala ya Fedha nilikuwa nimesoma vyote ingawaje mtaala ulikuwa unanitaka nivisome Kidato cha III!

Kimsingi, nilikuwa nasoma hadi vitabu vya ushairi ambavyo watu walikuwa wanajionea taabu tu kuvisoma, na wale waliovisoma ni kwa sababu tu hawakuwa na option... watu wa masomo ya arts!

Kufika Kidato III ndipo nikakutana na tabia yetu halisi Watanzania!

Kwavile nilikuwa nasoma sayansi, with no chance ya comb za arts kwa sababu tulikuwa hatusomi history, basi majority ya Washikaji pale class hawakuwa wasomaji wa vitabu!! Wengi walikuwa niwasimulie ili eti wajibu English/Swahili Literature kwa kusimuliwa!

Sasa kwa kuangalia mlolongo huo, hivi nitasema nilianza kuandika hadithi nikiwa Kidato cha Pili kwa sababu nilikuwa/nina kipaji au kwa sababu nilisha-develop tabia ya kusoma, na hivyo nami kuvutiwa kutaka kuandika?

My Inspirational Writer alikuwa Marehemu Elvis Musiba, ambae hadi nafika Form II nilikuwa nimesoma vitabu vyake vyote vya Willy Gamba kabla ya kuhamia kwa Mzee Mtobwa na vitabu vyake vya Joram Kiango!!

Kwahiyo ingawaje IS anasema kuandika hadithi kunahitaji kipaji, katu kipaji hicho hakitakuja kuonekana kama mwenye kipaji chake hana tabia ya kusoma na hatimae ku-develop kiu ya yeye kutamani kuandika kama yale anayosoma!!!

Wakati nipo chuo, kazi ikawa kwenye "dissertation"!

Kwavile binafsi nilisha-develop tabia ya kusoma na kuandika, nakumbuka wakati wenzangu wanahangaika na proposal ya kwanza TU, mimi nilikuwa nimeshaandika 2 na kuzipiga chini.

Si kwamba nilikuwa a bright student, HELL NO... not even close to a bright students circle bali ni kwa sababu kusuoma na kuandika kwangu haikuwa tatizo kama ilivyokuwa kwa wenzangu!!

Na hili la kusoma ndio changamoto yetu kubwa Watanzania hususani wa kipindi hiki, na ndio maana watu kama akina chige ambao tukianza tu kuandika neno la kwanza, maneno mengine yanakuja yenyewe tu bila hata kufikiria na hatimae kujikuta tumeandika thread reefu; huwa tunapata taabu sana hapa JF kwa sababu kitakachofuata hapo ni malalamiko na kejeli kutoka kwa watu wasiopenda kusoma!

Na usipopenda kusoma, itakuwa ngumu sana kuwa na ufanisi wa lugha kwa sababu, kila unaposoma, ndipo unapokuja kubaini makosa uliyokuwa unayafanya hapo kabla kutokana na matumizi ya lugha kimazoea!!!
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Kuna factors nyingi zaid ya hizo. Mazingira ya Tanzania kibiashara bado siyo mabaya kama unavyotaka kudai kwa kulinganisha na Kenya. Kwani Kenya hawilipi kodi? Au hawalazimiki kufuata sheria zilizopo?
 
Kwahiyo ingawaje IS anasema kuandika hadithi kunahitaji kipaji, katu kipaji hicho hakitakuja kuonekana kama mwenye kipaji chake hana tabia ya kusoma na hatimae ku-develop kiu ya yeye kutamani kuandika kama yale anayosoma!!!
"Hard work beats talent when talent doesn't work hard"
 
Back
Top Bottom