Ndugu yangu
JokaKuu,
Ahsante sana kwa kunikaribisha kwenye mada hii! Kwa sasa nitachangia kidogo kwenye hoja ya Kiswahili na baadae nitachangia kwenye mada kuu ya economic espionage!!
Kwanza nianze na hoja aliyokujibu
Infantry Soldier aliposema "Ninafikiri utunzi wa hadithi ni kipaji binafsi cha mtu na si kila mwanafunzi anaweza hili."
Kwa kiasi fulani, nakubaliana na yeye lakini kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe JK!
Case Study ni mimi mwenyewe!!
Siku moja nilikuwa na wana-Bongo Movie, na mjadala ulihusu uandishi wa script! Sasa mimi bila kuichunguza hadhira, nikaropoka kwamba:-
"...kwa Tanzania, ambako hakuna formal film making and screenwriting training, uandishi wa script unategemea sana kipaji! Sasa basi, kujua una kipaji, jiulize lini ulianza kuandika hadithi za kawaida! Kama unafahamu kabisa hadi unamaliza Kidato VI hukuwahi kuandika hata hadithi fupi, my friend, wewe huna kipaji kwa sababu kipaji kinaanza kuonekana mapema sana." Mwisho wa kujinukuu!
Wakuu JK na IS, baada ya kuisoma hadhira nikagundua wengi nilikuwa nimewakera sana, kwa sababu ilionesha wazi wengi walianza kuandika story baada ya kuingia kwenye tasnia ya filamu, kwahiyo kuwaambia hawana kipaji ilikuwa ni kama tusi kwao!!
Nadhani nilikuwa mbinafsi kwa kujichukulia mwenyewe kama case study kwa sababu, nikiwa Kidato cha Pili, nilishaanza kufanya attempt ya kwanza ya kuchapishiwa hadithi yangu, kwahiyo nikaamini mtu mwenye kipaji angeanza kuandika hadithi wakati akiwa na umri mdogo kama nilivyokuwa mimi!!
Inawezekana sikuwa sahihi, ingawaje hadi hivi sasa hivyo ndivyo ninavyoamini... na kwahiyo inawezekana hadi sasa sipo sahihi!
Lakini nirudi niliwazaje kuandikka hadithi na kutaka kuichapa kitabu wakati nipo 16!
Hapo ndipo ninaposema nakubaliana na wewe JK kwa kiasi kikubwa huku nikikubaliana na IS kwa kiasi fulani! WHY?
Mimi hadi nafikia Darasa la IV, vitabu vya simulizi mbalimbali pale shuleni nilikuwa nimemaliza karibu vyote, manake ilikuwa muda wa kutoka kwenda home, mimi naenda maktaba, na Ijumaa naazima kitabu/vitabu kwa ajili ya weekend!
Sikumbuki ni nani aliniambia kuhusu Tanganyika Library, basi baada ya kuifahamu, ikawa kazi ya kumsumbua sister anipeleke maktaba!
Hadi namaliza Form I, vile vitabu kama Kuli, Shida na takataka zingine hadi Hawala ya Fedha nilikuwa nimesoma vyote ingawaje mtaala ulikuwa unanitaka nivisome Kidato cha III!
Kimsingi, nilikuwa nasoma hadi vitabu vya ushairi ambavyo watu walikuwa wanajionea taabu tu kuvisoma, na wale waliovisoma ni kwa sababu tu hawakuwa na option... watu wa masomo ya arts!
Kufika Kidato III ndipo nikakutana na tabia yetu halisi Watanzania!
Kwavile nilikuwa nasoma sayansi, with no chance ya comb za arts kwa sababu tulikuwa hatusomi history, basi majority ya Washikaji pale class hawakuwa wasomaji wa vitabu!! Wengi walikuwa niwasimulie ili eti wajibu English/Swahili Literature kwa kusimuliwa!
Sasa kwa kuangalia mlolongo huo, hivi nitasema nilianza kuandika hadithi nikiwa Kidato cha Pili kwa sababu nilikuwa/nina kipaji au kwa sababu nilisha-develop tabia ya kusoma, na hivyo nami kuvutiwa kutaka kuandika?
My Inspirational Writer alikuwa Marehemu Elvis Musiba, ambae hadi nafika Form II nilikuwa nimesoma vitabu vyake vyote vya Willy Gamba kabla ya kuhamia kwa Mzee Mtobwa na vitabu vyake vya Joram Kiango!!
Kwahiyo ingawaje IS anasema kuandika hadithi kunahitaji kipaji, katu kipaji hicho hakitakuja kuonekana kama mwenye kipaji chake hana tabia ya kusoma na hatimae ku-develop kiu ya yeye kutamani kuandika kama yale anayosoma!!!
Wakati nipo chuo, kazi ikawa kwenye "dissertation"!
Kwavile binafsi nilisha-develop tabia ya kusoma na kuandika, nakumbuka wakati wenzangu wanahangaika na proposal ya kwanza TU, mimi nilikuwa nimeshaandika 2 na kuzipiga chini.
Si kwamba nilikuwa a bright student, HELL NO... not even close to a bright students circle bali ni kwa sababu kusuoma na kuandika kwangu haikuwa tatizo kama ilivyokuwa kwa wenzangu!!
Na hili la kusoma ndio changamoto yetu kubwa Watanzania hususani wa kipindi hiki, na ndio maana watu kama akina chige ambao tukianza tu kuandika neno la kwanza, maneno mengine yanakuja yenyewe tu bila hata kufikiria na hatimae kujikuta tumeandika thread reefu; huwa tunapata taabu sana hapa JF kwa sababu kitakachofuata hapo ni malalamiko na kejeli kutoka kwa watu wasiopenda kusoma!
Na usipopenda kusoma, itakuwa ngumu sana kuwa na ufanisi wa lugha kwa sababu, kila unaposoma, ndipo unapokuja kubaini makosa uliyokuwa unayafanya hapo kabla kutokana na matumizi ya lugha kimazoea!!!