Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

Njoo uwe mwenzetu huku Kenya
 
..Kenya walikuwa wametuacha kimaendeleo hata kabla ya vita vya Kagera.

..kumbuka Tanzania tulivyohangaika kuanzisha viwanda mara baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika kwasababu tulikuwa tukitegemea bidhaa toka Kenya.
Mkapa alipiga kazi tukaiacha Kenya kwa GDP,akaingia kibaki kule,mchumi,akafanya alofanya tumeachwa mpaka kesho
 
Mkapa alipiga kazi tukaiacha Kenya kwa GDP,akaingia kibaki kule,mchumi,akafanya alofanya tumeachwa mpaka kesho

..Tujitahidi kuboresha kilimo na ufugaji tutakuwa ktk nafasi nzuri ya ushindani.

..Kenya wanazalisha maziwa mengi kuliko Tanzania wakati sisi tuna ng'ombe wengi kuliko wao.
 
Tulikua na nafasi ya kuendelea kutumia English kama Lugha ya kufundishia. Leo hii kingekua kimetufungulia fursa nyingi sana nje. Wa Tz wapo wengi nje lakini wapo kimya sana tofauti na wenzetu wakenya au ugandans ambao wanaweza kujieleza vizuri kwa Lugha hiyo.
Watawala wameona Kiswahili kiendelee kutumika kufundishia mashuleni lakini watoto wao wanasoma English meadium schools na International schools
 
Yaani hapo kwakweli hata mie sitaacha kuwalaumu, nakumbuka tunaanza darasa la kwanza tuna rafudhi ya kiruga lakini tukafundishwa na kuelewa vizuri tena mwezi tu, kwanini asingekiacha tukaanza nacho tukiwa bado vichwa vinanasa vyema? Baba kwa hapo mmm hapana kwa watoto wamafukara inatesa sana. Wahindi wenyewe tupo nao humu halafu eti Kiswahili hawakijui ila mzungu au mchina akija siku 2 tu tunaongea naye kiswahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Swala la uchumi baina ya nchi za africa ya mashariki kwa kiasi kikubwa linamizizi ya ukoloni. Tutambue tu nchi yetu kwanza ilitawaliwa na mjerumani na baadae mwingereza km mwangalizi wa muda.

Kupitia wakoloni wa kiingereza kenya hasa nairobi ilijengwa sana na kufanywa km ndio makao makuu ya Africa mashariki huku tanganyika ikibaki km mashamba tu kwanza haikuwa mali ya mwingereza hivyo alijihusisha sehemu ndogo kwenye uchumi. (Gap la kwanza la uchumi likatokea hapo)

Maisha baada ya uhuru kwa nchi zote mbili pia yalikuwa na miundo tofauti sana hasa tanganyika tuliamua kufuata mfumo wa kijamaa na kenya wao waliendelea na ubepari. Mwanzoni ufumo wa kijamaa kwa tanganyika ulionekani mfumo sahihi sana maan uliweza kukuza uchumi kwa speed hadi miaka ya 77 nchi ilianza kujikuta kweny matatizo ya vita na kudondoka kwa ujamaa duniani hali hii ilipelekea nchi za kijamaa tulizokuwa tunazitegemea kusitisha misaada hali ikawa mbaya sana hivyo tukageukia ubepari kwa mashart magumu sana tukapewa mikopo.
(Gap la pili likatokea hapo)

Kufikia miaka ya 1995 nchi yetu ilikuwa hoi bin taaban kiuchumi inshort ilifilisika na ikaorodheshwa miongoni mwa nchi masikini zenye mzigo mkubwa wa madeni
Tukasamehewa na kuanza upya tena.

Baada ya kurudia ubepari tena toka uhuru jitihada mbalimbali zimefanywa na viongozi kwa kadri walivyoweza kuunyanyua uchumi tena ambao ulikuwa umeshakufaaa.

Hivi tunavyoongea tz ni miongoni mwa nchi 10 zenye uchumi mkubwa afrika kati ya nchi 54 sisi tukiwa namba 9 huku 8 akiwa Ethiopian na 7 kenya. U can imagine from down huko to top ten.

Maana yk ni kuwa tz inaendelea kwa speed sana kuliko kenya maan kenya hawajawahi kupata misukosuko ya kiuchumi km tz wala hawajawah kubadili mifumo ya uchumi ya nchi yao toka uhuru.
Achilia mbali wao walirithi nchi ikiwa na kila kitu teyar miundombinu ya kutosha, viwanda, man labour ya kutosha sisi hivyo vyote tulivisikia kwenye bomba na ilitubidi tuvijenge wenyewe maan tulichorithi ni reli na barabara ndogo ya rami.

Bongo kazi inapigwa sana ingawa pia baadhi ya viongozi wetu wanaturudisha nyuma ila kazi imepigwa haswa..
 
Umedadavua kisomi! Atleast naanza kuelewa wapi tulijikwaa
 
Umerenga mkuki pahala pake. Kukazia ni uongozi bora au siasa safi imekosekana. Waliopo wanaimizana kula kwa urefu wa kamba zao huku wakiongeza kamba ziwe ndefu wale zaidi. Mfano halisi ni uongezaji idadi ya wajumbe kwenye Nec yao ccm, kuna ulazima gani!
 
Still Kenya inategemea chakula kutoka tz kwa silimia nyingi sana
 
Kagera War (1978-1979)

Waakanzia kutupiga gape hapo.
Kisa vita ya kidini (Mkatoliki Nyerere vs Muislamu Amin)
Hapo umepuyanga yaani kabla ya vita gap lilikuwa kubwa sana kushinda sasa
 
Halafu tunawalisha
 
Umemaliza yote mkuu
 
..Tujitahidi kuboresha kilimo na ufugaji tutakuwa ktk nafasi nzuri ya ushindani.

..Kenya wanazalisha maziwa mengi kuliko Tanzania wakati sisi tuna ng'ombe wengi kuliko wao.
Siku hizi ndiyo tunarasimisha shughuli,huko nyuma palikua na wakulima na wafanyakazi,maana kilimo si kazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…