Kenya kama Malawi, wapanga kupeleka vibarua wa Mashamba ya Israel kwa ujira wa Ksh. 228,000 (4,000,000Tsh)

Kenya kama Malawi, wapanga kupeleka vibarua wa Mashamba ya Israel kwa ujira wa Ksh. 228,000 (4,000,000Tsh)

Wewe nae ni mbuzi tuu, kwenye Mpango wa Saudia na UAE Kuna watu wa fani mbalimbali wakiwamo hao uliowakariri.

Mwisho Samia hawezi wauza watu wake kisa Pesa.Kati ya maslahi ya kibiashara na utu,siku zote ccm inasimama upande wa utu.
Sasa ndugu yangu ya nini kunitukana kuniita mbuzi? Kuna sehemu niliyokukejeli?
Asante jioni njema
 
Mimi nafikiri hizi ni fursa kwa Vijana Afrika kupata Ajira!
Ni kuzichangamkia!
Kuliko wakikaa huku Afrika ambako mwisho wengine wanajiingiza kwenye vitendo vya ukabaji bora waende huko!
Mtakapoanza kunyanyaswa huko msije kusema hamkuambiwa.

Wenzako wanakimbia wewe unaenda tena mtu mweusi
 
Utumwa ni maamuzi ya MTU ili mtu akufanye mtumwa anaanza kucheza na hisia zako Kwa kuamini bila kufanya kazi ngumu utakufa njaa.


Huwa nasema Kama ilivyo ccm inatumia simba na yanga kuitawala nchi Kwa kuwapumbaza watoto ,vijana na wazee


MTU ukiona hataki utumie Akili zako Bali hisia lazima akutawale Leo kesho daima.
Ongezea na kubeti imewawehusha watoto na wanakuwa nazo
 
Utumwa gani hapo. Hiyo salary hata daktari hapati na ndio wanaenda kupewa tena kwenye mazingira mazuri, haki zinazingatiwa, bima, mapumziko, na mkataba unaovunjwa au wenye kikomo.

Kuna mmoja namjua ameenda Israel kakaa mwaka karudi na some few millions kwa diploma yake ya kilimo kutoka LITA. Kaja wiki kadhaa kabla ya mashambulizi ya Hamas alikuwa kwenye ufugaji.
Vipi kama ingekua wanaenda kufanya kazi Saudi Arabia au nchi yeyote ya Kiarabu,unge comment hivi hivi?
 
Daah.bora ningekuwa Kenya.
Samia nae mbona haoni hizi fursa jamani tuna nini sisi?

Ila wabongo tunadharau sana. Leo milioni nne tunaita utumwa?. Huo mshahara hara Assistant Lecture haipati labda Dr mwenye PhD. Acha wake ya wakapate fursa.
Halafu kutwa wanasema nauza kitanda
Mara mshahara wa laki 3 mwingi
Ila waswahili ni maskini jeuri
 
Vipi kama ingekua wanaenda kufanya kazi Saudi Arabia au nchi yeyote ya Kiarabu,unge comment hivi hivi?
Uarabuni mbona mbali sana, tuanzie Tanzania. Kama unakubali daktari kulipwa 1.5M kwa mwezi, kwanini ukatae kibarua kulipwa milioni 4 kwa mwezi Israel?

Kuna Watanzania wapo Dubai wanafanya biashara na ajira. Kuna vinyozi, wafanyakazi wa ndani na walinzi wapo Oman na Dubai. What's special with Saudi Arabia?
Kuna kazi uko umeona na renumeration ulete hapa tujadili, maana sina mtu yeyote ameenda uko na mazingira yao ya kazi siyajui.
 
Back
Top Bottom